KATI YA MANENO AMBAYO WATU WENGI HUCHANGANYA NI πππnini kinaanza na kipi kinamalizia na je vina umuhimu gani?
Sasa leo natamani Mungu afungue akili yako,atoe Giza lote la kiroho na uelewa ujumbe huu.
NEEMA, hii Ni zawadi ambayo anapewa mtu asiyestahili kupewa.
Mfano; mfano Mara nyingi mtu akikosea hustahili hukumu.
Ona hiiππ
Warumi 6:23
[23]Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; ..........
Mwanadamu baada ya kuanguka dhambini alistahili kufa, tena kifo Cha milele, badala yake Yesu alkuja kufa kifo Cha milele Kama mbadala, yeye alishinda kifo kwa sababu yeye Ni Mungu, hivyo tukifa Leo tukiwa tumempokea Yesu Kama Bwana na Mwokozi wa Maisha Yetu tunakuwa Kama tumelala, siku akija tutaamushwa na kumlaki mawinguni.
Hiyo ndiyo maana ya Neema, kwa maana nyingine hatukustahili kuokolewa lakini tukaokolewa hii Ni Neema 100% Wala si nguvu zetu Wala matendo yetu.
Hata nuhu hakustahili kuokolewa, lakini kwa kuwa alikuwa angalau mwenye haki kuliko wenzake akapata Neemaππππ Ona hii
Mwanzo 6:7-8
[7]BWANA akasema, Nitamfutilia mbali mwanadamu niliyemwumba usoni pa nchi; mwanadamu na mnyama, na kitambaacho na ndege wa angani; kwa maana naghairi ya kwamba nimewafanya.
[8]Lakini Nuhu akapata neema machoni pa BWANA.
Ndiyo maana Paulo anasemaπππ
Waefeso 2:5
[5]hata wakati ule tulipokuwa wafu kwa sababu ya makosa yetu; alituhuisha pamoja na Kristo; yaani, tumeokolewa kwa neema.
IMANI, Neema Ni bure kwa kila Mwanadamu anayekubali kumpokea Yesu Kama Bwana na mwokozi wa maisha yake, Lakini sehemu ya Mwanadamu Ni moja Ni kufanya uamuzi wa kuamini hiyo Neema, na kufuata kile ambacho Yesu anataka ufanye.πππOna hii
Warumi 10:9
[9]Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka.
Imani Ni silaha kubwa Sana ya mlei katika ulimwengu wa roho,,, ndiyo maana neno linasemaπππ
Waebrania 11:6,
[6]Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.
Tunza Imani yakoππ
MATENDO,, Baada ya kuikubali Neema utakuwa na Imani katika maisha yako, lakini pamoja na Imani hiyo lazima pawepo na matokeo ya Imani,
Rafiki yangu hakuna Imani isiyo na matunda na matunda Haya hutokana na roho mtakatifu. Ona hiiπππ
Yakobo 2:18,21-22
[18]Lakini mtu atasema, Wewe unayo imani, nami ninayo matendo. Nionyeshe imani yako pasipo matendo, nami nitakuonyesha imani yangu kwa njia ya matendo yangu.
[21]Je! Baba yetu Ibrahimu hakuhesabiwa kuwa ana haki kwa matendo, hapo alipomtoa Isaka mwanawe juu ya madhabahu?
[22]Waona kwamba imani ilitenda kazi pamoja na matendo yake, na ya kwamba imani ile ilikamilishwa kwa njia ya matendo yale.
Hivyo Imani haiwezi kukamilika pasipo matendo πππ
Mwandishi yakobo anahitimisha kwa kusema kwamba Imani bila matendo imekufa(Yaani kwa maana nyingine bila matendo huna Imani, maana Imani tutaiona tu kwa matendo yako)πππOna hii
Yakobo 2:17,26
[17]Vivyo hivyo na imani, isipokuwa ina matendo, imekufa nafsini mwake.
[26]Maana kama vile mwili pasipo roho umekufa, vivyo hivyo na imani pasipo matendo imekufa.
Hitimisho Ni hivi Neema huzaa Imani kupitia uzoefu wa Roho mtakatifu na Imani huzaa matendo Kama matunda ya roho mtakatifu.....KUELEWA SOMO HILI VIZURI INAHITAJI UONGOZI WA ROHO MTAKATIFU, UKISOMA KWA NGUVU ZAKO HUTAELEWA KAMWE......
Mimi Ni Pr Sanida Musa, kwa masomo mengi ya kiroho bonyeza link hii chiniπππ
https://youtu.be/nEEwlxuzX1I
Njoo Instagram kwa Pastor-Sanida-Musa wasap kwa 0787935914.
Mungu atubariki sote. Usikose SoMo lijalo,,,,, "UKWELI KUHUSU KUOKOKA"
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment