» » KESHA LA ASUBUHIJumanne 23/02/2021

*HAKUNA CHA KUOGOPA*

*Wakifanya imara roho za wanafunzi na kuwaonya wakae katika ile Imani, na ya kwamba imetupasa kuingia katika ufalme wa Mungu kwa njia ya dhiki nyingi.* Matendo ya Mitume 14:22 

☄️ Mungu humaanisha kuwa tukimtumaini Yeye tutanufaika na wema wake. Huweka mbele yetu siku kwa siku na tunapaswa kuwa na macho na uwezo wa utambuzi ili kuvichukua vitu hivi. Haidhuru ni mkuu na wa utukufu kiasi gani ukombozi mkamilifu kutoka katika uovu tutakaoupata tukifika mbinguni, haikusudiwi kwamba vyote vihifadhiwe hadi wakati wa wokovu wa mwisho. Mungu huuleta katika maisha yetu ya sasa.

☄️ Tunahitaji kujenga imani kila siku kwa Mwokozi aliyepo sasa. Tukiamini katika uweza ulio nje yetu na zaidi yetu, tukitendea kazi imani katika msaada usioonekana na uweza unaosubiri dai la wenye uhitaji na tegemezi, tunaweza kutumaini katikati ya mawingu hali kadhalika katikati ya mwanga, tukiimba juu ya wokovu wetu wa sasa na furaha ya sasa ya upendo Wake. Maisha tunayoyaishi sasa lazima yawe kwa imani katika Mwana wa Mungu. 

☄️ Maisha ya Mkristo ni mandhari ya mchanganyiko wa ajabu wa huzuni na furaha, kukatishwa tamaa na matumaini, hofu na ujasiri. Kutakuwepo na kutokuridhishwa kwingi na nafsi kadiri atazamapo moyo wake mwenyewe ukiwa umekazwa sana, umefura kwa tamaa inayoonekana kubeba yote mbele yake, na kisha hufuata majuto na huzuni na toba, ikifuatiwa na amani na furaha zilizofichwa ndani, kwa kuwa anajua, kwa kadiri imani yake inavyoshikilia ahadi zinazofunuliwa ndani ya Neno la Mngu, kwamba ana upendo unaosamehe wa Mwokozi mstahimilivu. Na hutafuta kumleta huyo Mwokozi katika maisha yake, na kushikamana na tabia yake. 

☄️ Ni mafunuo haya, mavumbuzi haya ya wema wa Mungu, yanayofanya nafsi iwe nyenyekevu na kuisababisha kupaza sauti katika shukrani, “lakini ni hai; wala si mimi tena, bali Kristo yu hai ndani yangu” (Wagalatia 2:20). Tuna sababu ya kufarijiwa. Majaribu makali ya nje yanaweza kuisonga nafsi ambayo Yesu hukaa ndani yake. Hebu tumgeukie kwa ajili ya faraja aliyotupatia katika Neno lake. 

🔘 *Kijito cha chini cha matumaini na faraja chaweza kutuangusha, lakini Vijito vya juu vinavyoujaza mto wa Mungu vimejaa sana na haviwezi kukauka. Mungu angependa usitazame katika chanzo cha mateso yako na kumwangalia Yeye aliye Mmiliki wa nafsi, mwili, na roho. Yeye ni mpenzi wa nafsi. Anaijua thamani ya nafsi. Yeye ni mzabibu wa kweli na sisi ni matawi. Hatutalishwa kiroho mpaka pale tu tunapoupata toka kwa Yesu ambaye ni uzima wa nafsi.*

*MUNGU AKUBARIKI SANA*👮‍♂️

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...