(Imeandaliwa na Mch E. Kasika, kama Somo la Ufafanuzi wa Utimilifu wa Unabii kwa wanadarasa)
TAFAKARI YA MATH 24; LUKA 21; 2WATHESO 2:1-4; UFUN 13:11-18
A. KWA NINI KUJADILI MADA HII TENA?
Kwa kuwa jamii imetikishwa na hoja ya kuwepo kwa msisitizo wa kufanyiwa chanjo dhidi ya Janga la Corona,
chanjo inayoonekana kulazimishwa na kwamba kwa wasioipenda wawekewe vikwazo vya kimafao na kikomo
cha uhuru kusafiri; Na kuwa baadhi ya nchi zilizotekeleza agizo hili zimesitisha zoezi hili kutokana na madhara
mchanganyiko yaliyoonekana kuhusishwa na chanjo hiyo; na kwa kuwa watu wengi wamekuwa na hofu
kuhusu kinachoendelea ulimwenguni, wengine wamekata tamaa na maisha na majukumu ya kuishi wafanyayo
kwa kushindwa kujua kitakachozaliwa na kesho yake. Wakati huo huo wapo wengine wanaotumia muda mrefu
kumwomba Mungu aingilie kati dhidi ya haya majanga, lakini kadri wanavyo muomba Mungu, majibu ni kuona
ongezeko la majanga kama siyo ongezeko la wanaokufa. Katika mkanganyiko huu wa kutokujua
kinachoendelea na kinachofuata kesho, wengine wameanza kuwa na mashaka na kinachoelezwa ndani ya
Biblia, tendo linalopelekea kuwafanya wawe na mashaka na mamlaka na uwezo wa Mungu.
Kutokana na maswali watu wanayojiuliza bila kupata majibu sahihi, hasa wanaotumia Biblia na unabii
wake kama nuru inayoangaza mahali penye giza, kama ilivyoandikwa katika 2Petro 1:19-21, lakini majanga
haya na hasa athari yake ya ongezeko la vifo, wamejitokeza baadhi ya waumini katika Maandiko Matakatifu,
Biblia, ambao wanatafsiri majanga haya kwa kuyahusianisha na MAREJEO YA KRISTO, wakiyahusinisha na
unabii wa Ufunuo 13:14-18. Kwa kuwa kuna wengi wasioelewa vizuri unabii wa Biblia, hasa wa kitabu cha
Daniel; Ufafanuzi wa Yesu mwenyewe katika vitabu vya Injili; ufafanuzi wa Mtume Paulo na Petro na Unabii
wa mtiririko wa matukio haya uliofunuliwa kwa lugha ya mifano katika kitabu cha Ufunuo, kwa maombi mengi
na kwa kuvilinganisha vitabu hivi vyote, Mungu ameniwezesha kufanya Muhtasari huu ili kuwasaidia
waliokata tamaa au wanaoendelea kuchanganywa. Kwa kuwa ni muhtasari mrefu kidogo inakubidi msomaji
upange muda mzuri wa kuketi na kujifunza kilichoandikwa hapa, pia ukimwomba Mungu akuthibitishie kuwa
maelezo haya ni ya kweli ni uendelezaji wa wazushi. Mwalimu wako wa mwisho anatakiwa awe Mungu. Mimi
nimeandika kama mwanadamu katika lugha ya kibinadamu tu. Mungu atakufunulia katika lugha ya rohoni.
Hivyo jisikie kunyenyekezwa na Mungu, wala siyo na maandishi haya. Mungu akikueleza kuwa kilichoandikwa
ni cha kweli, usisite kukifanyia kazi kwa kupngozwa na kanuni zilizofafanuliwa. Huo ndio uhuru ulio nao
msomaji. Miongoni mwa matukio yasiyoeleweka kwa wengi na yanayochanganya kuhusiana na jinsi unabii wa
Biblia ilivyoandikwa ninyafuatayo:
1. Chukizo la Uharibifu lililonenwa na nabii Daniel, ( Math 24:15,16). Mtekelezaji wake ni nani?
2. UKENGEUFU uletwao na mtu wa kuasi, mwana wa uharibifu, (2Wathes 2:1-4). Je hili tukio ndilo lililonenwa
na nabii Danieli au ni jingine? Kama ni lile lile mbona pia linamtaja mpinga kristo? Je, Chukizo la Uharibifu na
Mpinga Kristo, mtekelezaji ni yule yule au ni wawili tofauti?
3. Mnyama atokaye katika nchi, atajwaye na mtume Yohana katika a kitabu cha Ufunuo 13:11-18, anaye
elezewaa kuwa na na pembe mbili mfano wa mwanakondoo lakini akinena kama joka! Je, huyu ni tofauti na
Mpinga Kristo, au Chukizo la Uharibifu, au ni yule yule ila lugha iliyotumika ndiyo tofauti? Kama ni mnyama
kweli anawezaje kunena kauli za kuamrisha wanadamu kufuata maagizo yake?
4. Majanga mbalimbali, nguvu za mbinguni kutikisika na kusababisha hofu kwa wanadamu kama matokeo
ya kushindwa kujua kinachofuata na kuingiliana na hayo mengineyaliyoandaliwa kutendeka na au
yanayotendeka, yanayoelezwa katika vitabu vya Injili, Yesu alipokuwa akifafanua viashiria vya kutambulisha
ukaribu wa wakati wa kukomesha maisha ya dhambi na uovu wa dunia, ataruhusu. Haya yameandikwa zaidi
katika Mathayo 24 na Luka 21. Nguvu za utendaji wa Mungu zitatikisa nguvu za mamlaka na utendaji wa
ubunifu wa wanadamu, ili mwanadamu aone umuhimu wa kuelewa kuwa kuna mwenye mamlaka kumzidi
yeye; tena kwamba anatakiwa kumtambua na kumwamini ili adiangamizwe. Kwa kuwa mwanadamu mwenye
mamlaka na mjeuri ataonyesha moyo wa kiburi, Mungu ataruhusu dhiki, mateso na vifo kiasi cha
kumfundisha kuuelewa uwezo wa mungu.
2
5. Shule hii inayotupitisha katika mazingira magumu katika imekusudiwa kumwelimisha mwanadamu atambue
Vipindi viwili muhimu: (1) MWANZO WA SIKU ZA MWISHO- KABLA YA MAREJEO; (2) MWANZO WA KIZAZI CHA
MWISHO- KINACHOTANGAZA KUJIANDAA KWA MAREJEO YA KRISTO.
Wakati Ishara katika dunia na majini na angani zikiendelea, Mungu, kwa mujibu wa kauli ya unabii huo
anawaambia wale wamngojao wachangamke na kuinua vichwa vyao juu kwa kuwa wokovu wao umekaribia.
Huku kuchangamka na kuinua vichwa juu, kumeambatana na uwajibikaji maalumu watu hawa watakiwao
kufanya. Uwajibikaji ni wa aina mbili: (1) Kuhakikisha kuwa dhambi za anayetaka kuokolewa zimesamehewa
na Mungu, kutokana na kutumia muda kila siku kutubu, kuungama na kuombwa kujazwa na Roho Mtakatifu;
( 2) Kumtumikia Mungu kwa kuhubiri Habari njema ya Ufalme wa Mungu kwa wote ulimwenguni, ili
wasiomjua Mungu na utendaji wake nao wamjue na kumwamini. Matendo haya yataenda sambamba na
utimilifu wa dalili na ishara zingine, katika mazingira mazuri na magumu. Hii Mada imeandikwa kwa ajili ya
kutukumbusha majukumu yetu, wale wanaosubiri marejeo ya Kristo. Ni zaidi ya kuingia makanisani na kuomba
siku 3 au wiki nzima. Ni zaidi ya kukariri ahadi za Mungu alizowapa Israeli wa zamani. Kuna jukumu kubwa
KUJIWEKA TAYARI KUONANA NA MFALME WA WAFALME NA BWANA WA MABWANA, ( Math 24:42-51).
6. Katika maandalizi haya kuna ujumbe wenye msisitizo ambao Yesu Kristo amekusudia wanadamu wote
waelezwe na waelewe waziwazi. Anataka atambulike kwa wote kuwa yeye ndiye pekee mwokozi wa wenye
dhambi, siyo Kanisa, katika sura ya Taasisi. Kwa kuwa waumini wengi wamezoea kusikia na kupokea matamko
kutoka kwa viongozi wa Kanisa kama watawala wa Taasisi hizo, na kwa kuwa wametumika kuwaombea watu
na kupona katika shida zao mbalimbali, kutii msisitizo wa kuwapuuza viongozi wa Taasisi za Kanisa itakuwa ni
changamoto nyingine. Itazua mgongano wa mitizamo na mafundisho ya kidini. Wanaomuhubiri Kristo kuwa
na mamlaka dhidi ya Kanisa kama Taasisi wataonekana kuwa ni wazushi. Uamuzi utafanywa na viongozi wa
Taasisi za Kanisa kuwashughulikia wazushi hawa wanaotaka kuwapunguzia hadhi yao ya miaka mingi. Pamoja
na kuitwa wazushi, watashtakiwa kama wachochezi wa vurugu na machafuko wakivuruga amani katika jamii
kwa kutangaza dini mpya. Hiki ndicho kilimtokea mtume Paulo na wenzake katika zama zao za kumtangaza
Kristo kama Mwokozi wa wenye dhambi. Rejea kisa katika Kitabu cha Matendo ya Mitume 24:1-9.
7. Kama matokeo ya kilele cha ushuhuda huu wa wamgonjao Kristo, huku Injili ikihubiriwa, na wakati huo huo
wakiteswa, Mungu ataingilia kati kwa kuongeza majanga yatakayo ongezeka duniani, hali itakayofanya
Wainjilisti/ watarajia marejeo na wasiotarajia marejeo, wote waishi ndani ya kipindi kigumu. Tofauti zao
zitakuwa ni ulinzi wa Mungu kwa walio waaminifu kwake, lakini siyo kuwaondolea kabisa maumivu ya aina
yotote. Kuna kukinywea kikombe kichungu kila muumini kwa namna aliyoiruhusu Mungu, isiyolazimika
kufanana au kuwa sawa na uzoefu wa mwenzake. Imebidi Utangulizi huu uanze kwanza kwa urefu huu ili
anayesoma vipengele vinavyofafanua yaliyoelezwa katika Utangulizi, awe na msingi wa kuelewa kilichomo
katika mjadala.
B. NI RAHISI KUVIELEWA VIASHIRIA?
1. Ni rahisi kuvielewa VIASHIRIA maana vimetajwa katika Matandiko. Ugumu uliopo ni kuelewa mtiririko wa
utimiaji wake.
2. VIASHIRIA vilivyotajwa na Yesu katika Mathayo na Luka, vilikuwa vikihusisha matukio ya aina mbili ya
kiunabii, yanayoonekana kijirudia:
a. Tukio la kwanza ni kukoma kwa Taifa la Israeli na mfumo wake wa kiibada, na hivyo alikomesha utoaji wa
sadaka na dhabihu, kama ilivyotajwa katika unabii wa Daniel wa majuma 70. Hili lilienda sambamba na
kukomesha Agano la kwanza ili kusudi asimamishe Agano la pili, kama tusomavyo katika Waeb sura ya 9 na
ya 10. Rejea Waeb 10:1-20 na Luka 21:20-24. Mtekelezaji ni Chukizo la Uharibifu lililonenwa na Nabii Daniel.
b. Hili tukio la kwanza liliambatana na dhiki na mateso pia kwa mitume wa Kristo kwa sababu ya kumuhubiri
kuwa ni mwokozi. Kila mmoja alikufa kifo cha mateso ya aina yake. Mitume waliandaliwa kiakili kukabiliana
na mazingira ya aina hiyo.
c. Tukio la pili lilitekelezwa pia na chukizo la Uharibifu kwa kipindi kilichoamriwa cha siku 1,260, ambacho
kilihusisha Dhiki na mateso makubwa kwa watu walioamua kumhubiri Yesu. Tukio hili la kihistoria lilichukua
siku 1, 260, sawa na unabii wa Ufunuo 12:1-6, 13-17, wa wakati, nyakati mbili na nusu wakati, au miezi 42
inayotajwa katika Ufunuo 13:1-10. Unabii huu wa siku 1,260 na wa majuma 70 au siku/ miaka 490 ni MATUKIO
3
ndani ya matukio ya unabii mrefu katika Biblia wa siku 2,300, uliotajwa katika Daniel 8:13,14, ambao ulitimia
mwaka 1844. Endelea kufuatilia mtiririko wa kifuatacho.
3. Kwa kuwa VIASHIRIA hivi vyote vingelitokea baada ya Yesu kupaa mbinguni na vitajirudia kabla hajarejea
mara ya pili kuwachukua watakatifu wake, umakini unahitajika kwa kila asomaye na kila asikiaye maneno ya
unabii huu ili ayashike yaliyoelezwa kuwa yatakuwa ni ushuhuda wa kutangaza ukaribu wa marejeo yake. Rejea
Ufunuo 1:1-3.
4. VIASHIRIA hivi vinaelezea MATUKIO ya aina mbili; matukio yamayohusiana na KUTAMBUA UKARIBU WA
MAREJEO YA KRISTO:
a. Viashiria vya Kutambua mwanzo wa Siku za mwisho kwa mujibu wa mafunuo ya unabii. Kukomeshwa kwa
mamlaka ya mnyama, kwa awamu ya kwanza, ambako ndiko mwisho wa unabii wa siku 1,260 kunatambulisha
MWANZO WA SIKU ZA MWISHO. Mateso haya yaliyoanza mwaka 538BK hadi mwaka 1798, yakitekelezwa na
muunganiko wa Serikali ya Kirumi,( iliyotawala dunia zama hizo), pamoja na mamlaka ya Kanisa Katoliki,(
lililoungana na serikali kubadili baadhi ya Maandiko ya Biblia na umuhimu wake )
b. Sambamba na kukomeshwa kwa muda kwa mamlaka ya utendaji wa mnyama, uliohusisha dhiki, kulitokea
ishara zingine katika anga zikihusisha jua na nyota na matukio mengine ya kutisha, matukio yaliyoendana na
mwisho wa unabii wa Daniel 8:13,14 wa siku 2,300. Mwisho wa unabii huu haukuwa kurudi kwa Kristo duniani
kuchukua watakatifu wake, bali kulikuwa ni MWANZO WA HUKUMU YA UPELELEZI NA MAOMBEZI MAALUMU
AFANYAYO KRISTO KWA AJILI YA WATEULE WAKE, KABLA YA KUFUNGWA MLANGO WA REHEMA. Huduma hii
ikimalizika na mlango wa rehema kufungwa ndipo atakaporudi kuwachukua walio waaminifu kwake.
c. Kauli za Yesu katika Mathayo 24:29 na Luka 21:25,26 zinaonekana kujirudia. Zilitokea baada ya ile dhiki ya
mnyama iliyokomeshwa 1798. Zitajirudia tena muda mfupi kabla ya marejeo ya Kristo. Hii awamu ya pili ndiyo
inayohusisha Unabii wa Ufunuo 13:11-18.
C. VIASHIRIA VYA KUKARIBIA KWA MAREJEO NI VIPI?
1. VIASHIRIA hivi vinahusisha pia Ishara angani na nguvu za mbinguni kutikisika, mambo yatakayosababisha
hofu ya mataifa na watu kuvunjika mioyo kwa hofu. Hii ni kwa mujibu wa Luka 21:25-33.
2. Udhihirisho wa CHUKIZO LA UHARIBIFU, lililonenwa na nabii Daniel, utatokea tena, siyo kwa kipindi kirefu
cha kiunabii bali kipindi kifupi cha kuwatesa tena walio waaminifu kwa Mungu, ikiwa kumfunua mnyama
anenwaye katika Ufunuo 13:11-18, kuwa siyo mnyama halisi bali mamlaka ya kibinadamu yaliyojiamuria
kubadili MFUMO WA IBADA KWA MUNGU ili sasa mwanadamu aabudiwe kama Mungu kwa matarajio kuwa
atakomesha majanga yanayoendelea duniani. Huyu ndiye Mpinga Kristo na mtu atendaye kama SIRI YA KUASI,
kwa mujibu wa 2Wathesolanike 2:1-11. Hiki ndicho kilichoelezwa na Kristo katika Mathayo 24:15-25.
3. Mateso ya mamlaka haya ya kidini yatatanguliwa na kudhoofisha akili za wanadamu ili kuwapunguzia uwezo
wa kufanya maamuzi ya akili kutokana na akili zao kuharibiwa na mtindo wa maisha. Katika Ufunuo 13:16,17
kumetajwa kutiwa chapa katika kipaji cha uso- yaani kudhoofisha ufahamu na akili. Vitekelezaji ni vingi
vitakavyotumika. Katika Luka 21:34,35, kumetajwa: Ulafi; Ulevi na Masumbufu ya Maisha haya. Katika Math
24: 37-39, kumerudiwa yaliyotajwa katika Luka na kuongeza ngono/ kuoa na kuolewa.
4. Kikwazo kikubwa kitakachochoea mateso haya ni suala la uchumi. Tamko la kutiwa chapa katika kipaji cha
uso, na katika mkono wa kuume, litajwalo katika Ufunuo 13:16,17, na kwamba mtu yeyote asiyeafikiana na
masharti ya vigezo vikivyowekwa, asiweze kununua au kuuza mpaka atii hivyo, vitachochea ugumu wa maisha
na kuwafanya watu washindwe kuishi maana mali zao zimewekewa vikwazo.
5. Ni muhimu kufahamika kuwa vikwazo hivi havitatangazwa na serikali za kawaida ulimwenguni. Kwa mujibu
wa unabii wa Ufunuo 13:14;15, mwenye kutoa idhini ili serikali ya kawaida itangaze na kutekeleza haya inabidi
awe huyu mnyama; mwanadamu aliyeanza kunitambulisha kiuwezo duniani kuwa anayo mamlaka ya
kubadilisha matamko ya Biblia. Atafanikisha hili kwa kuidhinisha Biblia aliyoitafsiri yeye isiyo na masharti
magumu kama ile ya kwanza.
4
6. Tunachosubiri kusikia kikitangazwa na Mamlaka ya kidini ya Kanisa Katoliki ni kuirudisha ile amri ya kila
anayeabudu amwabudu Mungu siku ya Jumapili, siyo siku ya Sabato ya Jumamosi au nyingineyo. Asiyekubali
agizo hili kwa hiari atalikubali kwa mateso, kukiwemo kuwekewa vikwazo vya kiuchumi. Hili Tamko Tamko
bado halijatolewa rasmi na Kanisa Katoliki ijapokuwa muda sio mrefu litatangazwa hadharani. Kutangazwa
kwa Tamko hili ndiko tuakuwa kiashiria cha kuelewa kuwa dunia ya dhambi karibuni sana itakomeshwa na
Mungu. Hii ni kwa sababu Tangazo Tangazo hili litatambulisha mwanzo wa KIZAZI CHA MWISHO.
7. Kabla ya Tamko hili kutolewa, idhini imekwisha kutolewa na Kanisa Katoliki ya ndoa za jinsia moja na ngono
ya aina yoyote, ili maisha yafanane na ya siku za Nuhu na za Lutu. Hizi zote ni juhudi za kudhoofisha fahamu
za watendao, ikienda sambamba na kukosea kufanya maamuzi sahihi, kiasi cha kujikuta wamejiingiza katika
utumwa wa dhambi ulio mgumu kuacha, ( Hosea 4:10-14).
8. Kwa mujibu wa Math 24:24, utendaji wa mpinga Kristo unatumia pia uwezo mwingi, zikiwemo ishara na
maajabu, ili kufanikisha udanganyifu wake. Udanganyifu huu utahusisha ibada bandia, imayoweza kutangaza
Uponyaji usiotokana na Mungu. Wengi watamwendea ili kuombewa kwa matatizo mbalimbali waliyo
nayo. Aidha miujiza hii inaweza kutumia ubunifu wa kibinadamu. Miongoni mwake ni kuleta magonjwa kwa
wanadamu ma kuyaondoa kwa kutumia mbinu zile zile alizotumia kuyaingiza.
Ni katika muktadha huu hoja ya chanjo inayobishaniwa kwa muda mrefu sasa na zingine zinazoweza kuletwa
zaweza kuwa ni mojawapo ya mbinu zake. Ishara za aina hii zimekuwepo katika historia ya wanadamu na
zinaweza kujitokeza tena, ila siyo kiashiria cha karibia na marejeo ya Kristo. Ni muhimu kujua utofauti uliopo.
9. Kiunabii hizi ndizo ishara za kuonya watu wa Mungu lakini kutokana na kuleweshwa matendo haya ya zinaa,
yaitwayo, " Ibada ya Sanamu", waabuduo wengi watatekwa na mtindo huu wa maisha, ili uwafikishe kwenye
ghadhabu ya Mungu, ( Wakolosai 3:5-11).
10. Katika Ufunuo 14: 9,10, kumetolewa onyo maalumu na Mungu kwa mtu yeyote atakayemsujudia yule
mnyama au sanamu yake, na kupokea chapa katika kipaji cha uso wake au katika mkono wake. Adhabu ya
Mungu imetangazwa dhidi yake. Hapa ni muhimu kuelewa kuwa SANAMU YAKE, inahusisha pia MATENDO YA
IBADA YA SANAMU, yaliyoelezwa katika Waefeso 5:1-8, na Wakolosai 3:5-10. Ni zaidi ya kuabudu siku ya
Jumapili. Hivyo kuabudu siku ya Sabato, wakati mwenye kuabudu akidumisha ibada ya Sanamu, hatakuwa
tofauti na Wayahudi walimwabudu Mungu siku ya Sabato, lakini watakataa kumtambua na kumwamini Yesu
Kristo kama mwokozi wa wenye dhambi, aliyekomesha Agano la kwanza. Mwisho wake ni kuangamizwa sawa
na wenye dhambi wengine waliokataa kutii maagizo yote ya Mungu.
D. WAMSUBIRIO KRISTO WANALO JUKUMU LOLOTE AU YOTE HUFANYWA NA MUNGU?
1. Jukumu lao la kwanza ni kudhihirisha walivyo mashahidi wa Kristo kupitia mtindo wao wa maisha, (Matendo
1:8; Math 24:9; Luka 21:10-13).
2. Udhihirisho huu ni matokeo ya kujazwa na Roho Mtakatifu atakayeongea ndani yao katikati ya wawatesao,
( Luka 21:14-18).
3. Watajazwa Roho Mtakatifu kutokana na kukataa kupokea chapa katika kipaji cha uso au katika mkono,(
Ufun 14:9,10). Hawatakubali kuiga mitindo ya maisha ya ulimwengu huu itakayokuwa inahimizwa kimataifa,(
Warumi 12:2).
4. Wataendelea na kuvipiga vita vizuri vya imani kwa kumhubiri Kristo kama Bwana na Mwokozi wa wenye
dhambi na kwamba hakuna mwanadamu aliyepewa jukumu hilo, (Math 24:13,14; Matendo 4:7-12; Wafilipi
1:27-31).
5. Haya yote watayafanya wakidumu pamoja katika maombi na kujifunza Maandiko ili waishi kwa nguvu ya
ukweli wa Injili,(Luka 21:36;Math 24:42-44).
6. Pamoja na maombi ya pamoja mwandishi aliyevuviwa, aitwaye Ellen White, yanatushauri kwa kusisitiza
kuwa jukumu la kila mtu binafsi ni kutunza vyema makazi ambayo Mungu amempatia. Hebu dhambi isitawale
katika mwili wako ufao, na usitumie vibaya nguvu za kimwili ambazo Mungu amekupatia, bali tunza kwa
upendo sana nguvu zako, ukiweka tumaini lako lote kwa Mwokozi mkamilifu. Kwa kufanya hivyo
tutapata nguvu katika nguvu zake. Nguvu hizi zitatuwesha kukabiliana na upinzani toka kwa wahudumu wa
Kanisa kadri unavyoishi kuifikilia na kuwasilisha kwa wengine, kiwango cha juu cha dini ya Biblia. Dharau na
5
kuzomewa, kashfa na uongo vitakufuata. Nia na maneno yako, matendo yako vitaeleweka vibaya na
kutafsiriwa vibaya na kishutumiwa. Lakini ukiendelea na kazi licha ya manyanyaso unayopata, ukifanya vema,
ukiwa mwema na mvumilivu, mnyenyekevu katika roho, mwenye furaha katika Mungu, utakuwa na mvuto.
Utapata huruma ya wale wote walio wanyofu na wenye akili. Nukuru toka Kesha la Asubuhi, kitabu cha: Leo
na Mungu,( This Day with God), cha Ellen White, uk 53.
E. HITIMISHO
Kwa kifupi haya ndiyo yaliyofunuliwa kwetu hadi sasa. Yawezekana mafunuo zaidi yakaletwa na Roho wa
Mungu kadri tunavyoishi ili tujue vizuri na kunyosha tulipojichanganya. Hivyo tunategemewa tuisikie sauti ya
Roho anapozungumza ndani yetu kupitia nguvu ya maombi ya pamoja huku tukimtumikia Mungu.
Pamoja na ukweli kwamba shetani atatumia majeshi yake ya manabii wa uongo kutumia ishara na maajabu,
na anaweza kutumia wanasayansi kugundua magonjwa ma dawa za kuyatibu, badala ya kutumia muda
mwingi kujadili mbinu za Ibilisi na jeshi lake, ni busara kutumia muda mwingi kujifunza kuzijua na kuzitumia
mbinu alizotuagiza Yesu na kwa kutumia nguvu hizo kumwambia shetani, " Nenda zako shetani...", ambapo
kwa kumkemea, Mungu atawatuma malaika wake waje kuwatumikia waliobakia kuwa waaminifu kwake, (
Math 4:11; Luka 21:17,18).
KAMA UFAFANUZI HUU UMEKUSAIDIA KUUJUA WAKATI TULIOMO na UWAJIBIKAJI UTUPASAO, USISITE
KUMSHIRIKISHA MWENZAKO. Kama umepata ugumu mahali kokote waweza kuwa huru kuwasiliana na
mwandishi wa Muhtasari huu kwa simu hii- 0764 151 346
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment