» » KESHA LA ASUBUHIJumatano 24/02/2021

*JINSI YA KUIONDOA HATIA*

*Mtu mbaya na aache njia yake, Na mtu asiye haki aache mawazo yake Na amrudie BWANA, Naye atamrehemu; Na arejee kwa Mungu wetu, Naye atamsamehe kabisa.* Isaya 55:7

📚 Dada yangu mpendwa, nina uthibitisho kwamba Mungu anakupenda, na kwamba Mwokozi wa thamani aliyejitoa kwa ajili yako ili upate kuokolewa hatakusukuma toka kwake kwa sababu unajaribiwa, na katika udhaifu wako alipata ushindi...

📚 Sasa usijisumbue mikononi mwa Yesu mpendwa, bali lala kwa kutumaini katika imani. Anakupenda, anakujali, anakubariki, na atakupa amani na neema yake. Anakwambia, “Umesamehewa dhambi zako” (Luka 5:23). Ninakwambia Yesu anatupenda ijapokuwa tunafanya makosa na kumsaliti katika dhambi. Ataachilia makosa yetu, atatusamehe tena kwa wingi. Jipatie nafsini mwako ahadi tamu za Mungu... 

📚 Usiutazame unyonge wako na kuuangalia ukamilifu wa Kristo. Hatuwezi kujitengenezea haki kwa ajili yetu wenyewe. Yesu anayo mkononi mwake vazi safi la haki naye ataliweka juu yetu. Atasema maneno matamu ya msamaha na ahadi. Naye huwapatia nafsi zenye kiu chemchemi ya maji ya uzima, ambapo tunaweza kuburudishwa. Anatusihi tuje kwake na mizigo yetu yote, huzuni zetu zote, naye husema tutapata pumziko. Hivyo tunapaswa kuamini kwamba anatoa msamaha, na tunapaswa kuonesha imani yetu kwa kubaki katika pendo lake. 

📚 Hisia hii ya hatia ni lazima isalimishwe chini ya msalaba wa Kalwari. Hisia za kuwa mwenye dhambi zimetia sumu katika vijito vya maisha na furaha ya kweli. Sasa Yesu anasema, “Isalimishe yote kwangu; nitaichukua dhambi yako, nitakupa amani. Usivunje tena heshima yako binafsi, kwa kuwa nimekununua kwa gharama ya damu yangu mwenyewe. Wewe ni wangu, nia yako dhaifu nitaitia nguvu; hatia yako ya dhambi, nitaiondoa.” 

📚 Kisha geuza moyo wako wenye kujaa shukrani, kwa kutetemeka kwa mashaka, na shikilia tumaini lililowekwa mbele yako. Mungu hupokea moyo uliovunjika wenye toba. Hukupatia msamaha bure. Hutoa nafasi kukuasili katika familia yake kwa neema yake kusaidia udhaifu wako, na Yesu mpendwa atakuongoza hatua kwa hatua, ikiwa tu utaweka mkono wako katika mkono wake na kuruhusu akuongoze. 

🔘 *Zitafute ahadi za thamani za Mungu. Ikiwa Shetani anarusha vitisho mbele ya fikra zako, geuka toka kwavyo na kuzishikilia ahadi.*

*TAFAKARI NJEMA SANA*👮‍♂️

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...