*KUWAPO HAJA YA KUTENGANA:*
➡️Baada ya pambano la muda mrefu na kali, waaminifu wachache wakaamua kuuvunjilia mbali
muungano wa aina yo yote na kanisa lile lililokuwa limeasi endapo lingekataa kuachana na
[mafundisho yale ya] uongo pamoja na ibada ya sanamu.
➡️ Wakaona ya kwamba kujitenga kwao
kulikuwa ni kwa lazima kabisa kama wangetaka kulitii neno la Mungu. Hawakuthubutu
kuyavumilia mafundisho yale ya uongo ambayo yalikuwa na hatari ya kuzifisha roho zao, na
kuweka mfano ambao ungehatirisha imani ya watoto wao, na watoto wa watoto wao.
➡️Kujipatia
amani na umoja huo walikuwa tayari kufanya maridhiano yo yote ambayo yangepatana na
uaminifu wao kwa Mungu; lakini walijisikia kwamba ingekuwa ni gharama kubwa mno hata
kuweza kuipata amani kwa kuitupilia mbali ile kanuni. Endapo umoja ule ungeweza kupatikana
tu kwa kufanya maridhiano juu ya ile kweli na haki, basi, ilikuwa ni afadhali kuhitilafiana nao,
na hata kupigana nao vita.
*👉🏿Ingekuwa heri kwa kanisa na kwa ulimwengu huu kama kanuni zile zilizowasukuma watu
wale waliosimama imara zingefufuliwa tena katika mioyo ya wale wanaojiita watu wa Mungu.*
➡️Kuna hali ya kuogofya ya kutokujali kuhusu mafundisho yale ya dini ambayo ndiyo nguzo za
imani ya Kikristo. Maoni haya yanazidi kupata nguvu, kwamba, kwa vyo vyote vile,
mafundisho hayo sio ya maana sana. Mmomonyoko huo wa maadili unaitia nguvu mikono ya
vibaraka wa Shetani, kiasi kwamba nadharia za uongo pamoja na madanganyo ya kufisha
ambayo yalihatirisha maisha ya waaminifu katika vizazi vile vilivyopita walipoyapinga na
kuyafichua, hivi sasa yanaangaliwa kwa upendeleo na maelfu ya wale wanaodai kwamba ni
wafuasi wake Kristo.
➡️Wakristo wale wa kwanza walikuwa ni watu wa pekee kweli kweli. *Mwenendo wao usio na lawama pamoja na imani yao isiyoyumba vilikuwa kemeo la kudumu lililoivuruga amani ya
mwenye dhambi.* Ingawa wao walikuwa ni wachache tu kwa takwimu, bila kuwa na utajiri,
wala daraja, au vyeo vya heshima, *walikuwa tishio kubwa kwa waovu ko kote kule ambako
tabia na mafundisho yao yalijulikana.* *Kwa ajili hiyo walichukiwa na waovu, kama vile Habili
alivyochukiwa na Kaini aliyekuwa hamchi Mungu.* *Kwa sababu iyo hiyo Wayahudi walimkataa na kumsulibisha Mwokozi - kwa kuwa usafi na utakatifu wa tabia yake ulikuwa kemeo la
kudumu kwa uchoyo na ufisadi wao.*
➡️Tangu siku zile za Kristo mpaka sasa wanafunzi wake
waaminifu wameamsha chuki na upinzani toka kwa wale wanaozipenda na kuzifuata njia zile za
dhambi.
*Kwa jinsi gani, basi, injili inaweza kuitwa ujumbe wa amani?* Isaya alipotabiri juu ya
kuzaliwa kwa Masihi, alimpa cheo cha *“Mfalme wa Amani.”* Malaika wale walipowatangazia
wachungaji wale wa kondoo kwamba Kristo alikuwa amezaliwa, waliimba wimbo juu ya
nyanda zile za Bethlehemu, wakisema: *“Atukuzwe Mungu juu mbinguni, na duniani iwe amani
kwa watu aliowaridhia.” Luka 2:14.*
➡️Yaonekana kana kwamba pana kinyume [mgongano] kati
ya tangazo hilo la kinabii na maneno haya ya Kristo: *“Msidhani ya kuwa nimekuja kuleta amani
duniani; la! sikuja kuleta amani, bali upanga.” Mathayo 10:34.*
➡️Lakini yakieleweka vizuri,
yote mawili, yanapatana. *Injili ni ujumbe wa amani.* *Ukristo ni mfumo ambao kama
ungepokewa na kutiiwa, basi, ungeweza kueneza amani, umoja, na furaha ulimwenguni kote.*
➡️Dini yake Kristo itawaunganisha katika undugu wa karibu sana wale wote wanaoyapokea
mafundisho yake.
👉🏿Ulikuwa ni utume wa Yesu kuja kuwapatanisha wanadamu na Mungu, na
hivyo kila mmoja na mwenzake. Walakini ulimwengu wote uko chini ya utawala wa Shetani,
adui yule mchungu sana wa Kristo. Injili inawaonyesha kanuni za maisha ambazo zinagongana
kabisa na tabia na tamaa zao, nao wanafanya maasi dhidi yake. Wanauchukia usafi wa maisha
unaozifunua na kuzishutumu dhambi zao, tena wanawatesa na kuwaangamiza wale
wanaowasisitizia madai yake ya haki, na matakatifu. *Ni kwa maana hiyo - kwa sababu
inazileta kwao kweli hizo zilizotukuzwa ambazo zinasababisha chuki na ugomvi - ndiyo
maana injili hiyo inaitwa upanga.*
➡️ Maongozi ya Mungu ya siri yanayoruhusu wenye haki kuteswa mikononi mwa waovu
yameleta utata mkubwa kwa wengi walio dhaifu wa imani. Wengine hata wako tayari
kuutupilia mbali ujasiri wao kwa Mungu ati kwa sababu anawavumilia watu wale walio waovu kupindukia kuendelea kusitawi, wakati wale walio wema na safi kabisa wanaumizwa na kuteswa
vibaya chini ya uwezo wa kikatili wa waovu.
➡️ Yawezekanaje basi, wanauliza, kwamba yule
Mmoja aliye na haki na rehema, na ambaye pia ana uwezo usio na kikomo, aweze kuvumilia
kuangalia dhuluma na ukandamizaji kama huo? Hilo ni swali ambalo sisi hatuna lo lote la
kufanya juu yake.
➡️Mungu ametupa sisi ushahidi wa kutosha wa upendo wake kwetu, nasi
hatupaswi kuwa na mashaka juu ya fadhili zake kwetu hata kama hatuelewi ulivyo utendaji wa
maongozi ya Mungu.
➡️Mwokozi, akiangalia mbele mapema, aliyaona mashaka
yatakayowalemea mioyoni mwao katika siku zao za maonjo na giza, basi, akawaambia
wanafunzi wake maneno haya: *“Likumbukeni lile neno nililowaambia, Mtumwa si mkubwa
kuliko bwana wake. Ikiwa waliniudhi [walinitesa] mimi, watawaudhi [watawatesa] ninyi.”
Yohana 15:20.*
➡️Yesu alipata mateso makali mno kwa ajili yetu kuliko ye yote miongoni mwa
wafuasi wake awezavyo kuteswa kutokana na ukatili wa wanadamu waovu. Wale wanaoitwa
kustahimili mateso makali na kuuawa kama wafia dini wanafuata tu nyayo za yule Mwana
Mpendwa wa Mungu *[Flp. 1:27-30; Ufu. 12:11; 1 Pet. 3:13-18].*
*“Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake.” 2 Petro 3:9.* Hawasahau wala hawaachi watoto
wake; bali anawaruhusu waovu kuidhihirisha tabia yao halisi, ili asipate kudanganyika mtu ye
yote anayetamani kufanya mapenzi yake kuhusu walivyo hasa.
➡️Tena, wenye haki huwekwa
katika tanuru la mateso, ili wao wenyewe wapate kutakaswa; ili mfano wao upate kuwashawishi
wengine juu ya uhakika wa imani yao na utauwa; na pia kwamba mwenendo wao thabiti upate
kuwahukumu wale wasiomcha Mungu na wale wasioamini *[1 Pet. 4:12-16; Yak 1:2-4,12; Yn.
3:19-21].*
➡️ Mungu anawaacha waovu kusitawi na kudhihirisha uadui wao dhidi yake, ili watakapokuwa
wamekijaza kikombe chao cha uovu, wote wapate kuiona haki na rehema yake katika
kuwaangamiza hao kabisa.
➡️Siku ile ya kulipiza kisasi chake inaharakisha kuja, wakati wale
wote walioivunja Sheria yake [Amri Kumi] na kuwatesa watu wake watakapopata thawabu ya
haki kwa matendo yao; wakati kila tendo la kikatili au la dhuluma dhidi ya waaminifu wake
Mungu litakapopewa adhabu kana kwamba lilikuwa limetendwa dhidi yake Kristo mwenyewe.
👉🏿Kuna swali jingine na la maana sana ambalo lingepaswa kuyashughulisha mawazo ya
makanisa ya siku hizi. Mtume Paulo anatangaza kwamba *“wote wapendao kuishi maisha ya
utauwa katika Yesu wataudhiwa [watateswa].” 2 Timotheo 3:13.* Mbona basi, inaonekana kana
kwamba mateso yamesinzia [hayaonekani] kwa kiwango kikubwa? *Sababu ya pekee ni kwamba
kanisa limefuata desturi za dunia hii, na kwa sababu hiyo, haliamshi upinzani wo wote.*
➡️Dini
iliyopo leo si safi wala si takatifu kama ile iliyoonekana katika imani ya Kikristo katika siku zile
za Kristo na Mitume wake. Ni kwa sababu tu ya kuwapo kwa roho ile ya maridhiano na
dhambi, ni kwa sababu kweli zile kuu za Neno la Mungu hazijaliwi sana, ni kwa sababu hakuna
utauwa ulio hai ndani ya kanisa, *ndiyo maana Ukristo unaonekana kana kwamba unapendwa na
watu wengi sana ulimwenguni.*
*👉🏿Hebu pawe na uamsho wa imani na uwezo ule ambao ilikuwa nao kanisa lile la kwanza, hapo ndipo itakapohuishwa roho ya mateso, na mioto ile ya mateso
itawashwa tena.*
*_MWENYEZI-MUNGU ATUSAIDIE SANA._*
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment