NENO KUU.
TRH. 11/06/2021.
MCH. MARK WALWA MALEKANA.
SOMO: JINSI YA KUAHIRISHA MAZISHI YAKO.
Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.
Mathayo 11:28
Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu;
Mathayo 11:29
Kila mtu anapenda kuishi. Je, ninawezaje kuahirisha kifo?
Kwa hiyo, kama kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti; na hivyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi;
Warumi 5:12
Je, Mungu anafurahia kifo? Au kuona watu wakifa? Hapana!
Waambie, Kama mimi niishivyo, asema Bwana MUNGU, sikufurahii kufa kwake mtu mwovu; bali aghairi mtu mwovu, na kuiacha njia yake mbaya, akaishi. Ghairini, ghairini, mkaache njia zenu mbaya; mbona mnataka kufa, Enyi nyumba ya Israeli?
Ezekieli 33:11
Je, Mungu anapenda watu wake wawe na afya njema? Ndiyo,
Mzee, kwa Gayo mpenzi, nimpendaye katika kweli.
3 Yohana 1:1
Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo.
3 Yohana 1:2
Mungu anataka watu wake wafanikiwe katika mambo yote. Kielimu, Kiroho, Kiafya, Kijamii, na kiuchumi.
Je maisha yetu kwa Mungu yakoje? Anayaonaje maisha yetu hasa?
Nitakushukuru kwa kuwa nimeumbwa Kwa jinsi ya ajabu ya kutisha. Matendo yako ni ya ajabu, Na nafsi yangu yajua sana,
Zaburi 139:14
Mungu, fikira zako zina thamani nyingi kwangu; Jinsi ilivyo kubwa jumla yake!
Zaburi 139:17
Kama ningezihesabu ni nyingi kuliko mchanga; Niamkapo nikali pamoja nawe.
Zaburi 139:18
Mungu anadumu kusema nasi kwamba;
Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu?
1 Wakorintho 3:16
Kama mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamharibu mtu huyo. Kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu, ambalo ndilo ninyi.
1 Wakorintho 3:17
Mungu hafurahii watu wake wanapoteseka.
Hata kulipokuwa jioni, na jua limekwisha kuchwa, walikuwa wakimletea wote waliokuwa hawawezi, na wenye pepo.
Marko 1:32
Na mji wote ulikuwa umekusanyika mlangoni.
Marko 1:33
Akaponya wengi waliokuwa na maradhi mbalimbali, akatoa pepo wengi, wala hakuwaacha pepo kunena, kwa sababu walimjua.
Marko 1:34
Kuna watu ambao wanateseka dhidi ya Mwovu, lakini habari njema ni hii BWANA atakuponya uwe na moyo mkuu tu, usikate tamaa. Mungu hapendi watu wake wateseke kamwe.
Je, unazifahamu sababu zinazopelekea kifo? Maana utasikia watu wanasema mapenzi ya Mungu. Mtu anafia nyumba za wageni(guest) akifanya uzinzi hivi ni mapenzi ya Mungu kweli hayo? Hakuna mapenzi ya namna hiyo kwa Mungu.
Aina za kifo:
1. Kifo cha uzee.
Hizi ndizo siku za miaka ya maisha ya Ibrahimu alizoishi, miaka mia, na sabini na mitano.
Mwanzo 25:7
Ibrahimu akafariki, naye akafa katika uzee mwema, mzee sana, ameshiba siku, akakusanyika kwa watu wake.
Mwanzo 25:8
Hiki maana yake ni kwamba muda wako umeisha, hivyo unapaswa ulale tu kutokana na uzee wako mwema.
2. Kifo kinachosababishwa na watu wengine. Mfano ajari ya gari. Kutekwa na majambazi.
3. Kifo kinachotokana makosa ya mtu mwenyewe. Wizi, ubakaji, uzinzi.
Usiwe mwovu kupita kiasi; Wala usiwe mpumbavu; Kwani ufe kabla ya wakati wako?
Mhubiri 7:17
4. Kifo kisichojulikana. Yaani Mungu huamua tu mtu alale.
Siyo kila kifo ni mapenzi ya Mungu.
Tunawezaje kuishi maisha marefu yenye tija?
1. Ishi kwa kumwamini na kumtumaini Mungu na kutembea katika njia zake kwa kufuata maagizo yake yote. Na kumpenda Mungu kikamilifu maisha yako yote.
Mwanangu, usiisahau sheria yangu, Bali moyo wako uzishike amri zangu.
Mithali 3:1
Maana zitakuongezea wingi wa siku. Na miaka ya uzima, na amani.
Mithali 3:2
2. Heshimu wazazi.(Watu wazima wote wenye hadhi sawa na wazazi wako, wazee, viongozi)
Waheshimu baba yako na mama yako; kama Bwana, Mungu wako, alivyokuamuru, siku zako zipate kuzidi, nawe upate kufanikiwa katika nchi upewayo na Bwana, Mungu wako.
Kumbukumbu la Torati 5:16
3. Kula vizuri.
Mungu akasema, Tazama, nimewapa kila mche utoao mbegu, ulio juu ya uso wa nchi yote pia, na kila mti, ambao matunda yake yana mbegu; vitakuwa ndivyo chakula chenu;
Mwanzo 1:29
Mpango wa Mungu ulikuwa mwanadamu ale matunda na mbegu.
Baada ya dhambi kuingia,
michongoma na miiba itakuzalia, nawe utakula mboga za kondeni;
Mwanzo 3:18
Baada ya gharika.
Bwana akamwambia Nuhu, Ingia wewe na jamaa yako yote katika safina; kwa maana nimekuona wewe u mwenye haki mbele zangu katika kizazi hiki.
Mwanzo 7:1
Katika wanyama wote walio safi ujitwalie saba saba, mume na mke; na katika wanyama wasio safi wawili wawili, mume na mke.
Mwanzo 7:2
Tena katika ndege wa angani saba saba, mume na mke; ili kuhifadhi hai mbegu juu ya uso wa nchi yote.
Mwanzo 7:3
Kwa uasili chakula halisi kilikuwa ni mbegu na matunda.
4. Usitumie kabisa vitu vyenye madhara. Mfano Tumbaku, pombe, dawa za kulevya.
asiwe mtu katikati yenu, mume wala mke, wala jamaa, wala kabila, ageukaye moyo wake leo amwache Bwana, Mungu wetu, kwenda kuitumikia miungu ya mataifa hayo; lisiwe katikati yenu shina lizaalo uchungu na pakanga;
Kumbukumbu la Torati 29:18
Pombe,
Ni nani apigaye, Yowe? Ni nani aliaye, Ole? Ni nani mwenye ugomvi? Ni nani mwenye mguno? Ni nani aliye na jeraha zisizo na sababu? Ni nani aliye na macho mekundu?
Mithali 23:29
Mvinyo hudhihaki, kileo huleta ugomvi; Na akosaye kwa vitu hivyo hana hekima.
Mithali 20:1
*MUNGU ATUBARIKI SOTE.*
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment