NYAMONGO NET-EVENT 2021-AMANI ITOKAYO JUU.
Jumanne, 21/09/2021.
MCH. BEATUS MLOZI.
SOMO: MIGOGORO KATIKA NDOA/FAMILIA.
Migogoro huja baada ya watu kutofautiana kimawazo yaani mpishano wa hoja baina ya mtu na mtu au watu na watu.
Mwanzo 24-27 utakuta mgogoro kati ya Isaka na Rebeka, na Raheli na Lea juu ya watoto.
Lakini Sulemani yeye je anasemaje?
Afadhali mego kavu pamoja na utulivu, Kuliko nyumba yenye karamu nyingi pamoja na magomvi.
Mithali 17:1
Ni afadhali kukaa katika pembe ya darini, Kuliko katika nyumba pana pamoja na mwanamke mgomvi.
Mithali 25:24
Migogoro haiepukiki katika maisha hata hivyo ni Mungu ndiye anayetuwezesha kuishinda. Kwamwe usikimbie ndoa yako kwa sababu ya migogoro.
Hata hivyo migogo ina faida na inaleta changamoto chanya maishani.
Aina za migogoto katika familia.
1. Migogoro inayosababishwa na sababu za ndani yaani wanandoa wenyewe.
2. Migogoro ya wapambe(watu wa nje) kutoka nje.
Migogoro kutoka nje husababishwa na watu wafuatao:
1. Mama mkwe, mama wa Bwana arusi. Anaweza kumwambia kijana amwache binti wa kijana wake lakini hawezi kumwambia binti yake kuachika kwa kijana fulani. Hivyo akina amama acheni kuwadanganya watoto wenu mke wa kijana wako ni ni binti yako pia.
2. Mawifi pia ni vyanzo vya migogoro katika ndoa za kaka zao. Ni wasumbufu sana katika ndoa na chanzo cha migogoro.
3. Mama wa bibi arusi naye ana shida. Unasikia akimwambia binti huyo mume akikusumbua rudi nyumbani hujaua. Umeharibu wewe mama mzazi.
4. Mashemeji pia ni shida.
5. Mdogo wa bibi arusi wa kike. Hawa nao ni chanzo cha migogoro.
6. Baba mkwe. Huyu pia ni chanzo cha mgogoro nyumbani.
MUNGU ATUSAIDIE SOTE.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment