Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ya Jiji la Mwanza akiwa ameambatana na Afisa Elimu Msingi, Wajumbe Kamati ya Siasa Wilaya ya Nyamagana na viongozi wa CCM Kata, ujumbe wa ofisi yake ukiongozwa na Bi. Florah Magabe, Madiwani wa eneo husika na Madiwani Viti Maalum pamoja na watendaji wa serikali Kata kukagua ujenzi wa Shule za Msingi nne Mpya kati ya Shule Mpya sita zilizojengwa katika mwaka wa fedha 2022/2023 na kugharimu Tsh. 1,174,000,000.
Akiwa Kata ya Igoma amepongeza Kamati ya ujenzi Shule ya Msingi Samia kutumia maelekezo ya mchoro uliotolewa na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, na serikali za Mitaa TAMISEMI ambao unatumia tofali Nchi 6 kwa mtindo wa kuzisimamisha ambazo zinapelekea katika kila mradi wa ujenzi wa shule moja kupata madarasa matatu ya ziada.
Kadharika Mhe Mabula ameoneshwa kutoridhishwa na kasi ndogo za ujenzi wa Shule ya Msingi Bugayamba iliyopaswa kukamilika tarehe 25.11.2023 huku ujenzi wake ukifikia 50% huku fedha zote Tsh 259,375,000 zimekwisha tolewa na serikali na ikionesha viashiria vya uzembe wa kamati ya manunuzi pamoja na Afisa ugavi, hivyo ameshauri Mkurugenzi wa jiji la Mwanza kukaa na kamati hizi pamoja kutatua tatizo hilo ndani ya siku mbili na kuongeza wiki mbili wazabuni wakamilishe mradi huo ili itumike Januari 2024.
Shule zingine ambazo Mhe. Mabula amezitembelea ni pamoka na Majengo iliyopo Kata ya Mkolani inayogharimu Tsh 259,375,000, Shule ya Msingi Swilla inayogharimu Tsh 221,875,000, Shule ya Msingi Bugayamba iliyopo Kata ya Lwanimah inayogharimu Tsh 259,375,000, Shule ya Msingi Samia Suluhu Hassan iliyoasisiwa kwa maono ya Mbunge na Mkuu wa Wilaya Mhe Amina Makilagi ipo Kata ya Igoma inagharimu takribani Tsh 259,375,000.
Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo La Nyamaga.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment