» » Muulize Yesu kuhusu Sabato

Haya ni mazungumzo kati ya mtu anayetunza kitakatifu jumapili na Yesu, Hili ni jibu tosha kwa maswali mengi yanayoulizwa kuhusu Sabato, Na ni hitimisho la aidha kuchagua kutunza au kutotunza “Sabato Takatifu” ya BWANA MUNGU wako.
Swali: Niambie BWANA, eti una siku maalumu ya pumziko kwa ajili ya wafuasi wako?
_Jibu: “Nalikuwa katika roho siku ya BWANA…” Ufu 1:10_
Swali: Lakini siku ya BWANA ni siku gani? Au Wewe ni Bwana wa siku gani?
_Jibu: “…Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa Sabato” Mt 12:8_
Swali: Kuna siku saba katika wiki, Je siku gani ni Sabato?
_Jibu: “Siku ya saba ni sabato ya BWANA, Mungu wako…” [amri ya nne] Kut 20:10_
Swali: Kwani siku ya saba ni siku gani? Je ni Jumamosi au Jumapili?
_Jibu: “Hata Sabato ilipokwisha kupita, Mariamu Magdalene na Mariamu mamaye Yakobo…alfajiri mapema, siku ya kwanza ya juma, wakaenda kaburini jua lilipoanza kuchomoza…Wakaingia kaburini wakaona kijana…akawaambia msisistaajabu; Mnamtafuta Yesu Mnazareti, aliyesulubiwa; amefufuka.” Mk 16:1-6 (N.B: Kila mtu anajua kuwa jumapili ni siku ya ufufuo, na jana yake ilikuwa Sabato, Hivyo tuna uhakika kuwa Jumamosi ndiyo siku ya Sabato)_
Swali: Lakini Bwana, kwani hukuitangua sheria yenye amri ya Sabato?
_Jibu: “Msidhani ya kuwa nalikuja kulitangua torati au manabii; la, sikuja kulitangua bali kulitimiliza.” Mt 5:17_
Swali: Vizuri, Je hukubadilisha walau amri moja, na hivyo wafuasi wako watunze siku nyingine tofauti na siku ya saba?
_Jibu: “Kwa maana amini nawaambia, mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta moja ya torati haitaondoka, hata yote yatimie.” Mt 5:18_
Swali: Lakini Bwana, Jumamosi siyo siku ya Wayahudi? Siku ya saba si ni siku ya Wayahudi?
_Jibu: “…Sabato ilifanyika kwa ajili ya mwanadamu…” Mk 2:27 (N.B: Sabato ilifanyika na akapewa mwanadamu miaka 1500 kabra ya kuwepo Myahudi hata mmoja; angalia Mwa 2:1-3)_
Swali: Bwana, kuna mtu aliniambia eti baada ya kusulubiwa kwako, wafuasi wako hawakutunza Sabato kama ilivyo amri, Je hii ni kweli?
_Jibu: “Na siku ile ilikuwa siku ya maandalio, na sabato ikaanza kuingia. Na wale wanawake waliokuja naye toka Galilaya walifuata, wakaliona kaburi, na jinsi mwili wake ulivyowekwa. Wakarudi, wakafanya tayari manukato na marhamu. Na siku ya sabato walistalehe kama ilivyoamuriwa.” Lk 23:54-56_
Swali: Je Mtume Paulo hakukutana na Wakristo jumapili ili kuheshimu ufufuo? Kwani desturi yake ilikuwa vipi, kuhusu siku ya kuabudu?
_Jibu: “Na Paulo, kama ilivyokuwa desturi yake, akaingia mle walimo, akahojiana nao kwa maneno ya Maandiko Sabato tatu.” Mdo 17:2_
Swali: Je alikutana pia na watu wa mataifa siku ya Sabato? Labda alikutana na Wayahudi siku ya Sabato na wamataifa siku ya jumapili?
_Jibu: “Akatoa hoja zake katika sinagogi kila Sabato, akajaribu kuwavuta Wayahudi na Wayunani.” Mdo 18:4_
Swali: Kwani Paulo alifundisha nini kuhusu kutunza Sabato?
_Jibu: “Basi imesalia raha ya sabato kwa watu wa Mungu. Kwa maana yeye aliyeingia katika raha yake amestarehe mwenyewe katika kazi yake, kama vile Mungu alivyostarehe katika kazi zake.” Ebr 4:9, 10_
Swali: Lakini Paulo alimaanisha siku gani aliposema kustarehe kama Mungu alivyostarehe?
_Jibu: “Kwa maana ameinena siku ya saba mahali furani hivi, Mungu alistarehe siku ya saba akaziacha kazi zake zote.” Ebr 4:4_
Swali: Bwana, Je wewe pia unafundisha tutunze Sabato?
_Jibu: “Kwa maana sikujiepusha na kuwahubiria habari ya kusudi lote la Mungu.” Mdo 20:27 (N.B: Katika Agano Jipya kuna marejeo 59 ya Sabato. Na kitabu cha matendo kina Sabato 84, ambazo Paulo na wengine walifanya huduma za ibaada. Hata hivyo hakuna hata neno moja katika Biblia linaloamuru kutunza jumapili)_
Swali: Sasa kwanini wengi hutunza jumapili badala ya Jumamosi? Kama Biblia hufundisha kutunza Sabato, Je nani aliingiza utunzaji wa jumapili kwa Wakristo?
_Jibu: “Naye (pembe ndogo) atanena maneno kinyume chake aliye juu…Naye ataadhimu kubadili majira na sheria…” Dan 7:25_
Swali: Kanisa la Romani Katoliki ndiyo pembe ndogo ya Danieli 7; Je unamaanisha kwamba litaadhimu kubadili sheria ya Mungu?
_Jibu: “…Waulize Makuhani katika habari ya sheria.” Hagai 2:11_
Swali: Vizuri sana, Nitamuuliza Stephen Keenan, kuhani wa Katoliki, Stephen, Je kanisa lako hudhani lina nguvu ya kubadili sheria ya Mungu?
_Jibu: “Lingekuwa halina uwezo kama huo, lisingefanya kile ambacho dini zote za leo zinakubaliana nalo; lisingeweka utunzaji wa jumapili, siku ya kwanza ya juma, badala ya jumamosi siku ya saba ya juma. Badiliko ambalo halina mamlaka ya Maandiko.” –Doctrinal Catechism, page 174_
Swali: Je badiliko hili lilifanyika lini?
_Jibu: “Tunatunza Jumapili badala ya Jumamosi kwa sababu kanisa la katoliki katika balaza la Laodikia (364 B.K) lilibadilisha Sabato kutoka Jumamosi hadi jumapili.” –The Converts’ Catechism, Peter Geirmann, page 50. (Katekism hii ilipokea baraka za papa Januari 25, 1910.)_
Swali: Je unahisi hii ni alama ya mamlaka yako?
_Jibu: “Bila shaka kanisa la katoliki hudai kuwa badiliko, (la Sabato Jumamosi kuwa Jumapili) ilikuwa ni kitendo chake…na kitendo hicho ni ALAMA ya mamlaka yake katika mambo ya kidini.” –H.F. Thomas, Chancellor of Cardinal Gibbons_
Swali: Bwana ALAMA hii ya Roma ni kinyume na ALAMA yako? Je wewe nawe una ALAMA?
_Jibu: “Tena naliwapa sabato zangu, ziwe ishara kati ya mimi na wao, wapate kujua yakuwa mimi, BWANA, ndimi niwatakasaye…zitakaseni sabato zangu; zitakuwa ishara kati ya mimi na ninyi, mpate kujua yakuwa mimi ndimi BWANA, Mungu wenu.” Ezekieli 20:12, 20 (N.B: Maneno, “ishara/dalili,” “muhuri,” na “alama” ni visawe, na unaweza kuyatumia kwa kubadilishabadilisha. Kwa hakika imethibitishwa katika Rum 4:11 ambapo inasema, “…alipokea DALILI hii ya kutahiliwa, MUHURI ya ile haki ya imani…”)_
Swali: Je Wachugaji wa kiprotestanti hukubaliana na hili?
_Jibu: Congregationalist: “Ni wazi kabisa kwamba kwa uimara wowote au kwa uaminifu kiasi gani tunaweza kuitumia jumapili, hatutunzi sabato.” –Dr. R.W. Dale, The Ten Commandments, page 106._
_Methodist: “Sabato kwa kiebrania huwakilisha pumziko na iko katika siku ya saba ya wiki…na ni lazima kukiri kwamba hakuna sheria katika Agano Jipya inayohusu siku ya kwanza.” –Buck’s Theological Dictionary._
_Baptist: “Kulikuwa na sasa kuna amri ya kutunza kitakatifu siku ya sabato, lakini siku hiyo ya sabato haikuwa jumapili. Ilishasemwa…kwamba sabato ilihamishwa kutoka siku ya saba hadi siku ya kwanza ya wiki…Ni wapi inaweza kuonekana kumbukumbu ya badiliko hilo? Hakuna katika Agano Jipya kwa hakika hakuna…Bila shaka, Najua vizuri kabisa kwamba Jumapili haikutumiwa katika historia ya Wakristo wa mwanzo…Lakini inanisikitisha kwamba ilikuja imetiwa muhuri na alama ya upagani, na ikafanywa ya Kikristo kwa jina la mungu jua, ilipoingizwa na kutakaswa na uasi wa papa, na ikachukuliwa kama kitu kitakatifu kwa Waprotestanti.” –Dr. E.T Hiscox, author of the Baptist Manual._
_Kwa maoni zaidi ya madhehebu mengine kuhusu utunzaji wa sabato, Tafadhari bofya hapa._
Swali: Kama dini zote za kiprotestanti hukubali kwamba sabato haikutakiwa kubadilishwa! Kwanini wanafanya kama Roma?
_Jibu: “Dunia yote ikamsitaajabia mnyama…Na watu wote wakaao juu ya nchi wtamsujudu, kila ambaye jina lake halikuandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwanakondoo, aliyechinjwa tangu kuwekwa misingi ya dunia.” Ufu 13:3, 8_
Swali: Kwani kuna utofauti gani na siku nayotunza? siku ni siku siyo hivyo?
_Jibu: “Hamjui ya kuwa kwake yeye ambaye mnajitoa nafisi zenu kuwa watumwa wake katika kumtii, mmekuwa watumwa wake yule mnayemtii, kwamba ni utumishi wa dhambi uletao mauti au kwamba ni utumishi wa utii uletao haki.” Rum 6:16_
Swali: Sasa nifanye nini nitii sabato amri ya Mungu au nitii jumapili amri ya mwanadamu?
_Jibu: “…Imetupasa kumtii Mungu kuliko wanadamu.” Mdo 5:29_
Swali: Vizuri Bwana, Je unawafikiriaje wanaotunza jumapili?
_Jibu: “Mkalitangua neno la Mungu kwa ajili ya mapokeo yenu…Nao waniabudu bure wakifundisha mafundisho yaliyo maagizo ya wanadamu.” Mt 15:6, 9_
Swali: Lakini kwa hakika, ni mamilioni ya watu wanaotunza jumapili hawawezi kukosea, Kwani wanakosea?
_Jibu: “Ingieni kupitia mlango mwembamba; maana mlango ni mpana, na njia ni pana iendayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa mlango huo. Bali mlango ni mwembamba, na njia ni imesonga iendayo uzimani, nao waionao ni wachache.” Mt 7:13, 14. (Wachache tu walimtii Mungu katika siku za nuhu, na katika siku za lutu, na katika siku za Kristo wengi watapoteza.)_
Swali: Lakini flani ana hekima nyingi; kwanini yeye na wahubiri wakubwa wengine hawatunzi sabato?
_Jibu: “Maana, ndugu zangu, angalieni mwito wenu, ya kwamba si wengi wenye hekima ya mwilini, si wengi wenye nguvu, si wengi wenye cheo walioitwa; bali Mungu aliyachagua mambo mapumbavu ya dunia awaaibishe wenye hekima.” 1Kor. 1:26, 27 (N.B: Pia katika siku za Kristo waalimu wa dini waliukataa ukweli, wafuasi wake walikuwa watu wa kawaida)_
Swali: Lakini nimemkubali YESU; najua yeye ni mwokozi wangu; najua amenikubali pia, na ninatunza jumapili, kwa hakika sitapoteza kama nisipotunza sabato. Kwani nitapoteza?
_Jibu: “Basi, zamani zile za ujinga Mungu alijifanya kama hazioni; bali sasa anawaagiza watu wa kila mahali watubu.” Mdo 17:30_
Swali: Nakujua we, Bwana, huwezi kunihukumu kwa kuvunja sabato! Unaweza?
_Jibu: “Yeye asemaye, nimemjua, wala hazishiki amri zake, ni mwongo, wala kweli haimo ndani yake.” 1Yoh. 2:4_
Swali: Lakini haitoshi kwamba nakupenda BWANA na ninaishi kwa sheria ya upendo?
_Jibu: “Mkinipenda, mtazishika amri zangu.” Yn. 14:15_
Swali: Bwana, Unamaanisha amri zote kumi?
_Jibu: “Maana mtu awaye yote atakayeshika sheria yote, ila akajikwaa katika neno moja, amekosa juu ya yote.” Yak 2:10_
Swali: Vizuri, nadhani kama tukikaa ndani ya Yesu, hiyo inatosha na hiyo ndiyo lazima. Kwani sio hivyo?
_Jibu: “Yeye asemaye ya kuwa anakaa ndani yake, imempasa kuenenda mwenyewe vile vile kama yeye alivyoenenda.” 1 Yoh. 2:6_
Swali: Je ulienendaje Yesu, desturi yako ilikuwaje?
_Jibu: “Akaenda nazareti, hapo alipolelewa; na siku ya sabato akaingia katika sinagogi kama ilivyokuwa desturi yake, akasimama ili asome.” Lk. 4:16_
Swali: Lakini, hapo ilikuwa zamani miaka 1900, iliyopita. Je hautatunza siku nyingine tofauti na jumamosi kama ukija duniani leo?
_Jibu: “Mimi, BWANA, sina kigeugeu…” Mal. 3:6. “Yesu Kristo ni yeye yule, jana na leo na hata milele.” Ebr 13:8_
Swali: Kwani wokovu wangu unahusiana nini na kutii sabato?
_Jibu: “Naye alipokwisha kukamilishwa, akawa sababu ya wokovu wa milele kwa watu wote wanaomtii.” Ebr 5:9_
Swali: Je unadhani ni lazima sana kutunza amri ili kupata uzima?
_Jibu: “…Ukitaka kuingia katika uzima zishike amri Mt 19:17_
Swali: Lakini Bwana, siwezi kukubali kwanini umeng’ang’ania siku ya saba, si jumapili nayo ni nzuri tu kama jumamosi?
_Jibu: “Mungu akaibariki siku ya saba, akaitakasa.” Mwa 2:3 “…Yeye ameibariki, nami siwezi kulitangua.” Hes 23:20 “…Wewe Bwana, umebariki nayo imebarikiwa milele.” 1Nya 17:27_
Swali: Vizuri, mimi naona kama nikitunza siku moja yoyote katika siku saba, itakuwa vizuri tu pia!
_Jibu: “Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu; lakini mwisho wake ni njia za mauti Mit. 16:25 “…Mambo ya kiroho…yanatamblikana kwa jinsi ya Rohoni.” 1Kor 2:13, 14_
Swali: Lakini, Bwana, Bwana, siwezi kufanya vinginevyo, kwani imani yangu haitanifikisha mbinguni?
_Jibu: “Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.” Mt 7:21_
Swali: Bwana, Lakini si ninasali?
_Jibu: “Yeye aligeuzaye sikio lake asiisikie sheria hata sara yake ni chukizo.” Mit. 28:9_
Swali: Lakini, Bwana, angalia watu wanafanya miujiza kwa jina lako. wengine wanaponya wagonjwa, wengine wanaongea kwa rugha, na kufanya mambo mengi ya ajabu; lakini hawatunzi sabato vipi kuhusu hao?
_Jibu: “Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? Ndipo nitawaambia dhahiri, sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu enyi mtendao maovu.” Mt 7:22, 23_
Swali: Najua sabato ni nzuri, lakini biashara yangu itarudi nyuma kama nikifunga siku ya sabato. Nitapoteza kazi yangu sitaenda na wakati!
_Jibu: “…Itamfaidia mtu nini kuupata ulimwengu wote, akipata hasara ya nafisi yake?” Mk. 8:36_
Swali: Vizuri, kwangu mimi stajari, lakini vipi kuhusu familia yangu? haingekuwa vizuri nifanye kazi siku ya sabato, kuliko familia yangu ife njaa?
_Jibu: “Baba yenu wa mbinguni anajua mnahitaji hayo yote. Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake, na hayo yote mtazidishiwa.” Mt 6:32, 33. “…Sijamwona mwenye haki ameachwa wala mzao wake akiomba chakula.” Zab 37:25_
Swali: Marafiki zangu watanidharau na kunicheka!
_Jibu: “Heri ninyi watakapowashutumu…na kuwanenea kila neno baya kwa uongo, kwa ajili yangu. Furahini, na kushangilia kwa kuwa thawabu yenu ni kubwa mbinguni.” Mt 5:11, 12. “Iwapo ulimwengu ukiwachukia, mwajua ya kuwa umenichukia mimi kabla ya kuwachukia ninyi.” Yn 15:18_
Swali: Lakini, kama familia yangu haikubaliani nami, Je niende kinyume cha matakwa yao, kitu ambacho kinaweza kusababisha mafarakano nyumbani?
_Jibu: “Apendaye baba au mama kuliko mimi, hanistahili. Wala mtu asiyechukua msalaba wake na kunifuata hanistahili.” Mt 10:37, 38 “Basi, kadhalika kila mmoja wenu asiyeacha vyote alivyonavyo, hawezi kuwa mwanafunzi wangu. Lk 14:33_
Swali: Naogopa siwezi kustahimili majaribu yote hayo. mimi ni dhaifu sana!
_Jibu: “Neema yangu yakutosha; maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu…maana niwapo dhaifu ndipo nilipo na nguvu.” 2Kor 12:9, 10 “Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu.” Fil 4:13_
Swali: Sasa Bwana, zawadi yangu nini kama nikiwa mwaminifu kwako na kutii amri?
_Jibu: “Hakuna mtu ambaye ameacha nyumba, au mke, au ndugu, asiyepokea mara nyingi katika zama hizi na katika ulimwengu ujao uzima wa milele.” Lk 18:29, 30 “Heri wazifuao nguo zao, wawe na amri kuuendea huo mti wa uzima, na kuingia mjini kwa milango yake.” Ufu. 22:14_
Swali: Bwana, napasubiria nyumbani katika nchi mpya, Je huko nako tutatunza sabato?
_Jibu: “Kama vile mbingu mpya na nchi mpya, nitakazofanya, zitakavyokaa mbele zangu, asema BWANA, ndivyo uzao wenu na jina lenu litakavyokaa. Na itakuwa, mwezi mpya hata mwezi mpya, na sabato hata sabato, wanadamu wote watakuja kuabudu mbele zangu, asema BWANA.” Isa 66:22, 23._
Swali: Haya, Bwana, Mapenzi yako yatimizwe hapa duniani kama vile huko mbinguni. Kwa msaada wako nitaitunza sabato.
_Jibu: “…Vema mtumwa mwema na mwaminifu…”_

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...