» » UJENZI WA MRADI WA MAJI MAGU WAFIKIA ASILIMIA 85  

   Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira (MWAUWASA), Mhandisi Anthony Sanga amesema ujenzi wa mradi wa maji katika Mji wa Magu, Mkoani Mwanza umefikia asilimia 85 za ujenzi wake.   Mhandisi Sanga alisema hayo alipofanya ziara kwenye mradi huo Aprili 24 kwa lengo la kujionea na kujiridhisha hatua iliyofikiwa ya ujenzi wake ambao unasimamiwa na MWAUWASA kwa niaba ya Wizara ya Maji.   Mhandisi Sanga alisema utekelezaji wa jumla wa mradi umefikia asilimia 85 na ulazaji wa bomba kwa ajili ya kuunganisha wananchi imefikia asilimia 95.   Alibainisha kwamba mradi una uwezo wa kuzalisha lita 7,250,000 ambayo ni mahitaji ya Mji wa Magu kwa miaka 20 ijayo. “Mradi huu ni mkubwa sana hata kama wananchi wa Magu wataongezeka mara mbili zaidi bado utaweza kuwahudumia,” alisema Mhandisi Sanga.   Mhandisi Sanga alisema kukamilika kwa miradi inayotekelezwa chini ya ufadhili wa Serikali kupitia mpango wa Uboreshaji wa Huduma ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Ziwa Victoria, miji yote mikuu ya Mkoa wa Mwanza itakua imepata huduma ya majisafi na salama kutoka Ziwa Victoria.   “Mradi ukikamilika miji yote mikuu ya Mkoa wa Mwanza itakua imepata huduma ya maji safi na salama kutoka Ziwa Victoria kwani tumepeleka Nansio, Sengerema, Ngudu, Magu na Misungwi,” alisema.   Mhandisi Sanga aliupongeza uongozi wa Mkoa wa Mwanza na wa Wilaya ya Magu kwa ushirikiano mkubwa wanaotoa kwenye shughuli mbalimbali za utekelezaji wa mradi.   Aidha, aliwapongeza wananchi kwa ushirikiano wanaoutoa hususan wa ulinzi wa miundombinu ya maji inayotumika kwenye ujenzi wa mradi huo.        CAPTIONS 1 Mkurugenzi Mtendaji wa MWAUWASA, Mhandisi Anthony Sanga (kulia) akielekeza jambo wakati wa ziara yake ya ukaguzi wa ujenzi wa mradi wa maji Mji wa Magu Katikati ni mwakilishi wa Mhandisi Mshauri, Mhandisi Adam Jabir.   2 Mkurugenzi Mtendaji wa MWAUWASA, Mhandisi Anthony Sanga akiwaongoza wataalam wakati wa ziara yake ya ukaguzi wa ujenzi wa mradi wa maji Magu. Anayemfuatia ni Meneja Mradi, Mhandisi James Kionaumela na wataalam wengine.   3 Mkurugenzi Mtendaji wa MWAUWASA, Mhandisi Anthony Sanga (kushoto) akimuelekeza jambo mwakilishi wa Mhandisi Mshauri, Mhandisi Adam Jabir alipotembelea Tenki la mradi lenye uwezo wa kuhifadhi lita milioni 2 za maji.   4 Mkurugenzi Mtendaji wa MWAUWASA, Mhandisi Anthony Sanga akikagua ujenzi wa tenki la mradi ambalo lina uwezo wa kuhifadhi lita milioni 2 za maji.   5 Muonekano wa Mji wa Magu kutoka kwenye usawa lilipo tenki la kuhifadhia maji la mradi.    

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...