» » KESHA LA ASUBUHIJumapili 21/02/2021

IMARA KWA UWEZO WAKE*

*Basi, dhambi isitawale ndani ya miili yenu ipatikanayo na mauti, hata mkazitii tamaa zake.* Warumi 6:12

🔰 Dumuni kujifunza kwa Yesu, dumuni kuongezeka katika imani na kukua katika neema na ujuzi wa kweli. Tunafanya kazi kubwa, na Mungu ni msaada wetu, Bwana ni ngao yetu. Hatatuacha wala kututupa. Malaika wa Mungu wanashughulika katika kazi hii ya kutangaza ujumbe wa onyo kwa ulimwengu. Peke yetu hatuwezi kufanya lolote. Tu wadhaifu kama maji pasipokuwa na Roho wa Bwana. Nguvu yetu ipo katika kujificha ndani ya Yesu. Hebu Kristo aonekane mzuri sana, na mkuu miongoni mwa kumi elfu. 

🔰 Tena, nawasihi kutunza vyema makazi ambayo Mungu amewapatia. Hebu dhambi isitawale katika mwili wako ufao, na usitumie vibaya nguvu za kimwili ambazo Mungu amekupatia, bali tunza kwa upendo sana nguvu zako, ukiweka tumaini lako lote kwa Mwokozi mkamilifu. Anahitaji uwe mshindi na kuvaa taji ya kito cha thamani hatimaye. 

🔰 Mbingu, mbingu nzuri, ni makao ya milele ya watakatifu.Tutapumzika kitambo kidogo tu. Hebu basi tusitumie nguvu zetu isivyofaa, ili kwamba Mungu azizidishe na kuzitakasa na kuzifanya ziwe kwa utumishi wa juu sana. Hebu Bwana na aje karibu sana nawe, na kukupatia mvuto wenye nguvu kuangusha chini makosa na ushirikina na kazi za Shetani. 

🔰 Tunaweza kumwomba Mungu mambo makubwa naye atatupatia. Tutakuwa na nguvu katika nguvu zake. Utapata upinzani toka kwa wahudumu wa kanisa kadri unavyoishi kuifikilia na kuwasilisha kwa wengine, kiwango cha juu cha dini ya Biblia; dharau na kuzomewa, kashfa na uongo vitakufuata. Nia, na maneno yako, matendo yako vitaeleweka vibaya na kutafsiriwa vibaya na kushutumiwa. Lakini, ukiendelea na kazi licha ya manyanyaso unayopata, ukifanya vyema, ukiwa mwema na mvumilivu, mnyenyekevu katika roho, mwenye furaha katika Mungu, utakuwa na mvuto. Utapata huruma ya wale wote walio wanyofu na wenye akili.

🔘 *Shikilia Neno la uzima, dhoruba ya upinzani itajisambaza kwa ghadhabu yake yenyewe na kutulia. Ghasia zitafilia mbali... Upatanifu wa kweli utaonekana na utahisiwa na kutiiwa na wanyofu na wamchao Mungu.*

*MUNGU AKUBARIKI SANA*👮‍♂️

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...