» » KESHA LA ASUBUHIJumapili 07/02/2021


KIOO CHA KIMBINGU

*Lakini sisi sote, kwa uso usiotiwa utaji, tukiurudisha utukufu wa Bwana, kama vile katika kioo, tunabadilishwa tufanane na mfano uo huo, toka utukufu hata utukufu, kama vile utukufu utokao kwa Bwana, aliye Roho.* 2Wakorintho 3:18

🔰 Ndugu yangu mpendwa, umekuwa ukitazama nini? Kwa kutazama mapungufu ya wanaume na wanawake, unabadilishwa hatua kwa hatua na kufanana nao. Fanya badiliko la dhati, na mtazame Yesu, ili kwa kutazama ukamilifu wake, uweze kubadilishwa kuwa katika sura yake. Kisha Roho wake atatawala akili na tabia yako. Kwa uchaji Mungu na utauwa wako, kwa maneno na matendo yako, kwa juhudi yako ya kiroho kwa ajili ya kweli na haki, utamwakilisha Kristo. 

🔰 Mwanadamu anapogeuka toka katika mapungufu ya kibinadamu, na kumtazama Yesu, mabadiliko ya kiungu hutokea katika tabia yake. Hukaza macho yake kwa Kristo kama kwa kioo ambacho huakisi utukufu wa Mungu, na kwa kutazama, “tunabadilishwa tufanane na mfano uo huo, toka utukufu hata utukufu, kama vile utukufu utokao kwa Bwana, aliye Roho” (2 Wakorintho 3:18). “Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake” (Warumi 8:9)

🔰 Geuza macho yako toka katika mapungufu ya wengine, na kuyaelekeza kwa uthabiti kwa Knsto. Kwa moyo wenye toba, jifunze maisha na tabia yake. Huhitaji tu kuelimishwa zaidi, bali kuhuishwa, ili uweze kuona karamu iliyo mbele yako, na kula na kunywa mwili na damu ya mwana wa Mungu, ambayo ni neno Lake. Kwa kuonja neno zuri la uzima, kwa kujilisha katika mkate wa uzima, unaweza kuona nguvu ya ulimwengu ujao, na kuumbwa upya katika Kristo Yesu. Ukipokea vipawa vyake, utafanywa upya kuufikia utakatifu, na neema itazaa ndani yako matunda kwa utukufu wa Mungu. 

🔰 Roho Mtakatifu humfunua Kristo katika moyo, na imani humshikilia yeye. Ukimpokea Yesu kama Mwokozi wako binafsi, utatambua kwa uzoefu thamani ya kafara kubwa iliyofanywa badala yako juu ya msalaba wa Kalwari. Roho wa Kristo, akifanya kazi katika moyo huufanya upatane na sura yake; kwa kuwa Kristo ndio mfano ambao Roho hutenda kazi. Kwa huduma ya Neno lake, kwa majaliwa yake, kwa utendaji wake wa ndani, Mungu hutia muhuri mfano wa Kristo katika moyo. 

🔘 *Kuwa na Kristo ndio kazi yako ya kwanza, na kumfunua kama yeye awezaye kuokoa kwa kiwango cha juu wote wajao kwake, ni kazi yako inayofuata.*

*MUNGU AKUBARIKI SANA*👮‍♂️

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...