IJUE BIBLIA
Historia ya vitabu vya Biblia nawaandishi wake..
Biblia ninini? Biblia si neno la Kiswahili, bali nineno la kiyunani ambalo waliita
kwa lugha yao Biblos’ na waingereza nao wakakosa tafsiri halisi ya neno hilo
wakatohoa kwa kufananisha kidogo na Biblos’ wao wakaiita Bible hatasisi kwa
rugha ya Kiswahili tuli kosa neno kamili tuka tumia rugha ya kutohoa kutoka
Bible, na kuitwa Biblia ikiwa inamaanisha mkusanyiko wa maandiko matakatifu.
Biblia kama tulivyoona maana ya neno hilo ni mkusanyiko wa maandiko
matakatifu, mkusanyiko huo wa maandiko matakatifu umekusanya maagano
mawili moja linaitwa agano la kale na lapili linaitwa agano jipya, maagano hayo
yana lengo moja la kumpatanisha mdhambi na Mungu wake lakini
yametofautiana katika utekelezaji
8i. Agano la kale, niagano ambalo Mungu aliagana nawatu walio ishi kabla
ya kuzaliwa kwa Yesu ambalo agano hilo lilikua ni agano la damu ya
wanyama ilikuwa mdhambi ili apate upatanisho alilazimika kuchukua
kondoo na kumpeleka kwa kuhani, na kondoo huyo anachinjwa na
damu yake humiminwa katika mabakuli, na kuhani ataiingiza katika
meza ya upatanisho na huyo mdhambi anapata msamaha wa dhambi
zake. Soma Lawi 5:5-7 ndiyo maana likaitwa agano la kale.
ii. Agano jipya hili Mungu anaagana nasi tunao ishi baada ya Yesu kristo
kwamba mtu akitenda dhambi, basi halazimiki kumchukua kondoo na
kumpeleka kwa mchungaji bali mdhambi anapaswa kuitazama damu
ya Yesu msalabani na Mdhambi anasamehewa dhambi zake kupitia
dam ya Yesu soma mathayo 26:26-28 kwa sababu hizo ndiyo maana
likaitwa agano jipya.
Agano la kale peke yake lina vitabu 39 na sura 921 na limegawanyika katika sehemu kuu
tano ama ifuatavyo;
1. Vitabu 5 Vya Sharia
Kama tulivyoona agano la kale limegawanyika sehemu kuu tano. Na seshemu ya
kwanza ni sheria, sheria ambayo waebrania waliita Torah na Wayunani waliita
Pentantuk, sehem ya kwanza hiyo ina kamilishwa na vitabu vitano navyo ni hivi; Mwanzo, Kutoka, Mambo ya walawi, Hesabu, Kumbukumbu la Torati. Itaendelea kesho.....
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment