MTUNZI NA MWANDISHI-MWL YUSUPH ABEL NG'AHALA.
Sim no,0755683295/Watsap,instagram@mwalim_yuu, Email@yusuphngahala@gmail.com, Fb.com/Mwalimu Yusuph Abel Ng'ahala.
SEHEMU YA 44.
Tulipoishia, Kizuri ni kwamba watu walikuwa wengi sana hivyo nisingeonekana. Nilipepesa macho na nisimwone Zabroni. Lakini nikajipa moyo kwani watu waliendelea kutoka Sikuamini macho pale nilipoona ________Songa nayo........ Abiria wameisha na hakuna Zabroni wala Peris wala nani. Nilingiwa na woga nikishangaa huyu Zabroni ni nani mbona kama jini hivi? Nikaamua kuweka silaha yangu na kujongea mpaka kwenye ile ndege na kuangalia mle ndani sikumwona Zabroni. Lakini kuna begi nililiona alikuwa kaingia nalo Zabroni kabla ndege haijaruka kutokea Tanzania. Kilikuwa kibegi kidogo tuu. Nilijaribu kuangalia kama naweza kukichukua lakini wahudumu wa ile ndege walikuwa makini sana.
Nikaamua kusema nakaa hapa mpaka nione nani anachukua kile kibegi. Nilikaa pale mda mrefu mara wahudumu wakaja na kuniuliza "Hey! What is wrong with you? What are you waiting for? This is Ethiopia Adis Ababa" Nikajibu Am sory am waiting for someone. Basi mmoja akajibu You are doing the right thing, in the right time, but unfortunately in a wrong place" This is not the place you can sit and tell us you are waiting for someone please leave"
Ilibidi niwe mpole na kuondoka zangu kwenda sehemu za kukaa kusubiri mtu. Lengo haikuwa kumsubiri mtu lakini ilikuwa kumtafuta Zabroni. Mara nikawaona wale wahudumu wanatoka na kile kibegi cha Zabroni. Walikuwa wanaenda kwenye vyumba vyao vya mapumziko. Niliinuka na kuwafuatilia kwa nyuma kwa kuibia ibia. Kisha nikawaona walipoingia na kile kibegi. Nikarudi kukaa pale baada ya mda nikaamua kwenda kule ili nikaangalie uwezekano wa kuoata begi.
Nikafika mpaka mlangoni kisha mlinzi akanifuata na kuniuliza "Where are you going" we dont allow stranger here? Nikamjibu am sory i just want to see pilot of that plane nikamwonyeshea kwa kidole. Kisha akaniuliza, Do you have an appointment? Nikamjibu No! not real but i have something very important to tell him! Akaniuliza passport nikampa baada ya kujiridhisha akaniruhusu. Nikaingia na kujongea. Kumbe kuna mageti mawili nikaliona la pili hili lilikuwa na ukaguzi mkali zaidi. Nikaamua mbinu moja hivi ambayo ni kupata vazi la wafanyakazi.
Hao niliona wanapita bila ukaguzi. Nikajibanza sehemu na kusubiri apite mmoja. Kwakuwa ilikuw ni eneo la wafanyakazi hivyo wengi walipita baada ya mda mfupi. Mara kuna jamaa nilimwona anakuja pekeake. Nilimwangaliaa kisha nikafichama mpaka alipofika. Nikamvuta chemba na kumtia ngumi ya akili akaanguka na kuzimia kwani nilimpiga sehemu mbaya.
Alipoanguka mi nikamvua ngo na kuvaa haraka kisha nikaana safari ya kuelekea ndanj. Nilifika getini na kupita bila shida yoyote ishu ngumu ikaja ndani. Mlikuwa na wahudumu wengi sana mpaka nikawa sijui nianzie wapi na nimalizie wapi. Mara nikaona mbeba mizigo mmoja ambaye ni mfanyakazi wa mle ndani anaingia na mabegi chumba fulani. Nikaamua kumfuata kwa nyuma ili nione kama pia kibegi cha Zabroni nitakipata. Baada ya kufika ndani nilipishana naye akitoka na kwenda zake. Huku nyuma mi.i nikaanza kupekenyua makablasha mengi mengi nione kama nitapata chochote.
Nilikata tamaa na kutaka kuondoka. Mara nikaona kuna mhudumu mmoja akiingia na kupepesa macho kisha kulikuwa na shelf ivi akachukua kitu. Haaa kumbe ni lile begi natafuta wakati nainuka ili nimvamie akawa kashafungua mlango na kutoka. Nikaona hapa haiwezekani namfuata. Basi nikaona anaingia chhmba fulani ambacho kiliandikwa store. Nadhani huko walikuwa wanatunza vitu. Nikaamua kurudi kule nikae kwa mda kisha niende chumba kile.
Baada ya mda nikaenda na kukuta mlango uko wazi. Niliingia ndani na kukikuta kile kibegi. Lakini wakati nakichukua nilimwona miongoni mwa wahudumu wa kle ndege nilobishana nao. Hivyo nikajua akiniona atanishtukia. Kulikuw a naadumu hivi pale chini mengi sana nikaamua kujificha kwenye yale madumu ya mafuta. Aliingia na kutoka bila kuniona mimi nikainuka hjku nanuka mafuta na mengine yamenimwagikia. Sikujali kwani nilikuwa naazimia kupata begi na nimelipata.
Basi nikatoka na kufika sehemu nikaivua ile nguo na kuanza safari ya kutoka. Nilitoka na kufika nje bila kushitukiwa japo mlinzi aliniangalia jicho la kunitilia mashaka. Lakini kwa kuwa nilijiamini hakuwa na ujanja aliishia kuniangalia tuu. Niliamua kutoka pale uwanjani na kutafuta hotel nilale. Nilipata hotel moja iko karibu na lale uwanjani nikaingia humo na kulipia kwa siku mbili mapumziko ya pale. Nilifunga mlango na lile begi nikaliweka juu ya meza kisha nikajisea moyoni ngoja nioge kwanza halafu nitalikagua. Ile ingenipa mwanga wa wapi nianzie upepelezi wangu kwani pale uwanjani sikumwona na hilo lilinitatiza sana.
Basi nikaingia bafuni kuoga na baada ya kumaliza nikatoka na kujifuta kisha nikaanza kuiangalia ile begi ya Zabroni. Niliichukua na kuiangalia kwa makini mana isije kuwa na mabomu hasa ukizingatia yule ni jambazi. Basi baada ya kujiridhisha nikaanza kuifungua. Ambapo chakwanza nilikutana na Chupi mbili za kiume, pia nikakutana na tisheti na baragaishia. Nikaanza kulegea nakuona kujiumiza kote nakutana na upuuzi tuu.
Nikaendelea mpaka namaliza sikuona cha maana. Nilikasirika sana na kuamua kulitupa lile begi chini. Maana nilipokumbuka purukushani za kwenye madumu kuhatarisha maisha ili nipate lile begi halafu ni utumbo tuu mle ndani nilichukia kwakweli. Nikalitupa chini. Lakini baada ya kutupa mfuko wa pembeni uliangusha kitu kama bahasha hivi. Wakati nainama kuichukua nisome mara mlango wa kile chumba ukagongwa, ngo! Ngo! Ngo!____________________________________________________________________________________
Tukutane sehemu ya 45 nikupe habari kamili hahahaha nimekatisha utamu. Nawapenda woteeeeee jamani chaooooooo
YUSUPHU SIMLIZI: SIMULIZI YA KUSISIMUA-NANI KACHUKUA SURA YANGU?
MTUNZI NA MWANDISHI-MWL YUSUPH ABEL NG'AHALA.
Sim no,0755683295/Watsap,instagram@mwalim_yuu, Email@yusuphngahala@gmail.com, Fb.com/Mwalimu Yusuph Abel Ng'ahala.
SEHEMU YA 45.
Tulipoishia, Lakini baada ya kutupa mfuko wa pembeni uliangusha kitu kama bahasha hivi. Wakati nainama kuichukua nisome mara mlango wa kile chumba ukagongwa, ngo! Ngo! Ngo!______Songa sasa........... Niliingiwa na woga na kuhisi huenda Zabroni kafika na hapo sasa ndo wahenga walisema iliungua shoka mpini ukabaki. Ikiwa ni zabron basi nitapigana kufa na kupona. Nikainuka na kuchukua lile begi kisha nikaliweka kwenye kabati na kuja mpaka mlangoni na kuuliza nani "Yes, who is this? Akajibu mrembo its me" Nikafungua mlango ndipo nikakutana na mrembo wa hatari amelendeza na ananukia marashi haswaa.
Unajua watu wa Ethiopia walivyo alikuwa mweupe na nywele ndefu. Alikuwa kaumbika bambataa mashaallah. Nikamwangakia nikamwona anajiumauma kidole mdomoni na kuniangalia kwa jicho la kurembua. Nilikaa kimya kwa mda nikihisi kama nimeona malaika hivi. Kisha nikameza mate ya tamaa na kisha nikamuuliza. Yes how can i help you? Akajibu Am the one who is goin to help ya! Alijibu akiongea kama vile mtu wa America.
Nikamwangalia kisha nikamwambia, can you make it clear please! Akajibu ooh Yea! its like.. Like..... I saw you ... I.... Saw ya.. Comin in dis room, then i though we can spend the night here together! In short i wanna be with ya for the whole night then you will gime bucks! Kisha akatulia. Mtumeeee Roho yangu kumbe anajiuza. Mdada mrembo kama yule kwanini asitulie akakaa na kupata mume badala ya kujiuza hotelini.? Hayo yalikuwa mawazo yangu baada ya kujua shida yake. Nikamwangalia juu mpaka chini. Kisha kuna sauti ya mke wangu aliyefariki ikasikika ikisema Yuu usijaribu mume wangu. Nilijishtukia na lisha nikaamua kumjibu kwa ustaraabu tuu.
Ok sorry just give me your phone number i will call right? I like you by the way! Akajibu thank you akanipa business card. Haaa yani muuza uchi mmalaya ana business card? Daah hii ilikuwa mpya kwangu. Kisha akaondoka. Alikuwa kajaaliwa haswaa niliona mirindimo ya sehemu ya mili wake hakika alikuwa ana kila sifa ya kumshawishi mwanaume. Nilikuwa nina hamu ya mapenzi ndio. Tena si kidogo ni sana tuu. Lakini nilikuwa sitaki kumwamini mtu yeyote kwani kila niliyekuwa nikimwamini niliishia kulia na kuumia. Hivyo nikasema wacha hili balaa linipitie mbali kabsa.
Nikafunga mlango kwa hasira kisha nikamua kama nitasikia tena unagongwa sifungui. Naana huyu malaya alikuwa kashaniharibia siku. Nikaamua nikae nitulize kichwa kwanza kabla ya kuendelea na shughuli zingine. Baada ya mda nikainuka na kuanza kuifungua ile bahasha niliyoikuta kwenye begi ka Zabroni. Nilifungua na kisha nikaisoma. Ilikuwa imeandikwa kwa Lugha ya kingereza. Lakini ujumbe wake kwa kifupi ulikuwa unamaanisha kuwa. Baada ya wao kutua kwa ghafla Uwanja wa Nairibi ndege ilipopata tatizo kuna abiria walishuka. Na mpaka wanaondoka kuna abiria wawili walikuwa bawajafika. Hivyo ile barua ilikuwa inawataka walinzi kutunza ile begi mpaka mwenye nayo atakapopatikana na kuichukua.
Kumbe ile barua waliandika wahudumu wa ile ndege. Nilishtuka sana pia niliumia pale nilipogundua kuwa ndege ilipata matatizo na hivyo kutua kwa ghafla jijini Nairobi. Hapo ndipo zabron atakuwa kashukia. Kwaninj Zabroni anajua kila ninanchotaka kumfanyia. Jee alishuka na kusahaulika na au alishuka kwa nia ya kunikomoa tuu.
Niliamua, kuendelea kukagua. Ule mfuko wa upande nmoja sikuona kingine zaidi. Nijahamia uoande wa pili huku ndio kulikiwa na majanga. Nilikutana na Diary. Nikaiweka pembeni. Kisha nikakutana na simu fulani aina ya Samsang. Nikazidi kupekua nikakutana pia na sura moja ya bandia. Lakini kulikuwa na bastola na pia kulikuwa na miswaki miwili. Zaidi nilikutana na pesa za kimarekani yaani dola. Nikazihesabu zilikuwa dola 1000.
Nilizidi kuangalia Kwa makini kila mfuko ulikuwa kwenye lile begi. Kuna mfuko mwingine nilikutana na shanga za kike. Baada ya kuziangalia vizuri zilikuwa ni mchanganyiko wa kamera za kurekodi matukio pamoja na vinasa sauti. Nilisgangaa sana nikajosemea kwa mwendo huu Zabroni ataisumbua sana serikali kwani anajitosheleza sana. Ikiwa mpaka shanga ni vifaa ndo maana kila linalofanywa halifanikiwi.
Kuna sehemu pia nikaona koti ambalo lilikuwa ni sare ya JWTZ nikalitoa na kuliangalia kisha kuna kitu nilihisi juu ya lile koti. Ilikuwa ni vile vifungo vya lile koti. Vilikuwa vikubwa sana. Nikaamua kuvitoa na kuviweka mahali. Kisha nikaanxa kama kuvikagua hivi ambapo kimoja nikagundua kina risasi nne, na kingne pia na hivyo kukamilisha jumla ya risasi nane.
Nilikuwa tayari nimeshtuka juu ya vile vifungo. Nikajua tuu ile ni silaha. Nikaanza kuiunda na kuibuni mara nilipomaliza kuunga nilijikuta nimezalisha silaha. Ilikuwa ni bastola yenye risasi nane. Nilipigwa na butwaa na kujisemea moyoni ama kweli Tembea uone hadi vifungo ni silaha.
Nikamaliza ukaguzi wangu na kuamua kutulia kidogo. Mda ukaenda siku ya kwanza ikapita nikaamua nianze kujipanga jinsi ya kurudi Tanzania ukizingatia nilishajua Zabroni alishukia Nairobi mara baada ya ndege kupata tatizo ghafla. Wakati napitiapitia baadhi ya website za nyumbani nilikutana na habari ya kutisha kidogo. Niliona kama mtu kauawa hivi na maandishi chini. Nikaamua kuifungua ndipo nikakuta mi kweli aliyeuawa ni_______________________________________________________________________________________________________________________________________________________Tukutane sehemu ya 46 nikupe majibu. Nawatakia siku njema wapendwa. Kwa lolote namba ziko juu hapo. Chaoooóoooo
No comments:
Post a Comment