» »Unlabelled » MICHEZO LEO: Usajili 2016/17: Mambo muhimu yaliyotokea sokoni Uingereza

Usajili 2016/17: Mambo muhimu yaliyotokea sokoni Uingereza


Mshirikishe mwenzako
Manchester UnitedImage copyrightGETTY IMAGES
Image captionManchester United waliwalipa Juventus £89m kumchukua Paul Pogba
Klabu za Ligi ya Premia zilitumia zaidi ya £155m siku ya mwisho ya kuhama kwa wachezaji kipindi cha majira ya joto na kufikisha jumla ya pesa zilizotumiwa hadi rekodi mpya ya £1.165bn.
Klabu zilikuwa tayari zimetumia jumla ya£1.005bn kufikia saa nne mchana Jumatano saa za Afrika Mashariki na kuvunja rekodi ya mwaka jana ya £870m.
Klabu 13 za ligi hiyo kuu ya England zilivunja rekodi zao sokoni.
Hapa chini ni mchoro unaoonesha matumzii ya fedha kwa klabu za Ligi ya Premia kwa miaka 10 iliyopita, Majira ya Joto.
Matumizi EPL

Mchezaji aliyenunuliwa pesa nyingi zaidi ni Paul Pogba

Paul Pogba

Amerejea Manchester United

£89m
Pesa ambazo Man Utd wamelipa kumnunua Pogba kutoka Juventus
  • £1.5m Pesa ambazo Man Utd walimuuza Pogba kwa Juventus 2012
  • £61.9m Faida ambayo Juventus wamepata
Hapa chini ni orodha ya wachezaji walionunuliwa ghali zaidi na kalbu za Ligi ya Premia msimu wa 2016-17:
The list of the biggest fees spent by Premier League clubs during the 2016-17 summer transfer windowImage copyrightGETTY IMAGES

Klabu zajitanua kutumia pesa

Klabu zilizovunja rekodi zao binafsi katika ununuzi
Manchester United: Paul Pogba (£89m)Bournemouth: Jordon Ibe (£15m)
Liverpool: Sadio Mane (£36m)Sunderland: Didier N'Dong (£13.6m)
Crystal Palace: Christian Benteke (£32m)Hull: Ryan Mason (£13m)
West Ham: Andre Ayew (£20.5m)West Brom: Nacer Chadli (£13m)
Leicester: Islam Slimani (£29m)Watford: Roberto Pereyra (£13m)
Southampton: Sofiane Boufal (£16m)Burnley: Jeff Hendrick (£10.5m)
Swansea: Borja Baston (£15.5m)
Klabu mbili za Manchester, City na United, zilitumia zaidi ya £150m.
Meneja mpya wa Manchester United, Jose Mourinho, alimnunua Paul Pogba kwa rekodi ya dunia £89m.
Pia walimnunua kiungo wa kati kutoka Armenia Henrikh Mkhitaryanna beki wa Ivory Coast Eric Bailly, wawili hao kwa £30m.
City, chini ya Pep Guardiola, walinunua kiungo wa kati Leroy Sane kutoka Schalke kwa £37m kisha wakalipa Everton £47.5m kumchukua beki John Stones.
Chelsea na mmiliki wao Roman Abramovich, walimpa meneja mpya Antonio Conte nguvu mpya za kutumia pesa.
Alitumia £120m, ikiwa ni pamoja na £34m kumrejesha beki Mbrazil David Luiz kutoka Paris St-Germain na £33m kumpata mshambuliaji Mbelgiji Michy Batshuayi kutoka Marseille.

Waliotawala mitandao ya kijamii

Ni mchezaji yupi aliyezungumziwa sana mitandao ya kijamii?
Ilikuwa ni difenda Mbrazil David Luiz aliyerejea Chelsea kutoka Paris St-Germain.
Kulikuwa na ujumbe 330,000 katika Twitter kumhusu, akifuatiwa na Jack Wilshere wa Arsenal, aliyetumwa kwa mkopo Bournemouth. Kulikuwa na ujumbe 108,000 kwenye Twitter kuhusu kiungo huyo wa kati.
Kipa wa Manchester City Joe Hart, aliyeenda Torino kwa mkopo, saini mpya wa Tottenham Moussa Sissoko na Samir Nasri wa Arsenal, aliyetumwa Sevilla, ndio wachezaji wengine waliozungumziwa sana.
A graphic showing the list of the most talked about players on social media during the 2016-17 summer transfer deadline day. There were 330,000 tweets about David Luiz, followed by Arsenal's Jack Wilshere, who was sent out on loan to Bournemouth. There were 108,000 tweets about the midfielder

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...