» » Walinzi wa Trump kuifanyia majaribio ndege ya ulinzi

Haki miliki ya pichaGETTY IMAGESImage captionWalinzi wa Trump kuifanyia majaribio ndege ya ulinzi

Walinzi wa rais wa Marekani Donald Trump wana mipango ya kufanyia majaribio ndege ya ulinzi isiyo na rubani wakati Trump atazuru klabu yake ya gofu huko New Jersey baadaye mwezi huu.

Ndege ndogo itafanyiwa majaribio na walinzi wa rais katika uwanja wa Trump National Golf Club huko Bedminster

Trump anatarajiwa kufanya ziara ndefu katika klabu hiyo.

Walinzi wa rais wanasema kuwa watazifanyia majaribio ndege kadhaa zisizo na rubani kwa masuala ya ulinzi.

Wakati wa shughuli hii ndege hiyo itaruka umbali wa kati ya futi 300 na 400 au mita 91 na 121 angani.

Trump aondoshwa jukwaani na maafisa wa usalamaWalinzi wa Netanyahu na wa rais wa Togo wazozana LiberiaErdogan kuwalinda walinzi waliopiga waandamanaji Washington

Ndege hiyo ina kamera pande tofauti na walinzi wa Trumo wanasema watajulisha watu katika klabu kuwa ndege hiyo itakuwa ikihudumu eneo hilo.

Walinzi hao wanasema kuwa makao ya kibinafsi yanaweza kunaswa na kamera za ndege hiyo.

Picha na video ambazo zinatarekodiwa na ndege hiyo zitafutwa baada ya siku 30.

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...