» » Askofu anayepinga ndoa za jinsia moja asusia mkutano Uingereza

Image captionAskofu anayepinga ndoa za jinsia moja asusia mkutano Uingereza

Mmoja wa viongozi wakuu wa kanisa la kianglikana nchini Uganda, amesema kuwa atahudhuria mkutano unaokuja wa viongozi wa kanisa la Anglikana ambao utafanyika mwezi Oktoba nchini Uingereza, kwa sababu hakubaliani na wale ambao wameanza kukubali ndoa za jinsia moja.

Askofu mkuu wa Uganda Stanley Ntagali aliiambia BBC kuwa hakuwa tayari kukutana na wale wanaokubaliana na kile alichokitaja kuwa ndoa zisizoambatana na mafunzo ya Biblia.

Polisi watibua ndoa ya wapenzi wa jinsia moja NigeriaWabunge Ujerumani waidhinisha ndoa ya jinsia mojaMahakama Taiwan yaidhinisha ndoa ya wapenzi wa jinsia moja

Alisema amefanya uamuzi huo baada ya kuomba ushauri kutoka kwa viongozi wengine nchini Uganda.

Wakatai wa mkutano uliopita wa viongozi wa dunia uliofanyika Januari mwaka 2016, Askofu Stanley Ntagali aliamua kuondoka mapema na kutisha kutorudi tena ikiwa hali hiyo haitarekebishwa.

Tangu wakati huo makanisa ya kianglikana ya Scotland na Canada yameunga mkono ndoa za jinsia moja.

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...