MTUNZI NA MWANDISHI-MWL YUSUPH ABEL NG'AHALA.
Sim no,0755683295/Watsap,instagram@mwalim_yuu, Email@yusuphngahala@gmail.com, Fb.com/Mwalimu Yusuph Abel Ng'ahala.
SEHEMU YA 46.
Tulipoishia, Wakati napitiapitia baadhi ya website za nyumbani nilikutana na habari ya kutisha kidogo. Niliona kama mtu kauawa hivi na maandishi chini. Nikaamua kuifungua ndipo nikakuta mi kweli aliyeuawa ni________Songa nayo.........Yule mkuu wa kituo ambaye alikuwa akinisaidia mambo mengi sana. Nilishtuka sana baada ya kusoma chanzo cha kifo chake. Alikuwa kauwa sawa na wale waliokuwa wanauawa kwa kukatwa vichwa. Nikajua tuu hapo huenda Zabroni kahusika kwasababu ile ndiyo mtindo wake wa kuua yaani kukata vichwa vya watu. Alikuwa hata akituma vijakazi wake huu ndo ulikuwa mtindo wake.
Nikaendelea, kufungua baadhi ya website za nyumbani. Nilikutana na mambo mengi mapya yaliyoendelea wakati sipo. Nikiwa bado naangalia zile picha na habari za nyumbani simu ya ndani ikaita. Yaani simu ya mezani ya mle chumbani. Nikaenda kuipokea na kusikia sauti ya kiume ikisema Yuu pole afande wangu najua unashangaa nimejuaje uko hapo. Yuu mimi Zabroni nilishashindikana na kila mtu. Nilikuona unanifuatilia nikatumia akili. Bahati mbaya umejaa. Nilipanda ndege ukanifuata kwa taarifa yako mi ndo niliiharibu ndege ikatuwa Nairobi na mimi nikarudi Tanzania kuuwa kwani nilijua ukiwepo kazi yangu itakuwa ngumu.
Aliendelea kujitapa katika simu akijidai kwa kusema, Ulijua wanifuata mimi kumbe umeniacha Tanzania. Pole sana natamani kukumaliza wewe na huyo baba yako ila kuna kitu kinanizuia. Siku nikivurugwa utanijua lakini siyo mbaya naona umeamua kufanya utalii Adis Ababa. Wakati nataka kujibu akakata simu. Nilijiona mimi ni mjinga sana nisiyetumia akili kwani Zabroni alikuwa akinizidi maarifa ya kawaida kabisaa. Nilikaa nikatafakari ni nani atakuwa kamwambia Zabroni ya kuwa mimi niko pale nikapata jibu ni yule malaya aliyekuja kujiuza pale kwangu. Kumbe alikuwa mpelelezi wa Zabroni. Ama kweli kuwa uyaone.
Nikafikiria nikaona jibu ni moja tuu kulipa kisasi. Nikainuka ili nitoke nje nikamtafute yule malaya ndani ya ile hotel. Nilitoka na kuzunguka mle ndani ya hoteli sikumpata. Nikaamua kwenda kuuliza mapokezi kama huwa kuna huduma hiyo ya wanawake kujiuza pale. Nilipofika nikajibiwa iyo huduma haipo pale na wala hairuhusiwi na Serikali ya Ethiopia.
Nikajua tayari nilikuwa nimeingiliwa na mvamizi. Basi nikamuuliza juu ya yule dada aliyekuja na kuja mpaka chumbani kwangu. Akajibu siku aliyokuja ilikuwa ni mara yake ya kwanza kumwona ila kwa mda ule hua anakuja mara nyingi tuu. Hata pale tulipokuwa tunaongea alikuwa katoka mda mfupi uliopita hata barabarani hajafika. Alivyosema hivyo nikaamua kutoka na kumfuatilia kwa nyuma. Nilifuatilia sana bila kumwona.
Mara nikiwa nimekata tamaa nikamwona anavuka barabara. Nikachomoa kisu na na kumvizia. Nilikuwa sijamwona vizuri usoni ila umbo na kutembea alikuwa ni yeye. Nikamkaribia na bila kujali wtu nikamrushia kisu kwa mafunzo niliyopewa jeshini bila kukosea kikampata maeneo ya tumbo. Hapo ilikuwa utumbo unatoka. Nilikuwa sijashitukiwa na mtu yeyete kwani wakawa wanakusanyana kumsaidia ndipo na mimi nikajichanganya katikati ya watu na kusogea karibu. Lakini niliona kama watanishtukia nikaamua kuondoka na kurudi hotelini haraka sana.
Chaajabu ni kuwa nilipofika getini nikapishana nq yule dada aliyekuja kujiuza kwangu. Nilipigwa na butwaa nikamwangalia kisha nikamsalimia alipojibu nikajua nimejiroga nilikotoka sijamuua mtu aliye stahili kifo. Ila nimemuua mtu mwingine. Basi kwa kiwa nilikuwa na hasira pale pale nikamkamata yule malaya na kumbana. Si ndipo akashindwa kujizuia akaongea kiswahili bwana niachie. Kisha akaanza kuongea kingereza nikajua hili windo sasa ni sahihi nilikuwa na pete ile yenye sumu kali ya kuuwa ilikuwa inavaliwa mkono wa kshoto.
Na lia nilikuwa na pete ya sumu ndogo isiyouwa il a inakuzimisha kwa mda. Nipo nikaamua kuitumia hiyo ili nipate kumuuliza vitu vingi akizinduka. Nikamchoma na kumwona taratibu analegea na kwenda chini. Alipoanguka mi nikamshika na kumbeba kwa mtindo fukani hivyo wakati napita mapokezi nilipita bila mashaka. Nikaingia chumbani kwangu kisha nikatoa pingu nikamfunga mikono na miguu mdada yule kisha nikawa Nasubiri azinduke kizha ataje wenzio.
Nikamsubiri amalize usingizi wa dawa. Hatimaye akazinduka na ndipo alishituka na kutumia sauti yake. Kwani ukiwa usingizini ukiamka kwa ghafla utatumia sauti halisi ambapo nilisikia sauti ni ya kiume. Nikashtuka sana. Kisha nijamwuliza vipi aliponiangalia nadhani alikua kuwa kashtuka tayari akabadilisha sauti na kuanza kuongea ya kike.
Nilijua tuu kuna namna pale siyo bure. Nikamzibua na kofi la haja. Kisha nikamshika nywele zile na kuzivuta kwa nguvu kama sehemu ya kumkkmoa. Kumbe wakati navuta ilonisaidia sana kwani nikagundua mgongoni mwa yule mtu kuna kitu kama zip, iko kwa shingoni nikaamua kummvha nguo kw lazima. Hapo ndipo Nilipo haribu kwani nilikuta zip imetoka shingoni mlaka kiunoni. Nikaamua kumfungua kwa nguvu. Ndipo nikagundua yule siyo mwanamke ila amevaa kitu kama mwili wa mwanamke wa Rangi nyeupe kama ya Waethiopia. Yaani ilikiwa unaivua kama koti. Basi nikaanza kumvua nikashangaa ninapomvua analia sana na kuongea ksa kiswahili akisema kaka yuu nisamehe. Nilishtuka kumwangalia mara mbili kisha nikamvua lile dubwana na kushitushwa na ninachokiona mbele yangu. Alikuwa ni mtu ambaye sikutegemea kabisa. Oscar, Oscar, Oscar hata wewe. Mpaka unaamua kuwa mke ili unizunguke vizuri?Alikuwa akilia tuh na kisha akanambia____________________________________
_____________________________ _________________
Tukutane sehemu ya 47 nikupe majibu. Nawapenda woteeeeeeee.
SIMULIZI YA KUSISIMUA-NANI KACHUKUA SURA YANGU? SEHEMU YA 46. Tu
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment