» » Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Latoa ripoti ya hali ya kisiasa nchini Burundi


Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limesema kuwa linasikitishwa na hali mbaya ya kisiasa nchini Burundi zikiwemo taarifa za ongezeko la idadi ya wakimbizi na taarifa za mateso, kupotea kwa watu na mauaji ya kinyama.

Katika ripoti hiyo ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, limesema kuwa limekusudia kuwachukulia hatua wale wote wanaohusika na matukio hayo ndani na nje ya nchi hiyo kwakuwa wanatishia amani na usalama wa Burundi.

Taarifa hiyo iliyosomwa na Balozi,  Amr Abdellatif Aboulatta wa Misri ambaye ndio mwenyekiti wa Baraza hilo, amesema kuwa baraza hilo linasikitishwa na hali mbaya ya kibinadamu inayoendelea Burundi ambapo zaidi ya wakimbizi laki mbili wamekuwa wa ndani, huku watu raia milioni tatu wakiwa na mahitaji na zaidi ya raia laki nne wakitafuta ukimbizi katika nchi za jirani.

Aidha, Baraza hilo limeshukuru nchi zinazopokea wakimbizi kwa jitihada zao, mataifa ya kikanda kwa kuheshimu wajibu wao wa kimataifa hasa katika kujali hadhi za wakimbizi na kuhakikisha wanarejea waliokotoka kwa hiari yao kwa kuzingatia uamuzi wao na taarifa za usalama na utu wa binadamu.

Hata hivyo,  Baraza hilo limelaani vikali matamko ambayo yamekuwa yakihamasisha vurugu na chuki dhidi ya raia ikiwemo wito wa kulazimisha kuwapa ujauzito wanawake na wasichana na kuitaka Serikali na pande zote kusitishmara moja vurugu na kulaani kauli zote za chuki.

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...