» » Tafeyoco Wataka kampeni ya ‘Baki Magufuli’ Ipigwe Marufuku

Serikali imeombwa kukomesha kampeni mbalimbali zinazoanzishwa ikiwamo ya 'Baki Magufuli' ili kuondoa sintofahamu iliyopo kwamba wenye kampeni hizo wanatumwa na Rais John Magufuli.

Hayo yamesemwa leo Alhamisi Agosti 3 na Shirika Lisilo la Kiserikali la Vijana na Wanawake (Tafeyoco) wakati wakizungumza na wanahabari kuhusu  hali ya utawala bora na demokrasia inayoendelea nchini.

Mwenyekiti wa Tafeyoco, Elvice Makumbo amesema kampeni hizo siyo muda wake kwa sasa kwani zinatachochea kuzalisha kwa kampeni nyingine hali itakayoleta mvurugano nchini.

"Tukiwaacha hawa wenye kampeni ya 'Baki Magufuli' watazaliwa wengine wenye kampeni ya 'Ondoa Magufuli' madarakani na wao watataka kuisambaza kampeni yao," amesema Makumbo.

Makumbo amesema ni wakati muafaka kwa Serikali kupiga marufuku kampeni hizo, kwani Tanzania inaongozwa kwa Katiba inayoeleza awamu ya kwanza ya rais ni vipindi vitano baada ya hapo uchaguzi mkuu mwingine unaitishwa.

Amesema Rais Magufuli anafanya kazi kubwa kuiongoza nchi na kwamba haitaji ‘tochi’ kupima uwezo wake hivyo kuanzisha kampeni za yeye kubaki ni kutengeneza chuki  kati yake na Watanzania ambao wanaikubali kazi yake.

Mbali na hilo, Makumbo amewataka viongozi wa vyama siasa nchini kuacha tabia ya kuwatumia vijana kuendeleza siasa katika mitandao ya kijamii, kwani baadhi ya vijana wanatumia nafasi hiyo kuandika habari za uchochezi dhidi ya Serikali.

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...