» » Mbunge CHADEMA Aendelea Kusota Rumande......Alikamatwa Jana kwa Tuhuma za Uchochezi


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Mathias Nyange amesema bado wanaendelea kumshikilia Mbunge wa Mbozi, Pascal Haonga na watamfikisha mahakamani baada ya kukamilisha upelelezi.

Kamanda Nyange amesema sababu za kumtia mbaroni Haonga ni kutokana na kufanya mkutano bila kibali cha polisi katika mji mdogo wa Mlowo-Mbozi na kuwahamasisha wamiliki wa malori na abiria kuandamana kwenda ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo, Chiku Galawa.

Amesema Haonga alifanya mkutano huo jana Jumatano, Agosti 2 na  alihamasisha madereva wa malori, wamiliki na abiria  waende kumuona mkuu wa mkoa.

Amesema lengo la mbunge huyo kuwataka watu hao wamuone mkuu wa mkoa ni  kueleza kero yao juu ya adha ya usafiri baada polisi kupitia kitengo cha usalama barabarani kupiga marufuku malori kubeba abiria kutoka katikati ya mji wa Mlowo kwenda maeneo tofauti ya vijijini ambako hakuna usafiri mbadala zaidi ya malori.

“Bado hatujakamilisha upelelezi na tutakapokamilisha muda wowote tutamfikisha mahakamani na kuhusu dhamana tutafikiria kumpatia dhamana ama laa,” amesema Kamanda Nyange.

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...