» » Urusi: Marekani imetangaza ''vita vya kibiashara'' dhidi yetu


Image captionPutin na Trump: Waziri mkuu wa Urusi Dmitry Medvedev amesema kuwa vikwazo vipya vilivyowekwa na Marekani dhidi ya taifa hilo ni sawa na kutangaza vita vya kibiashara.

Waziri mkuu wa Urusi Dmitry Medvedev amesema kuwa vikwazo vipya vilivyowekwa na Marekani dhidi ya taifa hilo ni sawa na kutangaza vita vya kibiashara.

Amesema kuwa mikakati iliotiwa saini na rais Trump inaonyesha udhaifu wa rais huyo wa Marekani ambaye alisema ameaibishwa na bunge la Congress.

Sheria hiyo inalenga kuiadhibu Urusi kwa kuingilia uchaguzi wa Marekani wa 2016 pamoja na vitendo vyake dhidi ya Ukraine.

Bwana Trump alilishutumu bunge la Congress kwa kupindua sheria.

Katika kutia saini makubaliano hayo dhidi ya adui wa Marekani kupitia sheria ya vikwazo siku ya Jumatano, aliweka taarifa akisema kuwa mkakati huo sio wa sawa.

Sheria hiyo pia inaiwekea vikwazo Iran na Korea Kaskazini.

Iran imesema kuwa vikwazo hivyo vipya vinakiuka makubaliano ya mpango wa nyuklia na kwamba itajibu kwa njia ilio ''sahihi na sawia'' kulingana na chombo cha habari cha Isna.

Haki miliki ya pichaREUTERSImage captionWaziri mkuu wa Urusi Dmitry Medvedev amesema kuwa vikwazo vipya vilivyowekwa na Marekani dhidi ya taifa hilo ni sawa na kutangaza vita vya kibiashara.

Korea Kaskazini kwa upande wake haijatoa matamshi yoyote kuhusiana na hatua hiyo ya Marekani.

Bwana Medvedev pia alionya kwamba hatua mpya zinazolenga kumuondoa rais Trump madarakani zitachukuliwa kwa kuwa sio mtu aliye na utaratibu.

Moscow ambayo imekana kuingilia uchaguzi wa Marekani tayari imelipiza kisasi wiki iliopita wakati bunge la Congress lilipopitisha muswada uliowatimua maafisa 755 kutoka katika ubalozi wa Marekani nchini Urusi mbali na kuzuiwa kutumia jengo moja la Marekani pamopja na ghala moja nchini Moscow.

Mataifa kadhaa ya Ulaya ikiwemo Ujerumani yanahofia vikwazo hivyo vipya na rais wa tume ya Ulaya Jean Claude Juncker ameonya kwamba athari yake itaathiri maslahi ya kawi ya Ulaya.

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...