» » Rais Magufuli aahidi neema nyingine Tanga

Rais John Magufuli amewaahidi wakaazi wa mkoa wa Tanga kuwa serikali yake itapanua bandari ya Tanga na kuhakikishia ina uwezo wa kufikiwa na meli kubwa zitakazokuwa zikisafirisha mafuta yatayovunwa kupitia bomba linalotarajiwa kujengwa kutoka Hoima nchini Uganda hadi jijini humo.

Akiuhutubia umati wa wananchi waliohudhuria sherehe za uzinduzi wa mradi huo uliofanyika eneo la Chongoleani akiwa na mgeni wake Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, Rais Magufuli alisema kuwa amesikia kilio cha wananchi wa Tanga kupitia kwa Mkuu wa Mkoa huo na kwamba atalifanyia kazi kwa vitendo.

“Haiwezekani tukawa na mahali ambapo meli kubwa-kubwa zinakuja kwa ajili ya kuchukua mafuta ghafi halafu kina cha maji kiwe kidogo. Kwahiyo, tutapanua pia bandari ya Tanga ili tuwe na bandari tatu kubwa,” amesema Rais Magufuli.

“Kama tunavyopanua bandari ya Mtwara, kama tunavyopanua bandari ya Dar es Salaam na bandari ya Tanga tutaipanua ili kina chake kiongezeke; ili wananchi wa Tanga waweze kufanya biashara,”aliongeza.

Katika hatua nyingine, Rais Magufuli pia aliahidi ujenzi wa barabara mpya itakayounganisha jiji la Tanga na Bagamoyo ambayo itaratibiwa na jumuiya ya Afrika Mashariki.

Rais Magufuli na Rais Museveni wanazindua ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Ohima nchini Uganda hadi mkoa wa Tanga, ujenzi unataorajiwa kuchukua takribani miaka mitatu


Tuma picha/ habari what-sap 0769436440



BONYEZA HAPA KUPATA APP YA 4SN NEWS



tupe maoni yako

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...