» » Angalia Lowassa alipokuwa Kenya Kumnadi Uhuru Kenyatta

Zilikuwa zimebaki siku mbili nchi ya Kenya kufanya Uchaguzi Mkuu, Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Edward Lowassa amefunguka sababu kuu zinazofanya amtetee na kumnadi mgombea Urais kupitia chama cha Jubilee Uhuru Kenyatta kuwa ni kiongozi shupavu.

Lowassa ambaye jana alishiriki katika mkutano wa chama cha Jubilee alisema kuwa kuna watu wanauliza kwanini yeye pamoja na CHADEMA wanamnadi kwa kuwa kiongozi huyo ni shupavu na mpenda watu.

"Kuna watu wananiuliza kwanini mnamnadi Uhuru Kenyatta, nasema tena hadharani bila aibu yoyote huyu ni kiongozi shupavu anayependa watu, anaweza kuongoza watu wetu, lakini cha pili Uhuru Kenyatta anapenda Afrika Mashariki akiingia madarakani ataturuhusu tuendelee kuzunguka zunguka kwenye mipaka hii kama Namanga pale bila hata shida, la tatu ni kwamba aliingia madarakani nchi ikiwa kwenye vita lakini amewapa suluhu ameingoza nchi imekwenda taratibu na akafanikiwa" alisema Lowassa

Mbali na hilo Lowassa alisema kuwa licha ya mambo yote hayo lakini bado ukweli utabaki palepale kuwa Uhuru Kenyatta anapenda Demokrasia

"Tangu Demokrasia ya vyama vingi Uhuru Kenyatta hajaleta shida ya aina yoyote, siku moja nimeona kwenye TV yenu mama mmoja amemtukana mpaka matusi ya nguoni lakini asubuhi Rais anasema nimemsamehe bure, nawaambia huyu ndiye anawafaa, naondoka nikiwa na matumaini" alisema Lowassa

Siku ya Jumapili tarehe 8/8/2017 Wananchi wa Kenya watakuwa wakifanya uchaguzi kuchagua viongozi wao mbalimbali 

Tuma picha/ habari what-sap 0769436440


BONYEZA HAPA KUPATA APP YA 4SN NEWS



tupe maoni yako

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...