» » Trump aunga mkono makubaliano ya kuiwekea vikwazo Urusi


Image captionKashfa ya Urusi kuingilia uchaguzi wa Marekani imeendelea kumsumbua Trump

Ikulu ya White House imesema kuwa Rais Donald Trump, anaunga mkono makubaliano yasiopendelea upande wowote yaliyoafikiwa katika bunge la Congress ya kuiwekea vikwazo Urusi.

Imesema kuwa Rais Donald Trump, anaunga makubaliano yasiopendelea upande wowote yaliyoafikiwa katika bunge la Congress ya kuiwekea vikwazo Urusi.

Afisa habari wa Ikulu ya White House Sarah Huckabee-Sanders anasisitiza kuwa, licha ya hatua hiyo awali white house ilipinga mswada wa uamuzi huo, japo kuwa kwa sasa inafurahia mswaada wa mwisho uliopitishwa.

Image captionPutin amekana nchi yake kuhusika kuingilia uchaguzi huo

Bunge la Congress linataka Urusi iadhibiwe kwa madai ya kuingilia uchaguzi wa urais uliofanyika mwaka jana nchini Marekani.

Bunge hilo linatarajiwa kupiga kura hapo kesho siku ya jumanne kupitisha muswada huo kuwa sheria inayoitaka ofisi ya Rais kutoingilia mwenendo wa hatua za kidplomasia dhidi ya Moscow.

Ikulu ya white house hata hivyo imekuwa na kauli zinazotofautiana mara baada ya msimamo wa bunge la Congress katika vikwazo vipya dhidi ya tuhuma za Urusi.

Kupitishwa kwa sheria hiyo na bunge la congress kutamnyima uwezo Rais Trump, kuondoa kikwazo chochote kitakachopitishwa dhidi ya Urusi.

Urusi imeendelea kupinda shutuma za kuingilia uchaguzi huo.

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...