» »Unlabelled » Mkuu wa kukabili rushwa Kenya Philip Kinisu ajiuzulu

Mkuu wa kukabili rushwa Kenya Philip Kinisu ajiuzulu


M

Bw Kinisu alipokuwa akiapishwa Novemba mwaka jana
Image captionBw Kinisu alipokuwa akiapishwa Novemba mwaka jana

Mkuu wa tume ya kupambana na rushwa Kenya (EACC) Philip Kinisu, amejiuzulu siku moja baada ya kamati ya bunge kupendekeza afutwe kazi kwa sababu ya muingiliano ya maslahi.
EACC ilikuwa inatakiwa ifanye uchunguzi kuhusu tuhuma za ufisadi katika Huduma ya Vijana kwa Taifa (NYS) ambayo hufadhiliwa na serikali.
Lakini kampuni ambayo inamilikiwa na Bw Kinisu inadaiwa kushiriki katika shughuli za kibiashara na NYS.
Wabunge walikuwa wamemuomba Rais Uhuru Kenyatta aunde jopo la kumchunguza, na kuamua iwapo anafaa kufutwa kazi.
Bw Kinisu, ambaye ni mwenyekiti wa zamani ya kampuni ya wahasibu ya PwC Afrika aliteuliwa kuongoza tume hiyo Novemba mwaka jana.
Amesisitiza kwamba hana hatia na kusema badala yake watu wanafaa kuangazia "ufisadi".
Kuondoka kwake kutamfanya kuwa mkuu wa tume ya kupambana na rushwa Kenya aliyehudumu kwa kipindi kifupi zaidi.
Watangulizi wake wawili waliondolewa kazini baada ya kukabiliwa na tuhuma na shutuma, zikiwemo kutowajibika kazini.

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...