MTUNZI NA MWANDISHI-MWL YUSUPH ABEL NG'AHALA.
Sim no,0755683295/Watsap,instagram@mwalim_yuu, Email@yusuphngahala@gmail.com, Fb.com/Mwalimu Yusuph Abel Ng'ahala.
SEHEMU YA 43.
Tulipoishia, Wakati tumefika getini ile nafungua geti nje kulikuwa na kondi la majambazi. Mbele alikuwapo Peris na wengine walikuwa wamejipanga sana. Waliniangalia kwa kiasi kisha_____Songa nayo....... Milio ya risasi ikaanza kusikika kutokea upande wao wa nyuma. Hali ile iliwafanya wageuke kukabiliana na risasi zinazotoka nyuma yao. Na hiyo ndo ikawa nafasi yangu ya kukimbia. Nilimchukua baba yangu na kumpitisha juu ya ukuta na kumwachia kwa chini. Niliumia sana mikono kwani baba alikuwa hajiwezi hali iliyofanya nitumie nguvu nyingi sana.
Sikujali kuumia kwani lengo ilikuwa kumwokoa baba yangu na hilo lilifanikiwa. Hali ile ilinifanya nipate nguvu mpya. Nikamtoa na kutoweka eneo lile. Nilijiuliza ni akina nani walikuwa wakiwashambulia kwa nyuma sikupata jibu kwakweli. Nilimfikisha baba sehemubsalama na kuanza kumuhudumia nilimpa uji na kumuogesha. Baada ya mda akaanza kurudi katika hali yake ya kawaida. Nilimshukuru sana Mungu kwa hilo. Kisha niliamua kutoka na kwenda kufuatilia ni nini kikijiri kwani hali sasa ilikuwa imeanza kurejea kwenye usalama. Pia pale nilipokuwa nimejificha walikuwa hawezi kupatambua kutokana na simu ambayo ingeonyesha niko wapi niliizima lakini pia nilitoa kilichokuwa kinaonyesha niko wapi.
Nilitoka mpaka kwenye ile nyumba ambapo nilikuta hali ya usalama imetawala. Hapakuwa na fujo tena. Ila pale chini palizagaa damuu na kufanya palowane kama vile mvua ilinyesha. Nikawa najiuliza nini kimejiri baada ya mimi kuondoka. Sikupata majibu nikaamua kuondoka. Nikiwa njiani nikawasha simu na kumtafuta yule mkuu wa kituo ambaye ni mpenda haki sana. Baada ya kupokea simu nikasikia akisema Yuu afadhali umenipigia mana mimi nilikutafuta mara kadhaa ulikuwa hupatikani. Sasa naona mambo yanaelekea kuwa mazuri siku si nyingi serikali itajua ukweli wa mambo.
Nikamuuliza kwanini unasema hivo mkuu. Akajibu hebu njoo ofisini kwangu tuongee. Nikakata simu na kumfuata ofisini. Baada ya kufika akanieleza kuwa yeye ndiye aliandaa kikosi kuja kufanya shambulio pale hivyo majambazi wengi wamekamatwa wengine wamekufa wengine majeruhi na wengine walikimbia.
Akaniambia kuwa kuna maiti zaidi ya 10 na majeruhi kama wanne hivi. Lakini waliokimbia hawazidi watatu ni mwanamke mmoja na wanaume wawili. Hapo nikajua tuu Peris kafanikiwa kukwepa mkono wa sheria. Lakini kilichonifurahisha ni kuwa kazi imepunguzwa hivyo kwa sasa nitakuwa natafuta kukutana na Zabroni bila vikwazo vingi kama mwanzo kwani mtandao wake ulipunguzwa sana. Yule mkuu alinipongeza sana kisha akanambia sasa hivi kila hatua nitakayoiendea nimtaarifu. Nikamjibu sawa lakini moyoni nikajisemea mimi sina imani na binadamu wewe imekula kwako.
Kwa hatua niliyokuwa nimefikia hata angekuwa rais au nani haikuwa rahisi kumwamini mtu. Nikatoka na kwenda nyumbani nilikomficha baba. Huku nilijua wale waliopewa jukumu la kunilinda kama mimi ni kichaa watakuwa matatizo kutoka na kutoweka kwangu. Nilimkuta baba akiwa katika hali yenye unafuu. Nikaa naye mpaka asubuhi ambapo niliamua kwenda kumfuatilia Zabroni. Nilimwachia baba pesa ya kutosha ili kama nikifa huko aishi kwa pesa hizo. Baba yangu kabla sijaondoka aliniita kisha akaniwekea mikono kichwani na kusema mwanangu utafanikiwa.
Hapo ndipo nilipotoka na morali ya kumkamata Zabroni. Nilikuwa nimepenyezewa taarifa na chanzo changu cha siri kuwa Zabroni yuko mahali fulani. Ilikuwa yuko uwanja wa ndege na alionekana kama aliyekuwa akisubiri safari. Basi nikafanya haraka na kufika uwanjani pale baada ya nusu saa. Baada ya kufika nilihangaika kumtafuta kila kona Zabroni sikumwona. Nikajitahidi mpaka nikaingia kwenye ndege ambayo ilikuwa inaondoka baada ya dakika chache. Lakini sikumwona. Nikapata wazo nikaangalie orodha ya wasafiri
Baada ya kumwonyesha muhudumu kitambulisho changu alinipa orodha ile huku nikiwa naangalia nikaona ndege iko tayari kuruka. Ilikuwa ni ndege inakwenda Ethiopia na hapo ndipo nikamwona Zabroni akipunga mkono kwenye mlango wa ndege kisha mlango ukafungwa. Na hapo ndege ikaanza kuondoka. Niliingiwa na hasira sana nikajiuliza huyu Zabroni ni jini? Alijificha wapi. Baada ya kuona jina lake alikuwa akielekea Ethiopia Adis ababa.
Nikaona njia pekee hapa hakuna namna. Ni kumfuata tuu. Baada ya kupata hilo wazo nikaKata tiketi hapohapo kwa bahati nzuri kuna ndege iliyokuwa inatoka ikipishana na ile iliyotoka dakika 10 tuu pia hiyo ilikuwa inaenda Ethiopia hivyo nikawa nimepata usafiri. Nilitoa passport yangu kisha nikaingia kwenye Ndege. Nilitamani kumwambia rubani aondoe ndege haraka lakini asingeweza hivyo uvumilivu ulilazimika.
Baada ya dakika kadhaa ile ndege ikaaondoka hivyo safari ya kuelekea Ethiopia ikawa imeiva. Nilipoangalia saa ni kweli tulipishana na ndege iliyotoka dakika kumi. Hivyo nikajua tutafika huenda ndege ikawa bado haijafungua mlango au tutakuta abiria ndo wanashuka. Nikajipa moyo na kusema leo ndio leo asemaye kesho ni mwongo namwulia Zabroni nje ya nchi halafu nikirudi Tanzania sitaki yeyote ajue.
Safari iliiva na kufika Ethiopia ambapo baada ya ndege yetu kutua ile ndege niliiona nayo ndo kwanza inatua hivyo tulifika kwapamoja. Hali ile ilinishangaza kwani ndege haziwezi kufika wakati mmoja hivyo nikawa tayari nina mawazo. Baada ya sisi kushuka abiria wa ile ndege iliyokuwa imetangulia nao wakafunguliwa mlango na kuanza kutoka. Nikatoa bastola yangu kisha nikajiweka sawa. Sikujali kama ni uwanjani. Kizuri ni kwamba watu walikuwa wengi sana hivyo nisingeonekana. Nilipepesa macho na nisimwone Zabroni. Lakini nikajipa moyo kwani watu waliendelea kutoka Sikuamini macho pale nilipoona _________________________________________________________,______________________________________________________________________,,________________________________Check na mm sehemu ya 44 nikupe yaliyojiri huko Ethiopia au vipi? Nawapenda sana.
SIMULIZI YA KUSISIMUA-NANI KACHUKUA SURA YANGU? SEHEMU YA 43.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment