headlines

    07:42
» » Shambulizi la bomu lawaua watu 24 Kabul


Haki miliki ya pichaREUTERSImage captionShambulizi la bomu lawaua watu 24 Kabul

Shambulizi la bomu limesababisha karibu vifo vya watu 24 kwenye mji mkuu wa Afghanistan Kabul.

Kwa mujibu wa wizara ya ya mambo ya ndani nchini Afghanistan, takriban watu 42 pia walijeruhiwa wakati wa mlipuko huo.

Wapiganaji waliovalia kama madaktari washambulia hospitali Kabul

Mshambuliaji wa kujitoa mhanga alijilipua katika eneo lenye washia wengi magharibi mwa mji.

Lengo la shambulizi hilo halikutajwa mara moja na hakuna mtu aliyedai kuhusika.

Image captionShambulizi la bomu lawaua watu 24 Kabul

Shambulizi hilo llitokea karibu na nyumba na afisa wa cheo cha juu serikalini, Mohammad Mohaqiq.

Hakuna kundi la kigaidi lililodai kuhusika.

Bomu la kutegwa, laua watu 80 Afghanistan

Mashambulizi ya awali yamedaiwa kutekelezwa na Taliban au kundi la Islamic State.

Kabul umekumbwa na misururu ya mashambulizi likiwemo lililowaua watu 90 wakati lori lililipuka mwezi Mei.

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Trump aunga mkono makubaliano ya kuiwekea vikwazo Urusi
»
Previous
Vitisho vya China vyasababisha Vietnam kusitisha uchimbaji wa gesi baharini

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...