» » Vitisho vya China vyasababisha Vietnam kusitisha uchimbaji wa gesi baharini


Haki miliki ya pichaAFPImage captionVitisho vya China vyasababisha Vietnam kusitisha uchimbaji wa gesi

Vietnam imesitisha shughuli ya uchimbaji gesi katika eneo linalozozaniwa kusini mwa bahari ya China, kufuatia vitisho vikali kutoka China.

Taarifa zinaiambia BBC kuwa kampuni iliyokuwa ikiendesha uchimbaji huo iliamrishwa kuondoka eneo hilo.

Inajiri siku chache baada ya kampuni ya Respol kusema kuwa imegundua gesi nyingi.

China yazindua manowari mpya ya kijeshi

Ripoti zinasema kuwa wakurugenzi wa Respol waliambiwa wiki iliyopita na serikali wa Viertman kuwa China ilikuwa imetisha kushambulia vituo vyake katika visiwa vya Spratly ikiwa uchimbaji huo haungesitishwa.

Image captionVitisho vya China vyasababisha Vietnam kusitisha uchimbaji wa gesi

China inadai kuwa karibu eneo lote la kusini mwa bahari ya China ni lake, visiwa ambavyo pia vinavyodaiwa na mataifa mengine.

China: Hatua ya meli ya Marekani kukaribia kisiwa ni uchokozi mbaya

Vietnam inaliita eneo hilo Block 136-03 na imeipa zabuni kampuni inayoitwa Talisman-Vietnam.

China nayo inaliita eneo hilo Wanan Bei-21 ikiwa imetoa kandarasi kwa kampuni tofauti.

Haki miliki ya pichaAFPImage captionVitisho vya China vyasababisha Vietnam kusitisha uchimbaji wa gesi

Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About IVST TANZANIA

Hi my name is Gasto Alex Didas
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...

Popular Articles