» » Ufyatuaji risasi watokea kwenye ubalozi wa Israel nchini Jordan


Haki miliki ya pichaAFPImage captionVikosi vya usalama vimefunga barabara eneo hilo

Watu wawili raia wa Jordan wameuawa na muisrael mmoja kujeruhiwa wakati wa kisa cha ufyatuaji risasi kwenye ubalozi wa Israel katika mji mkuu wa Jordan Amman.

Watu hao walikuwa wakifanya kazi na kampuni moja ya zamani na waliingia ndani ya ubalozi kabla ya ufyatuaji risasi kuanza kwa mujibu wa polisi.

Ripoti chache zimetolewa kuhusu kile kilisababisha kutokea kwa ufyatuaji huo wa risasi.

Vikosi vya usalama vimezingira ubalozi huo na utawala wa Israel umewahamisha wafanyakazi.

Ufyatuaji huo ulitokea katika jengo moja linalotumiwa na ubalozi wa Israel.

Israel yafungua eneo takatifu JerusalemPolisi wawili wa Israel wauawa JerusalemIsrael kujenga nyumba 560 mashariki mwa Jerusalem

Mamlaka za Israel hazijazungumzia kisa hicho.

Ubalozi huo wenye ulinzi mkali uko mtaa wa Rabiyeh ambalo ambao ni wa kifahari mjini Amman.

Siku ya Ijumaa maelfu ya watu waliandamaa mjini Amman kupinga hatua ya Israeal ya kuweka vifaa vya kutambua chuma katika aneo takatifu kwa waislamu na wakiristo mashariki mwa Jerusalem.

Haki miliki ya pichaGETTY IMAGESImage captionRipoti chache zimetolewa kuhusu kile kilisababisha kutokea kwa ufyatuaji huo wa risasi.

Mshirikishe mwenzako 

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...