SIMULIZI YA KUSISIMUA-NANI KACHUKUA SURA YANGU?
MTUNZI NA MWANDISHI-MWL YUSUPH ABEL NG'AHALA.
Sim no,0755683295/Watsap, instagram@mwalim_yuu, Fb.com/Mwalimu Yusuph Abel Ng'ahala, Email@yusuphngahala@gmail.com.
SEHEMU YA 41
Tulipoishia, Nilitoka na kurudi kujificha mpaka siku ya pili ndipo nikarudi kuchukua majibu. Nilimkuta daktari yule ambapo akaniuliza maswali kadhaa kisha akanikabidhi majibu ambayo yalionyesha kuwa____songa sasa.......Yule ni baba yangu aliyezikwa. Nilimwangalia daktari nikaona kama ana woga fulani nikaona dawa ndogo tuu ni kujitoa akili nikainuka kama vile naondoka kisha nikamgekia na kofi la kushtukiza halafu nikamtemea lita nzima ya mate usoni. Wakati anashangaa nikamkuda kisha nikambeba juu juu toka pale alipo nikampitisha juu ya meza huku vimiguu vikining'inia nikamtua upande wangu.
Kisha nikamwangalia usoni huku ndita zikiwa zimejipanga kama matuta ya viazi. Nikamuuliza kwa mara nyingine nataka majibu ya ukweli ni yanaonyesha nini? Akajibu kweli mheshimi......... Kabla hajamaliza nikamsukuma kisha nikamwuliza mbona una wasiwasi umenisaliti eee sasa sikia....... Kabla sijasema simu yake ikaita nikampora na kupokea kisha nikasikia oya uyo mwanaharamu kwenye "location" anaonekana hapo hospitalini nadhani anakuja kuchukua ajibu fanya kama tulivokueleza tutakulinda sawa dokta?
Nikapata jibu kumbe nachoreshwa eee sasa nikaona dawa ni moja tuu. Yule daktari atanisaidia kibabe. Nikamfuata na kumwambia chagua moja mauti au unisaidie mimi! Kwa mikiki mikiki aliyopata mda mfupi alijua tuu huyu mtu kapagawa. Akainua uso na kuniangalia kisha akasema samahani nilikugeuka haikua dhamira yangu. Basi nikaona hapa nimepata msaada. Nikamwambia sasa fanya hivi tunatoka mimi na wewe kuelekea nje kisha utanifuata mimi hsionyeshe kama tuna ugomvi. Nimeua watu wengi sitaogopa kukuua kama utashindana na mimi uko tayari kusuka au kunyoa? Akajibu huku akitetemeka twende mkuu naipenda familiya yangu.
Basi tukatoka wote mpaka sehemu fulani pana jumba ambalo watu hawakai. Ilikuwa ni nyumba ya mtu ninayemfahamu hivyo nilikuwa na funguo nikaingia humo na yule daktari kisha nikaanza kumuhoji mambo mbalimbali juu ya wale majambazi. Kwa kuwa alihitaji kuokoa nafsi yake aliongea vitu vingi sana mpaka kunitajia wanapojificha. Akaongeza kuwa sababu ya wao kujua kila nilipo ni kwamba kuna siku wakati wamenichoa sindano nikalala walimwita yeye mwenyewe alinifanyia upasuaji mdogo maeneo ya shingo. Hapo waliweka kifaa kidogo chenye mawasiliano yao ya kujua mtu alipo. Hivyo hata pale walijua na ndiyo mana nashindwa kuwatia nguvuni. Akasema hata yeye kupokea ile mifupa aliandaliwa lengo lao ni kuwa niamini kuwa yule ni baba yangu aliyezikwa halafu baba yangu halisi wana shida naye sana tuu.
Hivyo wakati nafika alinipokea kwa haraka ila hakuwa zamu siku hiyo. Nikamwambia je hicho walichoniweka huku shingoni waweza kukitoa akajibu hata sasahivi mkuu kikubwa ujikaze kwasababu hamna ganzi. Nikajibu hebu toa kisha nikamgeuzia shingo. Basi akatoa kitu kana kiwembe kisha akanichanja na Baada ya sekunde kama 14 hivi akasema tayari hiki hapa. Akanipa kilikuwa ni kidogo sana kama punje ya mchanga. Nikakichukua na kukiangalia kisha nikamgeukia daktari. Nikamwambia ahsante kwa ushirikiano ila siku hizi sina imani na mtu. Nikamshika shingo na kumuua palepale kisha nikatoweka na kile kitu mpaka nyumbani kwangu. Nikakaa kidogo mara kuna mbwa wa jirani alikuwa pale nje nikaamua kukiingiza kile kifaa masikioni mwa yule mbwa. Ili wakiniangalia waone mahali alipo mbwa.
Kisha nikarudi ndani na kujipumzisha kiasi. Nikawa nimeshajua kuwa kumbe baba yangu yu hai. nilianza kuwaza jinsi ya kumpata baba yangu. Kikubwa kilichonifariji ni kuwa sasa hawatajua nilipo. Nikalala mpaka usiku kisha nikaamua nitoke nikalie doria nilipoelekezwa kuwa wanapatikana. Nikaenda mpaka eneo lile na kuangalia ilikuwa ni jumba la kifahari sana hata kuingia ilikuwa ni kuhatarisha maisha nikaangalia vizuri. Kwaku wa ilikuwa usiku nikashindwa kuipata ramani vizuri. Nikapanga nitarudi mchana ili niangalie vizuri nijue nitaingilia wapi. Na pia kikibuma nitatokea wapi? Nilitoka na kurudi nyumbani. Siku ya pili nikarudi mchana ambapo niliichora ramani vizuri sana kisha nikapanga usiku kuharibu mambo.
Nikarudi nyumbani na kusubiri usiku uingie ili nifanye mambo ya maana. Usiku ulifika nikatoka na kuelekea kwenye lile jumba la kifahari. Nilifika na kukuta pilikapilika zikiendelea watu walikuwa wakizungukazunguka mle ndani. Nikaangalia wapi penye giza ili niingilie hapo. Nikaona kuna sehemu taa za umeme hazimuliki. Nikarusha kamba na ikanasa. Taratibu nikakwea na kuingia nikafanikiwa kutua kimyakimya kisha nikajifunga vizuri na kuandaa silaha zangu. Nilijua mle ndani hawawezi kukosa silaha. Hivyo mbinu pekee ilikuwa ni kuua kimya kimya kisha niondoke nirudi siku nyingine.
Nikaanza kuwavizia wale wote wanaotoka na kuingia Nilimvizia wa kwanza nikamvuta kwenye giza nikachinja. Kisha nikatega mingo tena. Mara nikamwona mtu mwingine anatoka mle ndani nikamvizia nikamkuta nikamchoma tuu na ile sindano yangu ya sumu. Alianguka kwa kishindo puu!!! Hali ile iliwafanya waliomo ndani watoke kushuhudia ni nini? Hapo lilikuwa kosa kwao kwani malengo yangu yalitimia walipotoka mi nikaingia ndani na kujificha mahali.
Usiku ule walipagawa wakakagua kuzunguka nyumba lakini hawakumwona mtu. Ndipo wakaamua kurudi ndani. Walikaa mpaka kama saa saba hivi wakijadili uvamizi ule. Nilwasikia wakisema lakini mbona Yule mwanga haionyeshi yuko hapa! Huenda ni mwingine yule tungejua. Nikajua kumbe ndo mana nilikuwa sifanikiwi sasa mmekwisha ndo niko ndani mwenu. Nawasubiri mlale nichinje raia wa kutosha kisha nipotee.
Mda ukasonga mimi nikiwa pale huku nikiwa nasikia sauti ya mwanamke kama Peris vile. Kumbuka Peris alirudishwa kazini hivyo kama yuko pale maana yake kasaliti jeshi la polisi kwa mara ya pili. Nilisubiri sana pale walale lakini hali ilikuwa tofauti mda kama wa saa sita hivi nilikuta wanaandaa silaha wakidai kuna sehemu kuna pesa zaidi ya milioni 300, Hivyo waliokufa waliwapotezea. Nilikaa pale mda ulisonga sana lakini walikuwa ndio wanazidi kuondoka. Mara kwa mbali nilisikia mlio wa viatu mtu akija maeneo niliyojificha. Mara akapita na kuwa kama kahisi kitu akaanza kurudi niliko kisha_______________,___________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________Hahahahahaaaa nategemea kusikia fupi, ongeza urefu. Mashabiki wangu bhana nimeongeza sasa bado mtalamika? Hopely hapana tukutane sehemu ya 42 niwape michapo.
SIMULIZI YA KUSISIMUA-NANI KACHUKUA SURA YANGU? SEHEMU YA 41
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment