headlines

    07:42 AM M
» » SIMULIZI YA KUSISIMUA-NANI KACHUKUA SURA YANGU? SEHEMU YA 42.


MTUNZI NA MWANDISHI-MWL YUSUPH ABEL NG'AHALA.
Sim no,0755683295/Watsap,instagram@mwalim_yuu, Email@yusuphngahala@gmail.com, Fb.com/Mwalimu Yusuph Abel Ng'ahala.
SEHEMU YA 42.
Tulipoishia, Peris akadakia mkuu anywe yeye ikiwa hatakufa atahukumiwa kwani ametuhumu jeshi la polisi uwongo. Mana jeshi ndio limesimamia. Basi mi kwa hasira nikaichukua na kuinywa kisha baada ya sekunde kadha Nikaona_____Songa sasa.......Hakuna hali yoyote mpya naiona inayoashiria mabadiliko. Nikaanza kuingiwa na woga. Watu wote walikuwa wamesima na kutulia tulii wakishangaa kinachoendelea. Nilikaa zaidi ya dakika kumi huku kimya kimetanda lakini hapakuwa na mabadiliko yoyote.
Hapo ndipo kelele zikaanza, Apigwee! Apigwe! Anadanganya mbele ya umma apogwe. Mvua ya mawe ya kurushwa yakaanza kunielemea nilipigwa haswaa. Kisha polisi wakanitoa na kunipeleka kituoni. Niliingizwa mahabusu na kuachwa humo. Baada ya mda akaja Peris akasimama mlangoni na kuniambia Yuu pole sana. Hii dunia ya wabunifu kwanini hutumii akili. Sisi hatuwezi kumuua waziri pale mbele ya kadamnasi. Tutamuua wakati wowote tukijisikia kufanya hivyo na hakuna wakuzuia hilo. Ulikua mume wangu ila maamuzi yako ya kukurupuka sana.
Hata sisi tulivyoona notebook haipo tulijua siri imeshavuja tukagairi. Ona sasa unahukumiwa kwa kutaka kuokoa maisha ya mtu. Pole sana. Kisha akaondoka kwa mwendo wa kunesanesa akininringishia majaliwa ya mwenyezi Mungu Subhan Wataala. Unadhani akili yangu ingekua inaangalia maumbile badala ya kuumia. Ilikuwa ni maumivu makali yasiyovumilika hasa pale nilipoujua ukweli kuwa waligairi Nilibaki pale nalia huku nikikumbuka mambo mengi niliyowahi kufanya na Peris. Ama kweli. Basi nikapelekwa mahakamani kwa tuhuma mbalimbali, ikiwemo kutoroka jela, kuua watu na kudanganya mbele ya umati mkubwa nikituhumu jeshi la polisi ni wauwaji. Kutokana na kile kitendo hakimu alishauri nikapimwe hospitalini. Huenda akili yangu haiko sawa. Baada ya kupelekwa hospitalini nilipimwa na daktari mmoja hivi. Ambapo kwa mbali nilimwona Yule mkuu wa kituo ambaye nilimpelekea majambazi.
Baada ya kumwona alinionyeshea ishara ya kuwa nisijali nitakuwa sawa. Hapo akaenda zake. Baada ya siku mbili nikiwa mahabusu majibu yakaletwa kwenye kituo cha polisi na mahakamani. Majibu yalionyesha mimi nina maratizo ya akili ambayo imesababishwa na msongo wa mawazo. Hivyo mambo mengi nafanya bila kujijua. Ilipofika siku ya hukumu ambapo ilikuwa ni siku iliyofuata. Nilipelekwa mahakamani na kusomewa hukumu.
Kisha hakimu akasema kwa kuwa imethibitishwa kuwa na matatizo ya kiakili. Hivyo naachiwa huru kwani niliyafanya yote kwasababu sina akili nzuri. Akashauri pia kuwa chini ya uangalizi maalumu. Ambapo aliamuru madaktari wa muhimbili waniangalie mpaka akili yangu itakaporudi katika hali yake ya kawaida. Basi nikaachiwa huru na kurudi uraiani japo nilikuwa chini ya ulinzi mkali ili nisilete madhara mengine.
Maisha yalianza huku nikiwa naangaliwa kwa ukaribu sana. Kuna siku nikaamua kwenda kwa yule mkuu. Ndipo akanambia yeye ndiye alimshinikiza daktari kutoa majibu ya uongonili nimalize kai niliyoanza. Ila kwa tetesi ni kuwa Zabroni na kundi lake wameanza kuwa na mashaka. Hivyo huenda vipimo vikawa na uhitaji wa kurudiwa. Lakini usijali Yuu nipo kwaajili ya kukutetea kwasababu unapigania taifa.
Sintakuangusha kamwe, nilimshukuru sana na nikamuaga na kurudi nilipoambiwa niishi. Nilikuwa naishi kwa kulindwa sana mausha yale sikuyapenda kwani nilizoea uhuru. Lakini kwa sasa hali ilikuwa tofauti kutoka nilikuwa nalazimika kutoroka. Basi kuna siku niliwadanganya wale walinzi nakuwazubaisha kisha mimi nikaruka ukuta na kwenda kuendelea na kazi yangu. Nilitoka na kufika kwenye jumba moja hivi na hapo pia nilielekezwa kuwa ni makazi yanayotumiwa mara nyingi na wahalifu.
Niliruka na kuigia ndani ambapo nilianza kua walinzi wa pale na kisha nikaingia nda ni na kuanza kupekua pekua vitu. Mara ghafla nilijikuta natokea sehemu ambayo ina uwazi hivi. Huku nilimwona baba yangu akiwa kafungwa kwenye nondo. Niliumia kwani hata mdimo walimziba. Nikamkimbilia baba kwa machozi ya furaha kumwona tena nilitiririsha.
Nikaona nispoteze mda nikamfungua baba kwenye zile kamba na lumtoa yale mabandeji msomoni. Alikuwa amekonda sana na mwenye kulia kama mtoto. Niliumia sana kuona chozi la baba. Hakika niliumia nikaapa kulipa kisasi kwa yeyote aliyehusika. Kwakuwa kuna vitu vingine vilikuwamo mle ndani. Nilivikusanya ninavyoviona vya muhimu sana.
Kulikuwa na Cd nyingi sana ambazo zilifichwa na hizi nilizibeba. Nikachukua baadhi ya sura za bandia zilizokuwa mle ndani. Pia nilifanikiwa kuchukua baadhi ya vifaa vya kisasa vya kunasa Hakika mle nilifika mahali sahihi. Nikatmshika baba yangu mkono na kuana kutoka naye taratibu kabisaa. Alikuwa hawezi hata kutembea haraka. Nilimvuta kwa kujikongoja mpaka tukafanikiwa kuiacha nyumba nyuma. Wakati tumefika getini ile nafungua geti nje kulikuwa na kondi la majambazi. Mbele alikuwapo Peris na wengine walikuwa wamejipanga sana. Waliniangalia kwa kiasi kisha_________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________Cheki na mimi sehemu ya 44, gonga like, share, comment ili iwafikie watu wengi wajue vile sisi hufanyaga. Nawapenda sana jmn.

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Songwe chupuchupu ATUMBULIWE na Waziri Mkuu
»
Previous
Jeshi la Polisi lauwa Wahalifu Wawili KIBITI

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...