» » Jeshi la Polisi lauwa Wahalifu Wawili KIBITI

Jeshi la Polisi nchini limefanikiwa kuwaua watu wawili  wanaosadikiwa kuwa  ni miongoni mwa wahalifu wanaoendesha mauaji katika  Kanda maalumu ya  kipolisi Rufiji ambapo  mmoja  kati ya watu hao  ametambulika  kwa jina la Abdallah Ally Ngande Makeo ambaye alikuwa anatafutwa na Jeshi la Polisi kwa muda mrefu kutokana na kushiriki  kwake katika matukio ya  mauaji maeneo ya Ikwiriri, Kibiti pamoja na uvamizi wa kituo cha Polisi Ikwiriri.

Akielezea tukio hilo,  Mkuu wa Operesheni Maalum  za Jeshi la Polisi,  Naibu Kamishna wa Polisi Liberatus Sabas alisema kuwa tukio hilo lilitokea mnamo tarehe 19, julai, 2017 saa mbili usiku katika eneo la  Utende kata ya Ikwiriri,  wilaya Rufiji kanda maalum  ya Polisi  Rufiji.

 “Askari  Polisi  wa doria  waliwatilia mashaka watu wanaokadiliwa kuwa watano ambapo walipoanza kuwafutilia ndipo walianza kukimbia huku wakiwashambulia  askari kwa risasi. 

"Askari nao kwa ujasiri walijibu   mashambulizi na kufanikiwa  kuwajeruhi  wahalifu wawili miongonio mwao ambao baadaye  walifariki  wakipelekwa Hospitali  ya Taifa ya muhimbili kutokana na kuvuja damu iliyosababisishwa na majeraha ya risasi waliyoyapata” alisema Sabas.

Aliongeza kuwa  katika eneo  hilo la tukio ilipatikana silaha moja aina ya rifle 375 ambayo  ilikutwa imekatwa kitako na mtutu ikiwa na risasi mbili (2).  Aidha, Miili ya marehemu wote wamehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti hospitali ya Taifa ya muhimbili.

 Kamanda sabas ameendelea kutoa wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kutoa taarifa zitakazosaidia kukamatwa wahalifu wengine waliosalia na kwamba  opereheni hiyo ya kuwasaka wahalifu katika Kanda hiyo ya kipolisi Rufiji  ni endelevu  na hakuna atakayebaki.


Tuma picha/ habari what-sap 0769436440




tupe maoni yako

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn news

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...