» » Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Songwe chupuchupu ATUMBULIWE na Waziri Mkuu


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amempa miezi miwili kuanzia jana Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Songwe, Bw. Elias Nawera abadili mwenendo wake kiutendaji na ashirikiane vizuri na Mkuu wa wilaya hiyo Bw. Samwel Jeremiah.

Amesema Serikali ya awamu ya Tano inawataka watumishi wote kufanya kazi kwa ushirikiano na kuheshimiana na atakayeshindwa kufanya hivyo hatavumiliwa.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo (Alhamisi, Julai 20, 2017) wakati akizungumza na watumishi wa wilaya ya Songwe akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Songwe.

Amesema watumishi wote wanatakiwa kufanya kazi kwa ushirikiano ili malengo ya Serikali ya kuwahudumia wananchi yaweze kufikiwa. Pia waheshimiane sehemu za kazi na kila mtu azingatie mipaka ya madaraka yake.

“Mkurugenzi hapa hamsikilizi Mkuu wa wilaya anaondoka kituo cha kazi bila ya kuaga na amewagawa wakuu wa Idara. Namtaka afanye mabadiliko ya utendaji wake ndani ya miezi miwili na Mkuu wa Mkoa fuatilia jambo hili.”

Pia amewaagiza Wakuu wa Wilaya wote wasimamie utendaji wa wakurugenzi wa Halmashauri kwenye maeneo yao ili kuhakikisha wananchi wanahudumiwa ipasavyo.”Serikali hii si ya mchezo. Serikali hii inahitaji watumishi waadilifu wa kuwatumikia Watanzania.”

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Bibi Chiku Galawa amesema wamejipanga kuhakikisha changamoto zote zinazoukabili mkoa zinaboreshwa pamoja na kufikia malengo ifikapo 2020.

Ametaja malengo hayo kuwa ni kuhakikisha mkoa huo unakuwa kinara katika ukusanyaji wa mapato, kila mwananchi awe na bima ya afya pamoja na kuwa na hospitali katika kila wilaya.

Kuhusu mpango wa Serikali wa kuwa na uchumi wa viwanda amesema tayari wameshaanzisha viwanda vya maziwa, kukamua alizeti ikiwa ni kuunga mkono mpango huo.

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...