» » Mtoto aliyekuwa HIV aishi bila viini hivyo kwa miaka 9


Haki miliki ya pichaMANOAFRICAImage captionWanasayansi kutoka Afrika Kusini wamebaini kwamba mtoto aliyeambukizwa virusi vya HIV ameishi kwa miaka minane na nusu bila viini hivyo.

Wanasayansi kutoka Afrika Kusini wamebaini kwamba mtoto aliyeambukizwa virusi vya HIV ameishi kwa miaka minane na nusu bila viini hivyo.

Mtoto huyo alipewa dawa za majaribio ya kukabiliana na virusi hivyo alipokuwa mdogo lakini hajapewa dawa zozote za kukabiliana na HIV tangu aingie mwaka mmoja.

Hii ni mara ya kwanza kwa mtu aliyekuwa na virusi vya HIV kuweza kuishi bila virusi hivyo barani Afrika.

Wanasayansi waliogundua kisa hicho kwa sasa wanalinda utambuzi wa mtoto huyo ambaye sasa ana umri wa miaka 9 na nusu.

Wanasema kuwa visa kama hivyo ni vichache na kwamba famili ya mtoto hyo ina furaha.

Dawa hiyo alipewa mtoto huyo wakati ambapo haikuwa swala la kawaida.

Watafiti wanaamini kupotea huko kwa virusi sio kwa sababu ya matibabu ,lakini mtoto huyo ana jeni ama kinga isiyokuwa ya kawaida ambazo zimemlinda dhidi ya HIV.

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...