» » Tanzania na Kenya kuondoleana vikwazo vya kibiashara


Image captionKituo cha mpakani kati ya Kenya na Tanzania

Mataifa ya Tanzania na Kenya yalifanikiwa kuandaa mkutano ambao utapelekea kuondolewa kwa marufuku ya bidhaa zinazoingia katika mataifa hayo mawili kutoka pande zote mbili.

Waziri wa maswala ya kigeni na ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga alitangaza uamuzi huo jijini Nairobi kufuatia majadiliano kati ya rais John Pombe Magufuli wa Tanzania na Uhuru Kenyatta wa Kenya.

Na kufuatia hatua hiyo Kenya itaondoa marufuku ya Unga wa ngano na Gesi inayoingia nchini humo kutoka Tanzania huku Tanzania nayo ikiondoa marufuku ya sigara na maziwa kutoka Kenya.

Kuongezea, mataifa hayo mawili yataanzisha kamati ya pamoja kuangazia maswala tofauti.

Mzozo wazuka upya mpaka wa Tanzania na MalawiTanzania kuitisha fidia kutoka UjerumaniAcacia yakubali kuilipa TanzaniaTanzania yamtimua mkuu wa UNDP

Uhusiano wa kidiplomasia na kibiashara kati ya Kenya na Tanzania uliathiriwa kwa muda huku mataifa yote mawili yakiweka marufuku hizo.

Marufuku ya bidhaa kutoka Tanzania kuingia Kenya ilitokana na wasiwasi wa kiusalama na ubora wa bidhaa huku Tanzania ikijibu kwa kuweka marufuku kwa bidhaa za Kenya kama vile matairi ya gari, mafuta ya kupaka mkate na maziwa.

Tanzania pia imepiga marufuku usafirishaji wa maindi kutoka Zambia kuelekea Kenya, ambayo inakabiliwa na wakati mgumu wa ukosefu wa zao hilo muhimu.

Marufuku hizo, ikilingamishwa na idadi kubwa ya bidhaa zinazotoka na kuingia katika nchi hizo zinaweza kuathiri pakubwa biashara.

Katibu wa viwanda na uwekezaji nchini Tanzania Adolf Mkenda awali alikuwa amesema kwamba hakuna hatua zilizochukuliwa kutoka Nairobi tangu mwezi Februari na Juni wakati mataifa hayo mawili yalipokubaliana kwamba marufuku hizo ziondolewe.

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...