» » Tamko la CHADEMA Kuhusu Kauli ya Mzee Mwinyi Kwamba Magufuli Awe Rais wa Tanzania Milele


Chadema imelaani vikali kauli ya Rais wa awamu ya pili, Ally Hassan Mwinyi aliyesema kuwa kama siyo matakwa ya Katiba ya nchi, uongozi wa Rais John Magufuli ulipaswa kuendelea kuwapo miaka yote.

Kiongozi huyo wa awamu ya pili ambaye alikuwa akizungumza kwenye swala ya Eid El Fitri alidai pia laiti ingelikuwa Katiba iliyopo haikufupisha muda wa uongozi wa urais, amengemshauri Rais Magufuli awe Rais wa Tanzania wa siku zote.

Akizungumzia kauli hiyo katika makao makuu ya Chadema yaliyopo Kinondoni, leo (Alhamisi) Katibu Mkuu wa Baraza la Wazee, Roderick Lutembeka amesema matamshi hayo yanapaswa kukemewa kwa vile yanaashiria kulipeleka Taifa kuandaa viongozi watakopuuza Katiba ya nchi.

“Sisi wazee wa Chadema kwa kutambua madhara ya kauli kama hizi tumeamua tusikae kimya kwani  kauli hiyo inakiuka Katiba ya nchi inayoweza kulitumbukiza Taifa katika machafuko kama ambavyo imetokea kwa nchi jirani zilizopuuza uvunjifu wa katiba,” amesema.

Amewataka Watanzania kwa ujumla kujitokeza na kupinga kauli za namna hiyo ambazo alisema zinajaribu kuwaandaa wananchi kisaikolojia ili kuwa na viongozi watakaopindisha Katiba katika siku za baadaye.

Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About IVST TANZANIA

Hi my name is Gasto Alex Didas
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...

Popular Articles