KUREJESHA mwili katika hali yake ya kawaida si kazi rahisi. Upungufu wa virutubisho mwilini, msongo wa mawazo na kukosa mood, kama inavyokuwa kwa upungufu wa vichocheo muhimu katika mwili ambavyo hutokea kutokana na umri wa mtu.
Kurejea katika hali ya kawaida si jambo rahisi kama kula aina fulani ya vyakula ili kukusaidia katika hilo. Siri ipo kwenye afya ya jumla ya mwili wako.
Unahitaji kufanya mambo yote kwa pamoja, kuongeza uzalishaji wa vichocheo (hormone), mzunguko wa damu, kupunguza mawazo na kuimarisha afya ya ubongo, mambo ambayo iwapo yatakuwa katika mwili kwa pamoja yanaweza kuathiri mood ya mtu si tu katika mambo ya chumbani bali pia katika maisha yake ya kila siku.
Ni muhimu pia kutambua kwamba upo uwezekano kwamba kuna siri ya kiafya ambayo imejificha na kuathiri mwili wa mtu na hivyo kupunguza hamu yake ya kufanya mapenzi. Kama kawaida, inapokuwa ni masuala yanayouhusu mwili wako, ni bora ukawasiliana na daktari wako kama una wasiwasi wowote.
Zifuatazo ni siri tano za kumwezesha mtu kurejesha hamu ya kufanya mapenzi.
1. Vyakula vyenye madini ya zinc kwa wingi
Vyakula ambavyo vinaweza kusaidia kuongeza hamu ya kufanya mapenzi kama chaza (ama oyster) na matunda ambayo yanawakilisha alama ya uzazi vinaweza kuwa vinavutia, lakini ni kweli kwamba vinaweza kusaidia?
Jibu ni kwamba inawezekana. Chaza ina kiasi kikubwa cha zinc, madini ambayo yanaweza kuusaidia mwili kuzalisha vichochea mbalimbali mwilini kikiwemo kile kinachofahamika kama testosterone – kiungo muhimu katika kuuweka ubongo katika utayari (mood).
Hata hivyo, tatizo kubwa la chaza ni kwamba sio kitu ambacho kinaweza kupatikana kila siku katika mlo: kwa kuwa wanahitaji kuwa wanapatikana kwa wingi katika eneo unaloishi na pia kinahitaji awe na kipato kikubwa cha fedha kwa kuwa ni chakula ambacho ni ghali sana, jambo ambalo ni vigumu kuweza kununua kila siku.
Jambo zuri ni kwamba, zinc inaweza kupatikana katika vyakula vingine kama nyama ya ng’ombe, kondoo, mboga za majani aina ya spinach, karanga na vyakula vya mbegu.
Zinc pia inasaidia kuongeza uzalishaji wa mbegu za kiume, kwa hiyo ni madini muhimu kwa ajili ya uzazi.
2. Vyakula kwa ajili ya kuongeza mzunguko wa damu
Mzunguko bora wa damu unaweza kufanya miujiza katika kuongeza hamu ya kufanya mapenzi kwa kuongeza mzunguko wa damu katika viungo vya uzazi. Vyakula ambavyo vinasaidia katika hili ni pamoja na vitunguu swaumu, pilipili na tangawizi.
Vyakula hivi vina kitu kinaitwa allicin, ambacho kinasaidia kutanua mishipa ya damu na kuondoa mafuta kwenye damu, hivyo kuifanya damu kuwa nyepesi.
Protini aina ya omega-3 ambayo inapatikana katika samaki pia inasaidia kufanya damu kuwa nyepesi na kuongeza uwezo wa kutanuka na kusinyaa (elasticity) kwa mishipa ya damu, hivyo damu kuweza kupita kwa urahisi.
Hivyo, samaki pamoja na supu yenye viungo na pilipili kiasi kizuri ni jawabu tosha kwa mtu mwenye matatizo kitandani.
3. Chakula cha ubongo kitakurejesha katika mood
Mwili kuwa na hamu ya kufanya mapenzi muda wote sio tu kwamba unasaidia kimazoezi, lakini pia afya ya ubongo inaimarika zaidi.
Kwa lugha rahisi, ni jambo gumu kuwa na hamu ya mapenzi unapokuwa una msongo wa mawazo kuhusu masuala ya kazi na mambo mengine yasiyohusiana na masuala ya chumbani.
Ubongo ni mtandao tata wa jumbe za kikemikali ambazo huitwa neurotransmitters, ambazo zinaweza kukufanya ukose raha, au uwe na furaha au motisha.
Neurotransmitters kama serotonin na dopamine zinaweza kukupunguzia mawazo, na zinahitaji protini nzuri ili kuweza kufanya kazi sawasawa. Protini za omega-3 zinaweza kusaidia kwenye hili.
Hivyo basi, ongeza matumizi ya vyakula kama nyama, samaki, mayai, jibini, maziwa mgando, kunde, karanga na mbegu. Kama unahisi kwamba hutati protini ya kutosha katika chakula chako cha kila siku, fikiria juu ya kuongeza kiasi hicho katika milo ya nyumbani kwako.
4. Usiuchoshe mwili wako kwa mawazo
Msongo wa mawazo sio tu katika ubongo, bali pia ni katika mazingira unayoishi. Unapokuwa na msongo wa mawazo mwili wako unatoa kichocheo (hormone) kinachofahamika kama cortisol, ambacho kinaweza kupunguza hamu ya kufanya mapenzi.
Matokeo haya yanayotokana na msongo wa mawazo ni njia ambayo mwili unatumia ili kujilinda kwa kuzuia uzazi wakati wa hatari.
Katika zama hizi za leo watu wengi wanakuwa na msongo mkubwa wa mawazo, jambo ambalo linasababisha uzalishaji wa kichocheo cha cortisol kuwa vigumu kuzuia. Inawekana ikawa ni vigumu kuweza kubadili staili ya maisha ya mtu ili kupunguza stress, lakini hatua ya kwanza unayoweza kuchukua ni kupunguza vyakula ambavyo vinaweza kuongeza uzalishaji wa vichocheo vya msongo wa mawazo.
Vyakula vya wanga iliyoboreshwa kama mkate mweupe na sukari ni hatari sana, kwa kuwa husaidia kuzalisha vichocheo vya mwili ambavyo vinaweza kukujaza stress na kupunguza hamu ya kufanya mapenzi na pia uwezo wa kuzaa (fertility).
Kuepukana na hilo, chagua vyakula vya wanga ambavyo havijaboreshwa kama mahindi yasiyokobolewa na ngano halisi, pamoja na kula matunda na mboga za majani kwa wingi.
5. Chocolate nyeusi
Wanawake wengi hupenda sana chocolate, na ni jambo zuri sana. Kakao (cocoa) ina utajiri mkubwa wa misombo (compounds) yenye faida kwenye mwili wa binadamu kama antioxidants zinazofahamika kama flavonoids, ambayo ina kiasi kikubwa cha madini ya chuma, na mingine mingi sana.
Muhimu zaidi, kakao ina phenylethylamine, ambayo inasisimua mwili na kuufanya uzalishe vichocheo vya dopamine na serotonin katika ubongo, kitu ambacho kinasaidia sana kupunguza stress. Tazama sehemu ya 4 hapo juu.
Kwa bahati mbaya, chocolate ambayo unanunua kutoka kwenye supermarket imejaa sukari, hivyo faida yake kiafya ni ndogo. Badala yake, unahitaji ile nyeusi kabisa, ambayo imetoka shambani. Ukishazoea kula kakao hii, ambayo ni chungu kiasi, ili kupunguza uchungu, jaribu kuongeza kiasi fulani cha unga wa kakao iliyoboreshwa katika maziwa.
N.N: Ikumbukwe pia kwamba vichocheo vya dopamine na serotonin huzalishwa kwenye ubongo mara tu baada ya kufika kileleni wakati wa kufanya mapenzi.
Mwisho … mazoezi
Mazoezi yanaweza kusaidia sana uzalishaji wa vichocheo vya mwili.
Ndoa Maridhawa
kama una Apps ya 4sn news wambie nawenzako wa download hawatajuta washauri marafiki zako au wape namba yangu niwatumie link whats-app wa download 0769436440
Masomo nengi yanakuja kila iitwapo leo
ASANTE
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment