» » Fifa yaidhinisha nafasi mpya za Afrika Kombe la Dunia

Kuwepo kwa timu 48 ilikua ni moja ya ahadi ya Gianni Infantino katika kampeni zake

Image captionKuwepo kwa timu 48 ilikua ni moja ya ahadi ya Gianni Infantino katika kampeni zake
Baraza la Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) limeidhinisha uamuzi wa kulipatia bara la Afrika nafasi tisa timu zinazoshiriki fainali za Kombe la Dunia zitakapoongezwa na kuwa 48 mwaka 2026.
Hatua hiyo iliidhinishwa Jumatano nchini Bahrain.
Bara la Afrika kwa sasa huwa na nafasi tano pekee.
Taifa la kumi kutoka Afrika litashiriki katika michuano ya muondoano ya kufuzu, itakayoshirikisha nchi sita, kuamua atakayefaidi kutokana na nafasi mbili za ziada.
Baraza la Fifa lilitangaza pendekezo lake la kwanza kuhusu mpango wa kugawa nafasi hizo 48 tarehe 30 Machi.
Hatua ya nyongeza ya timu hizo inatajwa kama sababu mojawapo ya kuonekana kwa nchi ambazo zilikuwa hazipati nafasi
Image captionHatua ya nyongeza ya timu hizo inatajwa kama sababu mojawapo ya kuonekana kwa nchi ambazo zilikuwa hazipati nafasi
Nafasi mpya zitajazwa vipi?
Afrika - 9 kutoka timu za awali 5
Asia - 8 kutoka timu 4 za awali
Ulaya - 16 kutoka timu 13 za awali
Marekani ya Kaskazini, Kati na Caribbean - 6 kutoka timu 4 za awali
Bara la Oceania - 1 kutoka timu 1 ya awali
Amerika ya Kaskazini - 6 kutoka timu 4 za awali
Historia ya Mabadiliko Kombe la Dunia
Kombe la DuniaTimu
1930 Uruguay13
1934 Italia16
1950 Brazil13
1954 Uswizi16
1958 Sweden16
1974 Ujerumani Magharibi16
1982 Uhispania24
1986 Mexico24
1998 Ufaransa32




Tuma picha/ habari what-sap 0769436440






BONYEZA HAPA KUPATA APP YA 4SN NEWS






tupe maoni yako

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...