Haki miliki ya pichaREUTERSImage captionBi Park alifikishwa mahakamani akiwa amefungwa pingu
Rais wa zamani wa Korea Kusini, Park Geun-Hye amefikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza mjini Seoul kwa tuhuma za ufisadi.
Hii ndio mara ya kwanza ameonekana hadharani tangu kuondolewa madarakani na kuzuiliwa mwezi Machi mwaka huu. Amekanusha kufanya makosa yeyote.
Rais wa zamani wa Korea Kusini ashtakiwaRais wa zamani Korea Kusini akamatwa
Bi Park alifika mahakamani akiandamana na rafiki wake wa karibu, Choi Soon-Sil ambae anatuhumiwa kwa kujipatia fedha kutoka kwa makampuni makubwa.
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGESImage captionBi Park Geun-hye (kushoto)na Choi Soon-sil (kuliat) wakiwa mahakamani
Alipofika mahakamani Park Guen-Hye aliulizwa ajira yake na kujibu hana hajaajiriwa.
Yeye na rafiki wake huyo hawakuzungumziana na walikaa kando ya mawakili wao. Rais huyo wa zamani alivalia mavazi meusi na siyo sare za wafungwa ambazo amekua akivalia gerezani.
Feri iliyozama Korea Kusini miaka 3 iliyopita yainuliwa
Alikua pia na kibandiko cha nambari yake ya mfungwa 503. Nywele zake zilifungwa kwa kipini kilichotolewa na mamlaka za gereza. Kwa sasa kiongozi huyo anakumbwa na njiya panda baada ya kuondolewa kwenye ikulu.
Haki miliki ya pichaEPAImage captionChoi Soon-sil alifikishwa mahakamani mapema mwaka huu
Mshirikishe mwenzako
No comments:
Post a Comment