» » SIMULIZI YA KUSISIMUA-NANI KACHUKUA SURA YANGU?SEHEMU YA 18 NA 19

MTUNZI NA MWANDISHI-MWL YUSUPH ABEL NG'AHALA.

Sim no, 0755683295/WatSap, Instagram @mwalim_yuu, Email@yusuphngahala@gmail.com, Fb.com/Mwalimu Yusuph Abel Ng'ahala.

SEHU YA KUMI NA NANE.
Tulipoishia Nikamwona Zabroni akiondoka kwa kutembea na suti yake ya gharama haswaa. Nilijiona mjinga nisiye na akili ninayezidiwa na watoto wa mjini. Wakati naendesha gari mara nilihisi kama kitu nyuma ya gari. Nikageuka na kuona kuna______Enda nayo.....Kama kuna vifurushi viwili hivi. Sikua na kumbukumbu ya kuweka vifurushi kwenye gari langu yaani kwenye zile siti za nyuma. Nilitaka nisimame niangalie ni nini lakini foleni ilikua inasogea hivyo ikabidi niendeshe gari. Niliendesha huku nikitafuta sehemu ya kuchepuka ili nipaki gari niangalie vile vifurushi ni vya nini! Sikupata nafasi mpaka hapo niliposimamishwa na polisi wa usalama barabarani yaani traffic wakinihitaji kwa pembeni. Baada ya kusimama wakaniuliza leseni nikawapa. Kisha wakaniuliza kazi yangu nikawatolea kitambulisho cha kazi. 

Baada ya kukiangalia wakasema samahani tunaomba kukagua gari yako. Kwa kua walikua kazini ikabidi niwaruhusu wakague tuu. Walianza kwenye buti, wakasema kuko sawa. Kisha wakaja kwenye siti za nyuma na kuniuliza vile vifurushi ni vya nini? Nikawajibu naombeni muangalie wenyewe. Kwani hata sijui vimefikaje humo. Basi traffic mmoja akaanza na mfuko wa kwanza kisha akaonekana kama aliyeshtuka sana. Nikamwuliza vipi? Akasema Afande ni nini hiki? haya si madawa ya kulevya? Nikauliza nini? Alipokua akifunua furushi la pili mshituko uliongezeka. Mungu wangu Maiti! Alitamka yule traffic. Nikasema mbona siwaelewi. Mmoja akajibu hii si gari yako? na umetuambia wewe ni askari kwa mjibu wa kitambulisho. Sasa je maiti na madawa unapeleka wapi?

Nilikua kama niliyemwagiwa maji ya baridi kwenye msimu wa baridi. Nilishindwa hata nijibu nini. Nilivuta kumbukumbu kama wakati napanda vitu vile vilikuwepo. Lakini sikupata jibu. Nikajua tuu wakati Zabroni amenizubaisha pale kwenye foleni ni hapo ndipo kuna wajinga wenzie wakaingiza madudu yao kwenye gari yangu. Nilibaki nimesimama mpaka hapo niliposikia Upo chini ya ulinzi mheshimiwa. Nilitakiwa kwenda kituoni mara moja. Nilitii amri kwani ni kweli mimi nilikutwa na hivyo vitu. Sikua na ujanja.

Moyo uliniuma afisa mzima nakamatwa na madawa ya kulevya. Zaidi maiti ya mtu. Haaa ilikua kituko haswaa. Basi nikapakizwa kwenye gari la polisi halafu yule afande mmoja akawa anaendesha gari langu. Tulifika kituoni na chaajabu ni kua nilikuta kikundi cha watu wakilia na kuonekana walikua wakinisubiri kwa shauku kubwa. Waliponiona waliinuka kwa hasira na kunivamia kwa ngumi na mateke huku wakidai nimemuua ndugu yao. Polisi wakajitahidi kuwazuia pale na mara baada ya kufanikiwa nikaingizwa kituoni. Huko nikakalishwa mkuu mmoja akaanza kwa kusema Afande yuu nakufahamu sana kwa uwajibikaji wako. Siamini haya ninayoyaona. Kisha akatoa kitu kama Cd (santuri) Akaiweka kwenye kompyuta na kunigeuzia.

Ndipo nilipojiona nafyatua risasi ovyo kwenye ile benki nilikokua nimetoka. Nilishtuka zaidi pale nilipomwona mtu akiuawa na kuburuzwa kutolewa kwa chini. Kumbe wale majambazi walichimba chini kwa chi na kutokezea kwenye benki kwa ndani. Hivyo ndo mana kikosi changu hakikuwaona. Kisha nikaonyeshwa kua yule aliyevutwa kuelekea shimoni alikua ni meneja wa benki. Aliuawa kikatili sana na ndiye aliyekutwa kwenye gari yangu. Hivyo ikaoneka mimi ndiye nilimwua na kutoka naye. Kisha nikamsikia yule afande akisema hao uliowaona hapo nje ni ndugu zake. Wana hasira na wewe sana wanajua umemuua ndugu yao.

Ilikua ni habari ya kushtusha sana kwangu. Yule aliyekua akionekana pale alikua ni Zabroni ambaye nimefanana naye kwa kila kitu. Kilichofanyika ni vibaraka wa Zabroni kuchukua tape za matukio zilizorekodiwa mle benki na CCTv kamera. Kisha wakaziwahisha polisi. Na wakati wamenizubaisha pale kwenye foleni ndipo waliingiza madawa na maiti ya yule meneja wa benki. Hivyo kwa haraka kila mtu akajua mimi ndiye niliyehusika. Haah! Kucheza na Zabroni makweka ilikua inahitaji nguvu ya ziada. Alikua mwingi wa ubunifu na udanganyifu. Alikua ana uwezo wa kulitengeneza tukio na kulifanya lionekane kweli. Hakika niliishiwa pozi. Nilibaki nimekaa nisijue chakujibu. Hakika waliniweza.

Baada ya mahojiano ya mda mrefu na kuwaeleza jinsi tukio lilivyo. Wao wakadai kua wamenielewa lakini ndugu wa marehemu hawatanielewa kwasababu na wao walipewa kopi ya ile Cd, Na aliyewapa inasemekana ni kibaraka wa Zabroni. Hakika walifanikiwa kunichafua haswaa. Hivyo hapakua na jinsi zaidi ya kuwasikiliza wao wanasema nini. Akatoka askari mmoja na kuwaomba watulie nao wakatii. Kisha akajaribu kuwaelewesha kua mimi si yule aliyeonekana kwenye CD, Kwa mara nyingine makovu yakasaidia kunitofautisha na Zabroni. Walionekana kuelewa. Wakaomba ruhusa ya kuchukua mwili wa ndugu yao. Wakachukua na kuondoka zao bila kuongea lolote.

Baada ya askari yule kurudi akasema sasa Afande yuu pole sana. Nikajibu ahsante. Kisha akasema bwana tukuombe urudi hapa kesho ili tumalize hili swala mana tunajua leo ulikua unashuhulikia swala hilo la uvamizi wa benki. Niliwashukuru sana kwa ushirikiano wao. Hakika kwenye ukweli uwongo hujitenga. Mimi sikudhani kama ningetoka nilijua ni jela tuu hakuna kingine. Niliwashukuru sana kisha nikawaomba gale madawa wateketeze kwa moto. Mimi nikaondoka huku kichwani nikiwa na mawazo sana.

Niliendesha gari huku kichwa changu kikiwa kimejaa mawazo. Nilikua namuwaza huyu Zabroni ni mtu wa namna gani. Mbona ana michezo ya hatari. Nikiwa bara barani kwa mbali nikamwona mtu kama Peris akiwa ameshikana mkono na mtu ambaye nilidhani ni Zabroni. Walikua wakielekea mlango fulani wa gesti. Nikapatwa na hasira sana nikapaki gari haraka na kushuka kuwakimbilia huku nikijiapiza kuua. Niliwakimbilia mpaka nikawakuta. Niliita jina Perisi. Hawakugeuka nikaamua liwalo na lowe nikaamua kumpapasa begani Peris mara wote wakageuka Mshituko mkubwa ukanipata kwani______ ______________________________

___________________________________________________________________________________________________________________________Utafanya jambo la msingi kama utaisubiri kwa hamu sehemu ya 19,





SEHEMU YA KUMI NA TISA.
Tulipoishia Niliwakimbilia mpaka nikawakuta. Niliita jina Perisi. Hawakugeuka nikaamua liwalo na liwe nikaamua kumpapasa begani Peris mara wote wakageuka Mshituko mkubwa ukanipata kwani____Songa sasa....Hawakua wao bali watu wengine. Samahani niliwafananisha ndugu zangu samahanini sana. Mpuuzi wewe akajibu yule mwanaume na kumvuta msichana wake wakaondoka. Nilirudi na kupanda gari. Nilifika kituoni na kukuta wale maaskari waliokua wakifanya doria wamerudi. Nikawauliza juu ya usalama wa benki.

Wakanijibu ya kua waziri wa ulinzi na usalama, pamoja na Waziri wa mambo ya ndani wapo kituoni. Niliingiwa na woga kiasi nikamwuliza askari mmoja wako wapi? Akanijibu wana kikao ukumbi wa mikutano nadhani na wewe unahitajika. Nikatoka kwa kasi kuelekea kule kwenye ukumbi wa mikutano. Niliingia na kupiga saluti kama sehemu ya heshima kwao kisha nikataka kukaa. Nikaambiwa hapana njoo ukae hapa kuna "serious issue" tunakuhitaji uwe karibu. Nikasogea kwenye kiti ninachoonyeshwa. Nilipokaa nikasikia sasa bwana Yuu, Tulikua tunakusubiri wewe hapa na kama usingefika kwa mda mwafaka tulikua tunaacha maagizo hapa. Alisema waziri mmoja. Kisha akaendelea kuanzia leo umesimamishwa kazi kwa mda usiojulikana mpaka hapo tutakapokuita wenyewe. Huenda ikawa kesho au wiki ikapita. Kakini kaa tayari mda wote sawa. Sababu za kukusimamisha ni kupisha uchunguzi dhidi yako na tuhuma zinazokukabili.

Nikakabidhiwa barua pale na kuambiwa malipo yangu nitakua napokea kama kawaida. Ila sitaruhusiwa kujihusisha na shughuli zozote za kiaskari mpaka hapo nitakapotaarifiwa upya. Kuanzia sasa vitu vyote vinavyohusika na polisi utatakiwa kuviacha na utakaporudi utavitumia. Nikutakie likizo njema afande Yuu na ahsante kwa kulitumikia jeshi la polisi la Tanzania. Unaweza ukaondoka na kutupisha hapa mara moja tuna maongezi nyeti. Hivyo ndivyo alimaliza yule Waziri na kuniacha nikiinuka kwenye kiti huku machozi yakinilengalenga .Hayakua yanatoka kwasababu nimesimamishwa kazi. Yalikua yanatoka kwasababu sikujua kwanini jambo langu limeenda haraka vile.

Kwanini sikupewa nafasi hata ya kuongea. Kosa langu ni nini? Mbona napewa hukumu isiyonihusu. Kujituma kote matokeo yake ni kusimamishwa kazi. Nilitoka huku machozi yakitirika kwa uchungu. Niliingia ofisini kwangu na kuchukua baadhi ya vitu vyangu na kuacha vifaa vya jeshi. Nikatoka na kitambulisho tuu. Laptop yangu nilichukua na pia nikabeba bastola moja kama sehemu ya kujilinda. Nilitoka nje na kuingia kwenye gari langu huku nikilia kwa uchungu. Niliwasha gari na kuanza kuelekea nyumbani. Nilitaka kumpigia simu Peris lakini simu zangu alinyang'anya Zabroni. Nikaendelea hadi nyumbani. Lakini wakati nafika na kupaki gari kuna kitu nilihisi.

Kwanza milango ya nyumba ilikua wazi kitu ambacho siyo kawaida, nikasogea kwa umakini nikaona hali ya usalama ni mbovu. Nikatoa bastola na kuingia kwa kunyata ndani mwangu. Wakati naingia sebuleni nilimkuta "housegirl" Kaegeshwa kwenye kochi huku akiwa ametapakaa damu. Alikua amenitolea macho na ulimi nje. Nikamfuata na kumtingisha kichwa. Haa mara ghafla kichwa kikadondoka! Kumbe alikua tayari kauawa kwa kukatwa kichwa. Kisha wakamrudishia na kukitegeshea. Moyo ulilipuka kwa woga kisha nikaamua kusinga ndani. Huko mlangoni nilikutana na kiatu cha Peris chenye kisigino kirfu ambacho hupendelea sana kukivaa. Nikaingia ndani ndipo nilipokuta vipande vidogovidogo vya nyama ya binadamu.

Niliuona mkono na miguu vilikua ni vya mtoto mdogo. Nikaanza kuwaza ya kua majambazi wamepita pale. Nilipoangalia vizuri ile mikono ilikua ni ya mwanangu. Kwa mara ya pili majambazi wamemuua mwanangu na dada wa kazi. Hasira zikapanda, Uso ukabadilika rangi na kua mwekundu. Nilihisi nafedheheshwa. Wakati nat afakari yale mara kwa mbele ya kitanda nikaziona simu zangu. Ilikua ni ushahidi tosha ya kua Zabroni kapita nyumbani kwangu. Nikazisogelea na kutaka kushika simu moja lakini moyo ukasita.

Nikageuka nyuma na kuinama kuokota kile kiatu cha mke wangu Peris. Wakati nakiinua nilihisi kwenye kile kisigino kuna vitu. Nikakivunja kile kisigino na kukutana na vinasa sauti vidogo sana vinne. Kumbe ndo mana mara nyingi tulikua tukipanga mipango ya kukamata majambazi wanajua kumbe walikua wametuwekea vinasa sauti. Sasa swali likaja mke wangu anajua au hajui? je kile ni kiatu chake hakuhisi tofauti yoyote? Yalikua maswali magumu ambayo nilishindwa kujijibu. Nikiwa nimeduwa huku nina uchungu wa mwanangu kuuawa, msichana wa kazi kuuawa, pia mimi kusimamishwa kazi. Hakika nilikua na kila sababu ya kua na uchungu. Sikuweza kuyazuia machozi yangu.

Nilianza kutembea kuelekea sebuleni huku nikiwa sijui cha kufanya. Mda huo wote nikawa natafakari Peris yuko wapi kwani kazini sikumwona. Nilitaka nimpigie simu lakini kwakua simu yangu iliwekwa na majambazi nilihisi huenda ni mtego. Nikaamua kuacha. Nilitoka sebuleni na kumwangalia yule mdada wa kazi hakika aliuawa kikatili sana. Moyo wangu ulikua wa simanzi kila uchwao, sikupata hata nafasi ya kufurahia maisha yangu. Nikawaza na kulaani sana. Mungu wangu Mungu wangu mbona umeniacha. Tazama mke wangu wa kwanza kafa kisa majambazi, mwanangu alilawitiwa huyu wa pili sasa kakatwa vipandevipande. Haitoshi nimesimamishwa kazi, Nini malipo ya uaminifu wangu? nini malipo ya kujituma kwangu? Aaah Mungu uko wapi? Mbona nadharirika mja wako! Mungu ni kama alikua amenisahau. Nilijikuta miguu inaishiwa nguvu na kutetemeka.

Nikakaa chini na kujiinamia nisijue la kufanya. Mara kwa mbali nikahisi simu yangu inaita kule chumbani. Nilikua naogopa kupokea lakini nilipoingia na kuona aliyekua akipiga simu ni Peris ikabidi nijitoe ufahamu na kusema ikiwa ni mtego wacha na mimi nife. Kuna haja gani ya mimi kuishi ikiwa kila kitu changu kinaangamizwa. Tayari Peris nilishaanza kumtilia mashaka. Nikajitoa muhanga na kusema potelea mbali kama ni kufa bora nife. Sina hasara hakuna anayenitegemea. Wakati huo simu ilikua bado inaita. Basi kwa kua nilikua tayari kwa lolote nikainua mkono wangu na kuelekeza ilipo simu. Kisha nikaichukua huku mkono ukitetemeka sana. Wakati nataka kubonyeza kitufe cha kupokelea Ghafla________________________

_____________________________________________________________________________ __________________________________________________Check na mm sehemu ya 20, tujue yaliyomo kama yamo. Kwa lolote nichek Fb.com/Mwalimu Yusuph Abel Ng'ahala, au Emal@yusuphngahala@gmail.com, Au Instagram/mwalim_yuu. Nawapenda wote niwatakie ujenzi mwema wa taifa letu.

Kwa llt nitafte, 0755683295, Au Instagram/mwalim_yuu, Fb.com/Mwalimu Yusuph Abel Ng'ahala. Email@yusuphngahala@gmail.com. Tupendane wote.



Naomba Msamaha kwa kuchelewesha Kama unataka ku chare na Mimi chochote karibu WhatsApp 0769436440 karibu

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...