» » Wanajeshi 100 wa Afghanistan wauawa katika shambulio

Wanajeshi 100 wa Afghanistan wauawa katika shambulio

Wanajeshi wa fghanistan wakiimarisha ulinzi baada ya wanajeshi wenzao 100 kuuawa katika shambulio la TalebanHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionWanajeshi wa fghanistan wakiimarisha ulinzi baada ya wanajeshi wenzao 100 kuuawa katika shambulio la Taleban
Maafisa wa serikali ya Afghanistan wanasema kuwa watu waliokuwa wamevalia sare za jeshi wamewaua zaidi ya wanajeshi 100 katika shambulio la kambi ya kijeshi katika mji wa Kaskazini wa Mazari Sharif.
Msemaji wa jeshi, Nasratullah Jamshidi, ameeleza kuwa watu hao walishambulia wakati wanajeshi walipokuwa wakitoka katika maombi ya Ijumaa katika msikiti kwenye kambi hiyo.
Wanajeshi wengine walilengwa katika duka lililokuwa karibu.
Kundi la Taliban lililodai kuhusika limesema kuwa watu wake walitegua vilipuzi kabla ya kuwaruhusu watu wa kujitolea muhanga kuingia katika kambi hiyo.
Mapigano yaliendelea hadi baadaye mchana na maafisa hao wanasema kuwa wanatarajia idadi ya waliofariki kuongezeka.
Karibu Wataliban kumi walifariki katika makabiliano hayo.
Serikali ya Afghanistan inayoungwa mkono na mataifa ya Magharibi inaendelea kupigana vita vinavyojikokota na Wataliban na makundi mengine ya Waislamu wenye itikadi kali.

Tuma picha/ habari what-sap 0769436440

BONYEZA HAPA KUPATA APP YA 4SN NEWS

tupe maoni yako

Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About IVST TANZANIA

Hi my name is Gasto Alex Didas
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...

Popular Articles