» » NYUMBA AMBAYO MUNGU ANAWEZA KUIBARIKI

The Power of Forgiveness
Nyumba Ambayo Mungu Anaweza Kuibariki
Kwa maana nimemjua ya kwamba atawaamuru wanawe, na nyumba yake baada yake waishike njia ya Bwana, wafanye haki na hukumu. Mwanzo 18:19.
Machoni pa Mungu, mwanamume anapimwa kwa namna alivyo kwenye familia yake. Maisha ya Ibrahimu, rafiki wa Mungu, yalitambulika kutokana na heshima ya juu kwa Neno la Bwana. Aliendeleza dini ya nyumbani. Hofu ya Mungu ilipenya nyumbani kwake. Yeye alikuwa kuhani wa nyumba yake. Aliitazama familia yake kama amana takatifu. Nyumba yake ilikuwa na watu zaidi ya elfu moja na aliwaelekeza wote, wazazi na watoto kwa Mungu Mwenye enzi. Hakukubali namna yoyote ya ukandamizaji wa wazazi kwa upande mmoja au kutotii kwa watoto kwa upande mwingine. Kwa muunganiko wa mvuto wa upendo na haki, aliitawala nyumba yake katika kicho cha Mungu na Bwana alishuhudia uaminifu wake.
Yeye, “atawaamuru…nyumba yake.” Hapakuwa na uzembe wa uovu katika kudhibiti tabia ya uovu ya watoto wake, hapakuwa na upendeleo dhaifu, usio wa hekima, unaodekeza, wala kukubali kuacha kuwajibika kwa ajili ya upendo usiostahili. Ibrahimu hakutoa tu maelekezo sahihi, lakini angelidumisha mamlaka ya sheria za haki na uadilifu.
Wapo wachache sana katika siku zetu ambao wanafuata mfano huu. Kwa upande wa wazazi wetu wengi sana ipo hali ya kuongozwa na hisia zinazopofusha au za kibinafsi, hali inayodhihirika katika kuacha watoto ambao hawajaweza kufanya uamuzi na kunidhamisha shauku zao, waendeshwe na nia zao wenyewe. Huu ni ukatili mbaya kuliko wowote kwa vijana na kosa kubwa kwa dunia. Upole kupita kiasi kwa upande wa wazazi husababisha kukosekana kwa utaratibu kwenye familia na katika jamii. Hiyo huwathibitisha vijana katika tamaa ya kufuata mwelekeo wao, badala ya kujisalimisha kwa masharti ya Mungu.
Kama walivyo wazazi ndivyo ilivyo kwa watoto kuwa ni wa Mungu ili awatawale. Kwa muunganiko wa upendo na mamlaka, Ibrahimu aliitawala nyumba yake. Neno la Mungu limetupatia kanuni kwa ajili ya kutuongoza. Kanuni hizi hutengeneza kiwango ambacho katika hicho hatuwezi kuyumba kama tunadumu katika njia ya Bwana. Lazima mapenzi ya Mungu yawe ndiyo yenye umuhimu mkubwa. Swali ambalo inatupasa tuulize siyo: Wengine wamefanya nini? Ndugu zangu watafikiri nini? Au, watasema nini juu yangu kama nikichukua mwelekeo huu? Lakini swali liwe, Mungu amesema nini? Hakuna mtoto wala mzazi anayeweza kufanikiwa kweli katika mwelekeo wowote isipokuwa katika njia ya Bwana.

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...