» » Turks & Caicos: Nchi inayoongozwa na wanawake

Turks & Caicos: Nchi inayoongozwa na wanawake


Sharlene Cartwright-Robinson ni waziri mkuu wa kwanza mwanamke nchini Turks & CaicosHaki miliki ya pichaTURKS & CAICOS WEEKLY NEWS
Image captionSharlene Cartwright-Robinson (kulia) ni waziri mkuu wa kwanza mwanamke nchini Turks & Caicos
Wanawake wengi bado hawajapata fursa ya kuchukua nyadhifa za juu katika nchi nyingi, lakini hiyo ni kinyume kwa Taifa la Caribbean la Turks & Caicos au TCI.
Mwezi Disemba taifa hilo ambalo ni koloni ya zamani ya Uingereza, lilipata waziri mkuu wa kwanza mwanamke, Sharlene Cartwright-Robinson.
Wanawake pia wanashikilia nyadhifa za naibu gavana, mkuu wa sheria, jaji mkuu, mkuu wa mashtaka na makatibu wengine watano wa kudumu, miongoni mwa nyadhifa zingine.
Kufuatia wanawake kuwalemea wenzao wa kiume, sasa jitihada zinafanywa kuwapa motisha vijana wa ili wajeza kupigania nao nyadhifa za juu.

Waliofanikiwa

Wanawake nchini Turks & Caicos walipataje mafanikio kama hayo ambayo wengi wana ndoto ya kutapata?
Waziri wa elimu Josephine Connolly (kushoto) akiwa na waichana wenye maona mazuri na wanaumeHaki miliki ya pichaTCI GOVERNMENT PRESS OFFICE
Image captionWaziri wa elimu Josephine Connolly (kushoto) akiwa na "wanawake wenye maona mazuri siku za usoni pamoja na wanaume"
Bi Cartwright-Robinson ambaye chama chake cha PDM kilipata ushindi mkubwa tarehe 15 kwenye uchaguzi wa mwezi Disemba anasema kuwa alikuwa "mwanamume bora kwa kazi hiyo"
Akifanya kampeni kwa manifesto ya haki za jamii na serikali yenye uwazi, aliwashinda wagombea wengine 52 kupata wadhifa huo.
Ushindi wake ulifikisha kikomo uongozi wa chama cha PNP wa miaka 13, wa waziri mkuu Michael Misick ambaye anakabiliwa na kesi ya ufisadi.
Anaamini kuwa wanawake hufanya kazi kwa njia inayobora.
"Wanawake huwa waaangalifu zaidi. Tunashikilia nyadhifa ambazo hatujawai na ukweli ni kwamba tunaziendesha kwa njia nzuri," Bi Cartwright-Robinson alisema.
Rhondalee Braithwaite-Knowles aliteuliwa kuwa mwanamke wa kwanza mkuu wa sheria nchini TCI mwaka 2014
Image captionRhondalee Braithwaite-Knowles aliteuliwa kuwa mwanamke wa kwanza mkuu wa sheria nchini TCI mwaka 2014
Mwezi Februari mwaka 2014 Bi Braithwaite-Knowles, aliteuliwa kuwa mwanamke wa kwanza mkuu wa sheria nchini humo baada ya kufanyika uchaguzi huru kote nchini.
Kwa sasa kati ya wanafunzi 17 kutoka TCI ambao wamepata mafunzo nchi za kigeni 14 ni wanawake.
Nyadhifa nyingi za juu za sheria nchini TCI zinashikiliwa na wanawakeHaki miliki ya pichaTCI GOVERNMENT PRESS OFFICE
Image captionNyadhifa nyingi za juu za sheria nchini TCI zinashikiliwa na wanawake

"Hakuna vizuizi"

Mkuu huyo wa sheria anasema kuwa kile ambacho kitakuwa ni changamoto ni kujaribu kutekeleza majukumu ya kimaisha kama mama kwa mtoto wake wa miaka 7 na mke.
Anasema kuwa kwa wanawake kupata nyadhifa kama hizo, wanastahili pongezi. Anasema ni vyema kuonyesha kuwa wamepata nyadhifa hizo kwa njia iliyo ya haki.
BiConnolly, Bi Cartwright-Robinson na naibu Spika Karen Malcolm wana baadhi ya nyadhifa za juu nchini humoHaki miliki ya pichaKIER ADAMS
Image captionBiConnolly, Bi Cartwright-Robinson na naibu Spika Karen Malcolm wana baadhi ya nyadhifa za juu nchini humo
Naibu Gavana Williams anakubaliana na hilo.
Wajibu wake ambao ni pili kutoka ule wa London wa John Freeman, pia ulikuwa wazi kwa wagombea kote duniani.
Naibu Gavana Anya Williams aliapishwa kwa mara ya pili Desemba 21
Image captionNaibu Gavana Anya Williams aliapishwa kwa mara ya pili Desemba 21
Wajibu wa Bi Williams unahusu kusimamia idara ya wafanyakazi wa umma iliyo na wafanyakazi 1700. Aliapishwa na kujiunga na baraza la mawaziri kwa mara ya pili tarehe 21 mwezi Disemba.
Anaiambia BBC kuwa wanawake wameishikia nyadhifa za juu kwenyr nchi hiyo ya watu 35,000, hasa katika nyanja za elimu, afya, siasa na serikali.
Caicos
Kuwa wakwanza kupata kilicho bora kutoka 4sn news tuma namba yako whatsapp 0769436440 share Read More




Mkurugenzi +255769436440

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...