» » Mkalimani akamatwa Tanzania kwa kutafsiri visivyo matamshi ya mtalii

Mkalimani akamatwa Tanzania kwa kutafsiri visivyo matamshi ya mtalii


Mkalimani akamatwa Tanzania kwa kutafsiri visivyo matamshi ya mtalii
Image captionMkalimani akamatwa Tanzania kwa kutafsiri visivyo matamshi ya mtalii

Mkalimani katika mbuga ya wanyama pori nchini Tanzania amekamatwa baada ya kutafsiri visivyo matamshi ya mtalii mmoja kuhusu nchi na watu wake.
Kwenye video iliyosambazwa kwa wingi, mkalimani huyo anasema kuwa mtalii huyo anataka watu wa Tanzania waache kulalamika kwa sababu ya njaa
Ukweli ni kwamba mwananke huyo anasema kuwa wata wa Tanzania ni wazuri kupindukia.
Alikamatwa siku ya Alhamisi kwa agizo la waziri wa utalii.
Mkalimani huyo ambaye hakutajwa jina ni kutoka mbuga ya Serengeti iliyo kaskazini magharibi mwa nchi.
Kamanda wa polisi eneo hilo Philipo Kalangi, aliiambai BBC kuwa anahojiwa lakini hakutoa habari za kina.

Watalii wengi huzuru Tanzania kuona wanyamaporiHaki miliki ya pichaAFP
Image captionWatalii wengi huzuru Tanzania kuona wanyamapori

Mwandishi wa BBC mjini Dar es Salaam anasema kuwa huenda waziri alihisi kuwa mkalimani huyo alikuwa akimsuta mtalii au alikuwa akimuiga Rais John Magufuli.
Video hiyo iliyochapishwa na gazeti la Kenya, mtalii anasema:
"Hi. Ziara yangu nchini Tanzania imekuwa nzuri. watu ni wazui na wenye urafiki. Salamu kwa kawaida ni Jambo, nina furaha kuwa hapa, Ardhi ni nzuri."
Mkalimani anatafsiri hivi:
"Anasema watanzania mnalia sana njaa, kila siku mnalia nja wakati mna maua nyumbani, si mchemshe maua mnywe, anasema si vizuri kulia njaa."
Mtalii
"Aina nyingi ya wanyama na watu unaona ni wazuri, kinyume na sehemu zingine. Ni nzuri."
Mkalimani
"Anasema mnamuomba rais wenu awapikie chakula, kwani rais wenu ni mpishi, angahikeni mfanye kazi,chemsheni hata nguo mnywe."
Mtalii
"Ni kitu mabacho utakikumbuka katika maisha yako yote. Ni nzuri na ni ya kupendeza."
Mkalimani
"Anasema mhangaikeni pembezoni za nchi, muache rais hawezi kutoka Ikulu akuje kuwapikia chakula, hivyo mjipikie wenyewe."
Kuwa wakwanza kupata kilicho bora kutoka 4sn news tuma namba yako whatsapp 0769436440 share Read More




Mkurugenzi +255769436440

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...