» » DR John Pombe Magufuli amteua mkuu mpya wa majeshi Tanzania

Magufuli amteua mkuu mpya wa majeshi Tanzania


Mkuu mpya wa majeshi nchini Tanzania Jenerali Venance MabeyoHaki miliki ya pichaIKULU YA TANZANIA
Image captionMkuu mpya wa majeshi nchini Tanzania Jenerali Venance Mabeyo
Rais John Pombe Magufuli amemteua Luteni Jenerali Venance Mabeyo kuwa mkuu wa majeshi ya Ulinzi nchini Tanzania akichukua mahala pake jenerali Davis Mwamunyange aliyestaafu.
Taarifa kutoka ikulu iliotumwa katika vyombo vya habari inasema kuwa Luteni huyo sasa amepandishwa cheo na kuwa jenerali kamili.
Mabeyo alikuwa mkuu wa kikosi cha jeshi la nchi kavu kabla ya uteuzi wake.
Wakati huohuo rais amemteua meja jenerali James Mwakibolwa kuwa mnadhimu mkuu wa majeshi ya ulinzi akichukua mahala pake Jenerali Mabeyo.Pia yeye alipandishwa cheo cha luteni jenerali.
Rais amesema kuwa uteuzi huo unaanza kutekelezwa mara moja.
Tarehe ya kuapishwa kwa wawili hao itatangazwa baadaye.
Asante kwa kutembelea Blog yetu washirikishe na wenzako, Pia tunaomba maoni yako hapa WHATSAP (+255) 0769436440 Karibu Sana Read More

Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About IVST TANZANIA

Hi my name is Gasto Alex Didas
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...

Popular Articles