» » Trump ampigia simu Xi Jinping na kukubali msimamo kuhusu China

Trump ampigia simu Xi Jinping na kukubali msimamo kuhusu China


Ni mawasiliano ya kwanza ya simu kwa viongozi hao wawili wa mataifa makuu Duniani tangu kuapishwa kwa Donald TrumpHaki miliki ya pichaAP
Image captionNi mawasiliano ya kwanza ya simu kwa viongozi hao wawili wa mataifa makuu Duniani tangu kuapishwa kwa Donald Trump
Rais wa Marekani Donald Trump amekubali kuheshimu kile anachokiita sera ya "China Moja" pale alipompigia simu Rais wa China Xi Jinping, Ikulu ya White House imesema.
Sera ya China Moja ni elimu ya kidiplomasia, kwamba kuna serikali moja tu iitwayo China.
Bwana Trump alitilia shaka sera ya muda mrefu ya china, pale alipofanya mazungumzo na Rais wa Taiwan ,mwezi Desemba.
Hiyo ni mojawepo ya hatua kubwa mno ya kuvunja tamaduni ya muda mrefu ya kufuata taratibu ya uongozi, na kuchochea malalamiko rasmi kutoka kwa utawala wa China.
Mazungumzo hayo ya simu ni ya kwanza kati ya marais hao wawili tangu Trump alipoingia ofisini Januari 20, licha ya Rais Trump kuwapigia simu viongozi wa mataifa kadhaa duniani.
Ikulu ya White House inasema kuwa maswala mbalimbali yalijadiliwa wakati wa mazungumzo hayo ya simu ambayo ilitajwa kama " mzuri sana ".
Viongozi hao wawili walialikana kuzuru mataifa yao, inasema taarifa hiyo, huku wakitarajia kuendeleza zaidi mazungumzo yao.
Taarifa kutoka Beijing zinasema kwwamba, China inampongeza Bw Trump kwa kutambua sera ya China Moja.
Mataifa haya mawili "washirika wa karibu, na kupitia juhudi za pamoja, tunaweza kuboresha Zaidi uhusiano huu na kufikisha katika kiwango cha juu zaidi katika historia", Taarifa hiyo ilimnukuu Bw Xi.
Mazungumzo hayo ya simu yalifuatia barua iliyotumwa na Bw Trump kwa Rais Xi hapo jana Ahlamisi- hatua ya kwanza ya Trump kumfikia kiongozi huyo wa China.
China imekashirishwa na maoni ya Trump kuihusu TaiwanHaki miliki ya pichaEPA
Image captionChina imekashirishwa na maoni ya Trump kuihusu Taiwan
Awali Bw Trump alisababisha taharuki kubwa mno na Beijing, wakati alipokubali mawasiliano ya simu kutoka kwa kiongozi wa Taiwan Tsai Ing-wen.
Hata ingawa Marekani ni mshirika wa karibu wa kijeshi na Taiwan, hakuna Rais au Rais mteule wa Marekani amewahi kuzungumza moja kwa moja na kiongozi wa Taiwan, kwa miongo kadhaa.
Kuwa wakwanza kupata kilicho bora kutoka 4sn news tuma namba yako whatsapp 0769436440 share Read More




Mkurugenzi +255769436440

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...