» » Mihadarati ya Cocaine ya pauni milioni 50, yapatikana Uingereza

Mihadarati ya Cocaine ya pauni milioni 50, yapatikana Uingereza


Mabegi yaliyojaa dawa za kulevya aina ya cocaine yenye kiwango cha Pauni milioni 50 yalipatikana katika fukwe mbili tofauti, UingerezaHaki miliki ya pichaNCA
Image captionMabegi yaliyojaa dawa za kulevya aina ya cocaine yenye kiwango cha Pauni milioni 50 yalipatikana katika fukwe mbili tofauti, Uingereza
Mamlaka kuu ya kukabiliana na uhalifu nchini Uingereza, imesema kuwa dawa ya kulevya aina ya Cocaine, yenye kiasi cha pauni milioni 50, imepatikana ikiwa imesombwa na maji hadi katika ufukwe wa Norfolk, Nchini Uingereza.
Zaidi ya kilo 360 ya mihadarati hiyo ilipatikana imesombwa hadi katika ufukwe wa Hopton, karibu na Great Yarmouth na ufukwe mwingine ulioko hapo karibu wa Caister.
Mwananchi mmoja alifahamisha maafisa wa polisi wa kituo cha Norfolk, baada ya kugundua mabegi yaliyokuwa na dawa hizo za kulevya katika ufukwe wa Hopton.
Maafisa wa usalama waendelea kutafuta madawa zaidiHaki miliki ya pichaNCA
Image captionMaafisa wa usalama waendelea kutafuta madawa zaidi
Polisi na maafisa wa mamlaka hiyo kuu ya kupambana na uhalifu wanaendelea kusaka maeneo hayo.
Matthew Rivers, kutoka mamlaka hiyo kuu (NCA), na askari wa kulinda mipaka ya nchi, anasema kuwa: "tunafanya kazi pamoja na kikosi cha kulinda mpaka, idara ya polisi wa pwani, na maafisa wa polisi wa kituo cha Norfolk, ili kubaini namna mifuko hiyo ilifikishwa hapo, hata hivyo ni jambo la kutamausha ikiwa kweli madawa hayo yallikuwa yakifikishwa Uingereza.
"Bila shaka hii ni shehena kubwa Zaidi ya dawa za kulevya kupatikana, na kupotea kwake ni pigo kubwa kwa magenge ya uhalifu yanayohusika."
Wapelelezi hawaamini madawa hayo yalikuwa yakipelekwa katika eneo la NorfolkHaki miliki ya pichaNCA
Image captionWapelelezi hawaamini madawa hayo yalikuwa yakipelekwa katika eneo la Norfolk
Superintended Dave Buckley, kutoka jimbo la Norfolk Constabulary, anasema: "Huku tukiamini kuwa tumepata shehena yote, raia yeyote akipata dawa zingine, tunaomba atufahamishe mara moja.
"Tunao maafisa wa ziada watakaosalia katika eneo hilo ili kuendesha uchunguzi na kufuatilia taarifa zozote ambazo zinaweza kuchipuka." Dave Buckley alisema
Kuwa wakwanza kupata kilicho bora kutoka 4sn news tuma namba yako whatsapp 0769436440 share Read More




Mkurugenzi +255769436440

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...