» » Familia yenye watu 500 yapiga picha China

Familia yenye watu 500 yapiga picha China



Familia ya Ren yapiga picha kwa pamojaHaki miliki ya pichaZHANG LIANGZONG
Image captionFamilia ya Ren yapiga picha kwa pamoja

Zaidi ya jamaa 500 wa familia moja huko China wamepiga picha ya familia.
Picha hizo zilichukuliwa wakati wa kusherehekea mwaka mpya nchini humo ambao huadhimishwa na familia kubwa na vyakula.
Mpiga picha Zhang Liangzong alipiga picha hizo kwa kutumia ndege isiokuwa na rubani karibu na eneo la kitalii la Shishe.
Aliambia BBC kwamba familia ya Ren ambayo inatoka kijijini inadaiwa kuanza miaka 851 iliopita lakini rekodi ya udugu wao haijaangaziwa kwa zaidi ya miongo minane.
Wazee wa kijiji hivi majuzi walianza kuangazia rekodi za familia hiyo na kufanikiwa kupata ndugu wengine 2000 kupitia vizazi saba, alisema Bw Zhan.
Waliadhimisha mafanikio hayo kwa kuweka mkutano mkubwa na kuweza kupata zaidi ya wanachama 500 wa familia hiyo.

Familia ya Ren katika picha iliopigwa katika eneo moja la kitaliiHaki miliki ya pichaZHANG LIANGZONG
Image captionFamilia ya Ren katika picha iliopigwa katika eneo moja la kitalii

Chifu wa kijiji hicho Ren Tuanjie ameambia chombo cha habari cha Xhinua :Sababu moja ni kuelewa kule wajukuu wetu wameenea ,kule ambako walikuwa na kule walikoishi ili kuwajua mababu zao.
Na sababu nyengine ilikuwa kuwataka wajukuu wetu kujua mizizi yao ,ili popote wendapo wasisahau kule watokako ,alisema bw Ren, ambaye antoka katika kizazi cha 26 na mabye jina lake linamaanisha kukutana upya nchini China.
Waliadhimisha mafanikio hayo kwa kuweka mkutano mkubwa na kuweza kupata zaidi ya wanachama 500 wa familia hiyo.
Kuwa wakwanza kupata kilicho bora kutoka 4sn news tuma namba yako whatsapp 0769436440 share Read More





Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...