» » IBADA YA TAREHE 11 FEB, 2017 KUTOKA KANISA LA WA-ADVENTISTA "UDOM-EAST" DODOMA- UDOM

IBADA YA TAREHE 11 FEB, 2017 KUTOKA KANISA LA WA-ADVENTISTA "UDOM-EAST" DODOMA- UDOM
SABATO YA SITA YA MWAKA NA PILI YA MWEZI WA FEBRUARI


*SOMO:* *>TUNZA ALAMA YA UKOMBOZI*
*F/KUU:* `>YOSHUA 24:14-15```
*WIMBO:* >Namba 110 {Mlango Wazi}.
 _Mlango uko wa wema, Mlango wazi huo._
_Yesu ameufungua, na hakuna kufunga._

*SADAKA:* ```LUKA 6:28```
*Na:* ~```REV; YASSINI SAHANI```~
➡ *MATHAYO 19:27-29*
Maswali ya Msingi aliyoulizwa Bwana na wanafunzi wake,.. Kwa kuwa waliacha vyote na kuamua kumfuata Bwana.
Je, tutapata nini kwako.??
Jibu: _Waliomfuata Bwana wataketi atakapoketi Mwana wa Adam katika viti kumi na viwili, wakiwahukumu kabila kumi na mbili za Israeli._
➡ *YOSHUA 2:1-20*
Tunapata fundisho gani katika kutunza alama ya ukombozi?
Yoshua aliagiza wapelelezi kuipeleleza Yeriko, na RAHABU aliwahifadhi na walipotaka kutoka kwake walimpatia alama ya Ukombozi (Kamba Nyekundu).
• Rahabu aliwaomba wale wapelelezi waliotumwa na Yoshua, wampatie Hisani kwa kuwa aliwahifadhi..
• Tena aliomba alama ya uaminifu na uponyaji wa Ngudu zake wakati wa Saa ya ukombozi.
• Nao waliahidi kumtendea kwa Hisani na Uaminifu.
• Nao walimpatia maagizo juu ya *Alama ya Ukombozi* nayo ilikuwa ni kamba iliyotumika kuwatemelemshia watu wale wawili.
• Maagizo ya wale watu ni kufuata maelekezo aliyopewa Rahabu yule Kahaba.
➡ *YOSHUA 6:21*
 Mji wa Yeriko uliangamizwa, na ukombozi wa Rahabu ulipatikana, pamoja na ndugu zake wote na vitu vyote walivyokiwa navyo.
 Ukombozi ulipatikana kwa kutunzwa kwa *Alama ya Ukombozi*.
Kuitunza Alama ya Ukombozi ni kujihakikishia ukombozi pale ambapo Bwana atakuja kuukomboa ulimwengu.
*```JE ALAMA YETU YA UKOMBOZI NI IPI?```*
➡ *YOSHUA 14:12*
 Wazishikao Amri na imani ya Yesu. Hii ndio alama yetu kuu ya ukombozi. Na kukaa kwake YESU  kuna faida gani?
➡ *KUMB. TORATI 28:1*
Kutunza na kufanya yote atuagizayo yeye. Mibaraka tele itakuwa juu yetu  kwa kila kitu.
Kumngoja na kumtafuta Bwana si kupungukiwa kwa namna yoyote ile
La! bali wamtafutao Bwana Watabarikiwa kwa kila kitu walichonacho, mashambani, kazini, mashuleni, safarini na katika nyanja zote.
_Kwa nn leo usichague kumtumikia Bwana??_
➡ *1Petro 2:9*
Bali ninyi ni uzao ulioteuliwa na Bwana, kwa ajili ya urithi wa mema yake. Aliyoyandaa kwa ajili yetu hapo atakapokuja kuwachukua walio warithi wa mji.
➡ *Daniel 12:9-10*
Wengi siku za mwisho watajitakasa na kujifanya weupe, na wabaya watatenda mabaya zaidi na kutakuwa hakuna atakayeelewa bali walio na hekima ndio watakaoelewa....
Mwisho umekaribia, dhambi imehalarishwa, mambo mapya yamefunuliwa, na dhambi imefanywa kwa namna fulani hivi kuonekana sio dhambi...
*CHAGUENI HIVI LEO NI NANI MTAKAE-MTUMIKIA*.
~Kumtumikia Bwana kunahitaji kujitoa ndani ya mioyo yetu .~
Wimbo: Namba 142; (NASIKIA SAUTI YAKO)
  _Nasikia Mwito, Ni sauti Yako;_
_Nikasafiwe kwa damu, ya kuangikwa kwako._
⚜⚜⚜ *```TUNZA ALAMA YA UKOMBOZI```*⚜⚜
*BWANA AWABARIKI SANA MNAPOTAFAKARI NENO LAKE.*

Prepared by:
*​PR: SABUYA_JR98*
*Watsapp:* +255 766 060 303.
*Facbook:* Sabuya Willy Jr.
*Instagrm:* Sabuya_jr98

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...